|
|
|
Mhe. Kapuya awe ‘Min’kum’ Ndugu Mhariri. Ninamshukuru Allah (s.w.) kwa kujaalia kuwepo kwa chombo hiki, Gazeti la An-nuur, ambacho kupitia kwacho watu wote bila kujali itikadi zao (za kidini au kisiasa), rangi zao, jinsia zao na kadhalika, hupewa fursa sawa ya kutoa maoni yao. Sisi Waislamu tunafaidika zaidi kwa vile vyombo vingine vya habari hutubagua sana. Kwa kupitia gazeti hili ninapenda kuzingatia hotuba ya Waziri Kapuya aliyoitoa huko Bagamoyo wakati wa Hafla ya Maulidi ya Mtume (s.a.w.) ambayo tuliisikia moja moja kupitia redio ya taifa, Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) siku ya Jumanne, 07/07/98. Kwanza kabisa ninapenda kuiheshimu elimu yake ya ubobeaji katika fani tete aliyonayo. Mtu mjuzi si sawa na yule asiyejua (rejea Qur’an ...???). Lakini nimeshangazwa na kusikitishwa sana na kauli za Mhe. Kapuya, mtu mwenye elimu kiasi hicho. Nilitaraji angaliogopa sana kutoa kauli zile. Pamoja na kuwa mbali na Waislam, inaonyesha wazi kuwa hakuitumia vema elimu yake kufanya uchambuzi na utafiti juu ya hali halisi iliyopo na jinsi ilivyojengeka historia ya Waislam hapa Tanzania. Si mara moja wala mbili, Mheshimiwa huyu amekua akitoa kauli hizo kila anapopewa jukwaa katika hafla za Waislam. Hii ni dalili mbaya ya kutoiona nafsi yake katika dini. Kinyume na ambavyo amekuwa akifanya, angaliutumikia Uislam - kwa elimu yake na kwa kipaji chake. Ni vizuri akarejea akawa "MIN’KUM", na hili si yeye peke yake bali na wale waheshimiwa wengine Waislam ambao hawajajaaliwa fursa ya kutushutumu bila ya kujiwajibisha wao wenyewe kwanza. Historia imeonyesha wazi kuwepo kwa mikakati maalum ya kuwadhibiti Waislam hapa nchini katika fani zote za maendeleo. Maendeleo katika Uislam - kiimani (spiritual) na kimazingira (infrstractual) au maadili na huduma - yamepambanuliwa vizuri ambapo yote hayo yamechafuliwa kwa makusudi kabisa. Jitihada zozote za Waislam kuukabili uonevu huo huishia kutajwa kuwa ni ‘siasa kali’, ‘kuhatarisha amani’ au ‘vurugu za kidini’ na wahusika kuitwa kwa kejeli ‘mujahiddina’. Kwa kukosa mandeleo hayo ndiyo maana wale tuliowategemea hatuwaoni ila kama wageni rasmi kwenye minenguo ya Valentine Day, Generali Defao, mashindano (maonyesho) ya kukaa uchi n.k. wakisaidia kuua fikra ya Uislam. Ninachomkumbusha Bw. Kapuya ni kuwa hali tuliyonayo Waislam leo hii ni matunda ya mitandao maalum (conspiracies) dhidi ya Waislam iliyopo serikalini ambayo imerithiwa toka wakoloni wa kikanisa. Hivyo tumekuwa tukipandikiziwa watu na kuundiwa jumuiya (Bakwata) ambazo zitafanya kazi ya kudhibiti hatua zozote za maendeleo ya Waislam. Tunao ushahidi wa wanafiki wengi sana ambao hawana kazi ila kutekeleza mikakati ya serikali hii dhidi ya Waislam. Hawa wanakula michango na misaada yoyote ya mendeleo; aidha wamechangia kwa kiasi kikubwa kutufanya Waislam wa nchi hii kuwa Wiaslam wa maulid tu, kulakula, kaswida sana, kutojenga tabia ya kupenda kusoma, kuheshimu unyanyasji dhidi yetu, kupandikizwa fikra ya Uislam wa Utaifa, kupangiwa maimamu, kutojalishwa Sharia n.k. Haya yote yameletwa na serikali ili Waislam wasiujue Uislam wao, haki zao za kiraia na ili Kanisa liwe juu yao na waiogope serikali kama wanavyomuogopa Mwenyezi Mungu na pengine hata zaidi ya wanvyomuhofu Allah (s.w.). Ninasema ninamkumbusha Mhe. Kapuya kwa vile haiyumkiniki kuwa Athuman, tena, Alhamdulillah, mwenye elimu ya upeo wake awe hayajui haya kama sio kutafuta ‘uwenzetu’ kwa akina Julius, William na Fred. Alhamdulillah, ndio kama hivyo tumeyajua tayari sitegemei historia hii kuendelea kujirudia zaidi. Waislam sio wajinga vile inavyodhaniwa, unafiki tutauondoa tu japo gharama yake ni kubwa (lakini faida yake ni kubwa zaidi) na, Insha’Allah, siku moja tutakuwa huru kufanya ibada zetu, kupanga maendeleo ya kweli, tutaitengeneza jamii hii inayoharibika kwa kasi ya ajabu, na hatutouawa wala kupigwa misikitini tena. Baada ya mazingatio haya Bw. Kapuya bila shaka ataona wajibu wake na nafasi anayotakiwa kuchukua ili awe katika sisi kama waheshimiwa wenzake (wasio Waislam) walivyochukua au kugawana nafasi makanisani na wakaendesha mipango bila kusubiri kufuatwa. Wabillah Taufiq. ABUBAKAR MSHAM S.L.P. 35085 DAR ES SALAAM.
Polisi kujenga msikiti si hoja Ndugu Mhariri, Napenda kuchukua fursa hii kwa lengo la kuwakumbusha baadhi ya Waislamu ambao huona wana desturi ya kusahau haraka mabaya ambayo yamepita mara tu aidha kwa kupewa sifa au kwa kudanganywa ni jambo la kushangaza kwa Waislamu wa Tanzania kwa macho yetu hayaja kauka kutokana na madhila ambayo tumetendewa na Polisi hao hao ambao leo anapewa sifa ya kujenga banda. Ndugu Waialsmu jueni ya kwamba nyoka ni nyoka tu iwe nyoka huyo ametokea Umasaini au ametokea Ujapani, akitokea Usukumani au Uzaramaoni huyu atabakia kua ni nyoka tu na sumu yake itabakia palepale na ndio viyvo hivyo kwa polisi ambao mnawaona wema ati wamejenga msikiti, sasa mimi nasema kama ni mabanda tu pale Mwanza lipo na hapo Unguja lipo na lina saliwa kila siku na kila kipindi cha sala lakini utashangaza utawaona hawa hawa wanaosifiwa wakiwa nje ya Misikiti. Huo wa Newala kama nyingi mnaona wao nitafauti na Dar basi jaribuni kufanya maandamano yakupinga yale waliyo yafanya polisi wa Dar muuone Uislamu wao. Mimi ninachosema Polisi wa Unguja, Songea na Arusha wote hawa ni baba mmoja na mama moja na kama wapo wazuri . Miongoni mwao basi tuwaone kama alivyo fanya Malima na K.K. tuone au tusikie waziwazi. Ahsante. Abbas Machano Zanzibar.
Ni kweli Serikali inawapenda Waislamu Ndugu Mhariri MIMI naungana na wale wote wanaosema Serikali inawapenda Waislamu na kupigana vikali na wale wanaosema serikali haiwapendi Waislamu. Nasema hivi kwa maana kuu moja. Serikali inampenda kila atakaejiita Muislamu kwa jina, kuvaa kanzu, kofia vilemba na kufanya Maulid ila asiwe tayari kuutekeleza Uislamu kama ulivyoamrishwa na Allah. Ndio maana siku ya tarehe 7 mwezi huu wa saba, Waislamu waliopenda kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume wa watu wote Nabii Muhammad (s.a.w.) kwa kufanya maandamano kupitia barabara ya Bibi Titi Mohammed huku wakicheza na kuimba barabarani huku wakipeperusha bendela, walipewa ulinzi mkali wa polisi mpaka kuyazuia magari yasiwabughudhi na kuwalazimisha madreva wapitie Mtaa wa Lumumba. Serikali ilifanya hivi makusudi kuonyesha ni kwa kiasi gani inawapenda na kuwathamini Waislamu. Ulinzi huo uliwekwa ili kuzuia nini? Mimi bado sijapata jibu. Lakini ni Waislamu haohao wakisimama na kutumia vipaza sauti hivyohivyo wakasema Mungu ni Mmoja, hakuzaa wala hakuzaliwa, Yesi si Mungu wala si mwana wa Mungu kitu ambacho kimeelezwa ndani ya vitabu vyote vya dini yaani (Qur’an na Biblia), Serikali itapambana nao hata kwa kuwatandika risasi na kuwaua hadharani. Ukweli ni huu kama tukikubali Uislamu wetu uwe ni wa Maulid kula wali , kuvaa kanzu na vilemba vikubwa, kuvuta tasbih na dhikri basi serikali itatupa ulinzi hata wa jeshi la Wananchi na Vifaru. Yaasin Kasandalala (Farouq),
Mlokole Rashid atangaza hali ya hatari dhidi ya Waislamu Tarakea Ndugu Mhariri, Naomba japo nafasi kidogo ili niweze kuwafahamisha Waislamu. Kutokana mahubiriya Mchungaji aliyedai anaitwa Rashid alie zaliwa Tanga na alikuwa Muslamu kama anayo wadanganya watu na alisoma (TAMTA), Lamu hatimaye nchi za Arabuni. Mloloke huyo alianza kashfa dhidi ya Uislamu, kusema Waislamu wachawi, Mtume Muhammad sio Mtume, Uislamu sio dini kwa sababu yeye ameusoma. Hapo ni kaanza kuona machungu nikatafuta kanda za mihadhara nikaanza kuweka ili aweze kuelewa Uislamu. Baada alipo sikia ukweli wa mambo akaanza kutishia dhidi yangu na Waislamu wengine. Na akaenda kituo cha Polisi kutoa malalamiko kwamba Waislamu wanamkashifu kwa uchache hii ndio hali ya Rombo dhidi ya Waislamu. Kudra Mwindadi,
Ndugu Mhariri, NAOMBA nafasi katika gazeti lako la AN-NUUR nitowe pongezi zangu za dhati kwa Sheikh Bafadhil. Ni jambo la kutia moyo kusikia kama katika BAKWATA kuna wasomi waliopevuka kufikia kiasi cha kuogopa kuwa masheikh wa Serikali na kuamua kusema ukweli tena unaouma ili ulimwengu uelewe hiyo kwa BAKWATA iache mambo ya siasa ishughulikie matatizo ya Waislamu Tanzania haswa iwe mtetezi wa Waislamu. Tunachukulia kauli ya Sheikh Bafadhil iwe na changamoto kwa Bakwata katika kuchukua sura mpya ya historia . Nasoro Shabani Boga, Mbagala Dar es Salaam. |
Maoni yetu: Umakini wa Wabunge unatia wasiwasi AGIZO LA MANISPAA KUPEWA MAJINA YA
WANAFUNZI WA KIKATOLIKI
Madai ya Ali Ameir kuhusu Chuki yakanushwa
Mwanamuziki Nyota CAT STEVENS asimulia alivyosilimu Watakiwa kuacha kuwatuma watoto mitaani
Kijana wa Kibarbaig aliyejitolea kupigania
dini yake
'Waislamu wenye sisa kali'
MAKALA: Maisha ya ndoa kwa Muislamu
- 2
Mjibuni Mwinjilisti Kusupa msitukane
Vigogo wahusishwa na madawa ya kulevya
Z'bar
Da’awa Handeni yashika kasi
Kongamano la vijana wa
Kiislamu Masjid Nuur Dar
Mashairi - uzawa wa Mtume (S.A.W)
|