AN-NUUR
Na.159 Rabi' Awal 1419, Julai 24 - 30, 1998
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Mafundisho ya Qur'an

Haja ya kusimamisha maadili ya Kiislamu

Tangu Waislamu wasahau wajibu wao wa kuuongoza ulimwengu huu na badala yake kujiingiza kwenye migogoro na mapambano ya wenyewe kwa wenyewe, dunia imekuwa ikiongozwa na mifumo ya kibeberu ya mrengo wa kikristo na kiyahudi (kiliberali) au ile iliyodaiwa kuwa ni ya kikomunist na kijamaa. Kutokana na mifumo hiyo ya kitwaghuti wanaadamu wameachwa taabani kiuchumi, kisiasa, kijamii na kimaadili

Mifumo hiyo ya kibeberu imeweka sura mbaya sana duniani. Imeweka matabaka ya walionacho na wasionacho. Dunia imejaa uchoyo na uroho, chuki na mauaji, udhalimu na unafiki. Historia ya dunia iliyotawaliwa na mifumo hiyo ya kibeberu inatuonyesha kuwa imesababisha madhila makubwa duniani. Mifumo hiyo ya kibeberu ndiyo iliyoanzisha, kusimamia na kuendesha biashara ya utumwa. Mifumo hiyo ndiyo iliyopora uhuru wa nchi na watu na kuwatawala kwa nguvu. Mifumo hiyo ndiyo iliyoanzisha na kuchochea vita na mauaji. Mifumo hiyo ndiyo iliyoanzisha vita kuu ya kwanza na ya pili ya dunia. Mifumo hiyo ndiyo iliyomporomosha Mwanaadamu kutoka kwenye utu na kumrudisha chini kuliko hata wanyama. Wanaadamu wanaadhibiwa na urongo walioufuma wao wenyewe. Wanaendelea kudhurika, kutaabika na kudhalilika, kuliko kunufaika, kustawisha na kuboresha maisha yao. Kwa nini iendelee kuwepo na kupandikizwa katika vichwa vya vizazi vipya? 

Mfumo wa maisha ya Kiislamu ndio mtatuzi wa madhila haya, lengo lake si kuwalazimisha watu wote wawe waislamu, bali kuboresha hali za wanaadamu kimaaadili, kiuchumi, kisiasa na kijamii. Kuweka na kusimamia Uadilifu, haki na maendeleo ya kivitu na kiroho katika maisha yao. Ni kutokana na lengo hili la Uislamu, Waislamu wanatakiwa wafanye jitihada na harakati mbali mbali kwa mali na nafsi zao kuhakikisha kuwa dola na Serikali zinaendeshwa kwa kufuata sharia ya Allah (s.w.).

"Enyi mlioamini! Shikeni hadhari yenu (juu ya maadui zenu. Msikhadaike). Tokeni (kwenda vitani) makundi moja moja au tokeni nyote pamoja."(4:71) 

Na mna nini hampigani katika njia ya Mwenyezi Mungu na (katika kuwaokoa) wale waliodhaifu katika wanaume na wanawake na watoto- ambao husema: "Mola wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhalimu, na tujaalie tuwe tuna mlinzi anaeyetoka kwako na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anayetoka kwako. (4:75) 

Kwa hakika Lengo la Uislamu ni kuona kuwa ulimwengu mzima unakombolewa toka mikononi mwa Makafiri na unakuwa Jamhuri ya Kiislamu (World Islamic Republic):

Yeye ndiye aliyemtuma Mtume wake kwa uongofu na Dini iliyo ya Haki, ili ishinde na kuwa juu ya dini zote. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Shahidi.(48:28)

Juu 
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI 

Maoni yetu: Umakini wa Wabunge unatia wasiwasi 

AGIZO LA MANISPAA KUPEWA MAJINA YA WANAFUNZI WA KIKATOLIKI 
Na Mwandishi wetu, Morogoro 

Madai ya Ali Ameir kuhusu Chuki yakanushwa 
Na Mwandishi wetu 

AN-NUUR  kwenye Internet 

Mwanamuziki Nyota CAT STEVENS asimulia alivyosilimu 

Watakiwa kuacha kuwatuma watoto mitaani 
Na. Kassim Juma 

Kijana wa Kibarbaig aliyejitolea kupigania dini yake 
Na. Ali Njuki 
 
MAKALA: Zanzibar na tamasha la filamu
Na Said Mzee

'Waislamu wenye sisa kali'
Na. Ustaadh A. S. Fundi 

MAKALA: Maisha ya ndoa kwa Muislamu - 2
Ustaadh Khamis Suleyman Nassoro, Usangi, Mwanga - Kilimanjaro

Pongezi hizi za nini?

Mjibuni Mwinjilisti Kusupa msitukane 
Na Paskal Msemakweli

BARUA YA WAZI KWA WABUNGE

Vigogo wahusishwa na madawa ya kulevya Z'bar
Na Mwandishi Wetu

Da’awa Handeni yashika kasi
Na Ibn Muhammad

Kongamano la vijana wa Kiislamu Masjid Nuur Dar
Na Mwandishi Wetu

Mafunzo ya Quran 

Barua za wasomaji 

Mashairi - uzawa wa Mtume (S.A.W)

Habari za Madrasa 

Masomo 

Chakula na Lishe 
  

 

 
 Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita