AN-NUUR
Na.159 Rabi' Awal 1419, Julai 24 - 30, 1998
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
MAKALA
Zanzibar na tamasha la filamu

Kuanzia Julai 11 hadi 18 Zanzibar ilifanya maonyesho ya filamu (The Zanzibar International Film Festival) ambapo washiriki walitoka pembe mbali mbali za dunia. Jee ni nini athari ya maonyesho hayo kwa jamii ya Zanzibar, Mwandishi SAID MZEE anatufahamisha. 

Ni kinyume na sheria za maumbile mtu kupanda mti mwiba akataraji kuvuna zabibu au komamanga.

Wakati Rais Dk. Salmin Amour alipoingia madarakani mapema miaka ya tisini mbali na kukuza uchumi wa Zanzibar alitoa ahadi kwa Wazanzibari kwamba watakula zabibu na pilau toka Shangani hadi Kwamtipura.

Pamoja na ahadi hizo Dk. Salmin pia alitamka kwamba ataitumikia Zanzibar ikiwa ni sehemu ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uadilifu na kuahidi kuilinda na kuitetea katiba ya Visiwa hivyo.

Tafsiri ya neno uadilifu pengine humaanisha vitu tofauti kwa watu tofauti. Inawezekana uadilifu kwa wanasiasa ni kufanya kila hila, katika kuona kwamba anaendelea kuwepo madarakani.

Ni ukweli usiopingika kwamba wakati Dk. Salmin akiingia madarakani uchumi wa Zanzibar ulikuwa katika hali mbaya sana hivyo kulihitajika juhudi za makusudi katika kuufufua uchumi huo.

Miongoni mwa juhudi alizozichukua Dk. Salmin ni pamoja na kukaribisha au kuimarisha biashara ya utalii Visiwani hapa.

Baada ya muda sio mrefu tulitangaziwa kwamba uchumi wa Zanzibar unakuwa kwa kasi. Hilo linaweza likawa ni sawa kwa kutumia vigezo vya kuongezeka kwa pato la Taifa ukilinganisha na miaka iliyopita.

Lakini wakati serikali ikitangaza hivyo maisha ya Wazanzibari yanazidi kuhuzunisha na kutia mashaka huku ardhi yao ikiuzwa kwa wageni wasio na maadili mema, vijana wao wanatiwa wazimu kwa madawa ya kulevya, usalama wao umo mashakani kwa kuongezeka vitendo vya wizi na uporaji na mabinti zao wanazalishwa nje ya ndoa. Imani na Uislamu nao vinavuliwa na watalii wanaotembea uchi, maduka ya pombe na mabaa yanayofunguliwa kila pembe kila kukicha.

Hivi karibuni kwa lengo lile lile la kuitangaza Zanzibar kupitia utalii SMZ iliandaa tamasha la kimataifa la filamu, ambapo mbali na shughuli nyingine ngoma na michezo mbali mbali iliyowashirikisha watoto na watu wazima ilichezwa. Katika hali ambayo haikutarajiwa na Wazanzibari wengi ngoma na michezo hiyo mingi haikuwa na asili na utamaduni wa Mzanzibari, bali vilikuwa na muelekeo wa Kimagharibi hasa.

Msanii mmoja maarufu Visiwani hapa ambaye alizungumza na mwandishi wa habari hizi alieleza kwamba maonyesho mazima hayakwenda na utamaduni halisi wa Mzanzibari.

Msanii huyo msomi alidai kwamba wengi wa watu walitaraji kwamba maonyesho hayo yangeambatana na utamaduni halisi wa Mzanzibari kwa lengo la kuwaonyesha wageni kwamba Zanzibar ina utamaduni wake ili nao waweze kuiga utamaduni huo wafikapo Zanzibar.

Aliendelea kudai kwamba kwa kuendeleza utamaduni wa Kimagharibi. Zanzibar haina ilichokifanya zaidi ya kutetea utamaduni wa kigeni na kutoa picha kwamba Zanzibar haina utamaduni wake.

Msanii huyo alimtaka mwandishi wa habari hizi kuangalia kijitabu cha orodha ya mambo yaliyokusudiwa kutendwa kwenye maonyesho hayo ya filamu (1998 Programme, The Zanzibar International Film Festival July 11-18) ambapo mbele ya kijitabu hicho kuna nembo ya kampuni ya bia Tanzania (TBL) na ukurasa wa saba mna picha ya mwanamke ambaye hakuvaa sawa sawa.

Msanii huyo alitaka kujua mantiki ya kuwekwa nembo ya TBL mbele ya jarida hilo na kitendo cha kuonyesha picha hiyo inayodaiwa ya uchi kama kweli kinaendana na utamaduni wa Mzanzibari. Alimalizia kwa kudai kuwa lengo zima la maonyesho hayo limepotezwa kutokana na kuwekwa mambo ambayo hayahusiani na utamaduni halisi wa Mzanzibari.

Kufuatia maonyesho hayo ya Tamasha la Filamu kudhaminiwa na TBL, gazeti la Nipashe toleo Na. 01248 la Jumpili Julai 19, 1998 katika ukurasa wake wa 16 lina habari kwamba klabu kumi na mbili zinazoshiriki kwenye ligi kuu ya Zanzibar nazo zimeiomba SMZ iruhusu makampuni ya kutengeneza pombe yaruhusiwe kudhamini michuano hiyo. Hali hii imefuatia vilabu hivyo kugundua kwamba SMZ imetoa ruhusa kwa TBL kudhamini maonyesho hayo.

Hatua hii ya SMZ kukataza vilabu vya mpira kudhaminiwa na makampuni ya bia lakini ikaruhusu nyanja nyingine kudhaminiwa na makampuni hayo ni dhahiri inaonyesha ni jinsi gani viongozi wa SMZ walivyo wanafiki katika utekelezaji wao wa majukumu mbali mbali kwani hata kabla ya maonyesho hayo SMZ yenyewe ilikuwa inaendesha biasharfa ya pombe kwa kutumiabar zake za Kilimani, Africa House Hotel na Zanzibar Hotel.

SMZ mara kadhaa ilikwisha shauriwa kuhusiana na azma yake ya kutaka kuimarisha utalii Zanzibar pasipokuwa na sera madhubuti na yenye malengo ya mbali lakini imekuwa ikidharau ushauri huo na wale wanaothubutu kukemea hadharani ama kufukuzwa nchi au huitwa ni wapinga maendeleo na wachochezi.

Pengine linalopelekea Zanzibarf kuyafumbia macho mashauri haya ni mambo matatu. Moja ni pungufu wa fedha serikalini ambao umeipelekea Serikali kufunya chochote ambacho inakifikiria kwamba kinawseza kuwaongezea mapato. Pili siasa za upinzani ambazo zimekuwa na nguv u Visiwani kiasi cha kusababisha hadi wsahisani kuikatia misaada Zanzibar. Tatu na pengine ndio kubwa ni asilimia fulani ambayo viongozi huahidiwa pindipo watgapitisha miradi mbal mbali ya wanaodai mwekezaji.

Hili ndilo lililopelekea Zanzibar kukubali elimu ya ngono isomeshwe mashuleni kwa sababu tu wafadhili wa mradi huo walikuwa ni taasisi yenye fedha nyingi. Mambo haya kwa ujumla wsake yamesababisha kuimarishwa uhusiano wa Kimagahribi Visiwani humu kwa jina la utalii. Ardhi, visiwa na fukwe za bahari0 wanazouziowa wageni tayari zimeshaanza kuzua manung’uniko aMbayo yamewapelekea wananchi kuona kuwsa serikali yao haiwatakii heri.

Jambo kama hili lisipoangaliwa kwa makini ni agenda nzuri kutumiwa na wanasiasa. Hali halisi inayojitokeza katika jamii ni kwamba watu wsalioathirika na ukikwaji huu wa utalii wa kihuni ni wengi kuliko wanaodaiwa kunufaika.

Tayari kesi kadhaa ya kuharibiwa mabinti wa kike, kupewa mimba nje ya ndoa, kuwalevya vijana, kuwawekea mabaa hadi chini ya v ipenu vya nyumba zao na hata za mauaji ya kutisha zimesharipotiwa toka sehemu mbali mbali zenye idadi kubwa ya watalii.

Huu wote ni mzigo mkubwa kwa serikali changa kama SMZ ambayo inawategemea zaidi vijana wake wachache kwa lengo la kuwaletea maendeleo. Iwapo asilimia kubwa ya vijana wenyewe ndio hao walioathirika kwa kubwia unga na kupewa mimba nje ya ndoa ni nini taifa hili linatarajia.

Mfcumo huu wa utalii unaoendelezwe na SXMZ ni namna nyingine ya serikali kuiongezea sera mpya zaidi ya sera kadhaa ambazo tgayari0 imeshindwa kuzigekeleza.

Ni karibuni tu SMZ iliomba ijengvewe kituo cha kitibu walevi wa madamu haramu, wakati imeshindwsa kuendesha hospitali zake chache zikiwamo za wagonjwa wa akili na ukoma ambazo hiv i sasa zinaonekana kama ni magofu ya kihistoria.

Wananchi wanahamishwa kwenye sehemu zenye rutuba na kupewa wageni kujenga mahoteli, wav uvi nao hawana ruksa ya kuvua kwani v isiwa, fukwe na baadhi ya sehemu ya bahari imeshauzwa.

Ni kipindi cha karibu miaka kumi sasa toka Zanzibar ijiingize katika biashara hii ya kihuni lakini bado inaona aibu kutaja pato litokanalo na utalii huo.

Hivi sasa ni jambo la kawaida kuona vikundi vya vijana vikiuza na kubwia unga (madawa ya kulevya) hadharani katika kona za mji wa Zanzibar.Wakati utalii haujainufaisha serikali kwa chochote, tayari Serikali imejikuta inalazimishwa kufanya mambo nje ya mipango yake ili kudhibiti athari zake.

Ni muhimu kwa Viongozi wakafahamu kwamba wanachokipinga Waislamu ni Wazungu kutembea uchi, kufunguliwa maduka ya pombe, madawa ya kulevya, kuuliwa kwa maadili ya Kiislamu na mengine kama hayo ambayo ni kinyume na maadili ya Kiislamu. Yote haya yapo na yanaendelezwa ama kupewa ulinzi na serikali iliyopo madarakani.

Viongozi wetu watambue kwamba uongozi waliopewa ni dhamana tu
 

Juu 
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI 

Maoni yetu: Umakini wa Wabunge unatia wasiwasi 

AGIZO LA MANISPAA KUPEWA MAJINA YA WANAFUNZI WA KIKATOLIKI 
Na Mwandishi wetu, Morogoro 

Madai ya Ali Ameir kuhusu Chuki yakanushwa 
Na Mwandishi wetu 

AN-NUUR  kwenye Internet 

Mwanamuziki Nyota CAT STEVENS asimulia alivyosilimu 

Watakiwa kuacha kuwatuma watoto mitaani 
Na. Kassim Juma 

Kijana wa Kibarbaig aliyejitolea kupigania dini yake 
Na. Ali Njuki 
 
MAKALA: Zanzibar na tamasha la filamu
Na Said Mzee

'Waislamu wenye sisa kali'
Na. Ustaadh A. S. Fundi 

MAKALA: Maisha ya ndoa kwa Muislamu - 2
Ustaadh Khamis Suleyman Nassoro, Usangi, Mwanga - Kilimanjaro

Pongezi hizi za nini?

Mjibuni Mwinjilisti Kusupa msitukane 
Na Paskal Msemakweli

BARUA YA WAZI KWA WABUNGE

Vigogo wahusishwa na madawa ya kulevya Z'bar
Na Mwandishi Wetu

Da’awa Handeni yashika kasi
Na Ibn Muhammad

Kongamano la vijana wa Kiislamu Masjid Nuur Dar
Na Mwandishi Wetu

Mafunzo ya Quran 

Barua za wasomaji 

Mashairi - uzawa wa Mtume (S.A.W)

Habari za Madrasa 

Masomo 

Chakula na Lishe 
 

 

 
 Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita