AN-NUUR
Na.159 Rabi' Awal 1419, Julai 24 - 30, 1998
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Madai ya Ali Ameir kuhusu Chuki yakanushwa

Mama Chuki asema Waziri hakusema kweli

Na Mwandishi Wetu

MADAI ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Mh. Ali Ameir aliyoyatoa bungeni hivi karibuni kwamba mwanafunzi Chuki Athumani alikamatwa na makaratasi ya uchochezi yamekanushwa.

Akiongea na mwandishi wa habari hizi hospitalini Mwanafunzi huyo alisema kwamba amefadhaishwa na kusikitishwa sana na taarifa hizo za Waziri.

Alisema siku ya tukio alikuwa akitoka nyumbani kwao kwenda kwa ndugu zake Magomeni Kagera, alichoshtukia ni risasi inampiga na kuanguka chini na akaongeza kusema kwamba hakuwa na kipande chochote cha karatasi.

Aidha mama yake naye amekanusha kwamba amewahi kumwambia Mh. Waziri Ali Ameir kwamba mtoto wake hatarudi tena shuleni alikokuwa.

Mama huyo katika hali ya huzuni ameeleza kuwa pamoja na yote yaliyomkuta mwanawe inasikitisha kwamba bado haachwi akapata utulivu bali anazidi kusingiziwa mambo.

Ameendelea kusema kwamba inavyoelekea shutuma hizi mpya zinalenga kuwaweka mbali hata wale ambao wangetaka kumsaidia mwanawe. "Wakisikia kwamba anatuhumiwa kwa uchochezi wajiweke mbali kuepuka matatizo", amesema kwa masikitiko mama huyo.

Aliongeza kusema Mama Chuki kwamba kilichotokea ni a siku mwanawe alipofunguliwa pingu maafisa wa Wizara walimhoji endapo walimu wake Chuki wanakuja kumuona ambapo aliwajibu hapana.

Ikawa imejengwa hoja kwamba waalimu hao hawamtakii kheri mtoto Chuki.

Lakini mama Chuki anasema kwamba haoni ni vipi waalimu wake walaumiwe kutomtembelea mwanafunzi wao wakati ule ambapo hata yeye mwenyewe mama mzazi alikuwa haruhusiwi kumwona ila kwa kibali maalumu na siku akiwa hana kibali hicho huzuiwa au hughasiwa.

Mama huyo amesisitiza kwamba sio kweli kuwa amemweleza Waziri wa Mambo ya Ndani au mtu yeyote kwamba eti mwanawe hatasoma tena katika shule ya sekondari ya Al-haramain kwa sababu inafundisha mambo ya uchochezi au kashfa.
 

Juu 
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI 

Maoni yetu: Umakini wa Wabunge unatia wasiwasi 

AGIZO LA MANISPAA KUPEWA MAJINA YA WANAFUNZI WA KIKATOLIKI 
Na Mwandishi wetu, Morogoro 

Madai ya Ali Ameir kuhusu Chuki yakanushwa 
Na Mwandishi wetu 

AN-NUUR  kwenye Internet 

Mwanamuziki Nyota CAT STEVENS asimulia alivyosilimu 

Watakiwa kuacha kuwatuma watoto mitaani 
Na. Kassim Juma 

Kijana wa Kibarbaig aliyejitolea kupigania dini yake 
Na. Ali Njuki 
 
MAKALA: Zanzibar na tamasha la filamu
Na Said Mzee

'Waislamu wenye sisa kali'
Na. Ustaadh A. S. Fundi 

MAKALA: Maisha ya ndoa kwa Muislamu - 2
Ustaadh Khamis Suleyman Nassoro, Usangi, Mwanga - Kilimanjaro

Pongezi hizi za nini?

Mjibuni Mwinjilisti Kusupa msitukane 
Na Paskal Msemakweli

BARUA YA WAZI KWA WABUNGE

Vigogo wahusishwa na madawa ya kulevya Z'bar
Na Mwandishi Wetu

Da’awa Handeni yashika kasi
Na Ibn Muhammad

Kongamano la vijana wa Kiislamu Masjid Nuur Dar
Na Mwandishi Wetu

Mafunzo ya Quran 

Barua za wasomaji 

Mashairi - uzawa wa Mtume (S.A.W)

Habari za Madrasa 

Masomo 

Chakula na Lishe 
  

 

 
 Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita