AN-NUUR
Na.159 Rabi' Awal 1419, Julai 24 - 30, 1998
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
AN-NUUR kwenye Internet
URL:http:/www.islamtanzania.org/an-nuur/index.html

Mapinduzi makubwa katika uwanja wa mawasiliano yamepatikana baada ya kubuniwa mawasiliano ya kutumia kompyuta kupitia utando unaounganisha kompyuta za dunia nzima yaani Internet. Tanzu ya Internet iliyotia fora sana ni ile inayoitwa "world wide web" (www), yaani utando wa dunia. Utando huu hutumia protokali maalum kuwezesha ubadilishanaji wa taarifa baina ya kompyuta za dunia nzima zilizounganishwa katika Internet. Kwa njia hii, taarifa au mafaili ya kompyuta yaliyohifadhiwa katika kompyuta moja yanaweza kufikiwa na kusomwa kutoka kwenye kompyuta nyingine popote pale duniani. Haya ni mapinduzi ya aina yake ya mawasiliano yanayofanya usambaaji wa habari kuwa rahisi na wa kasi kubwa. Wataalamu wanaeleza kuwa hii ni nyenzo muhimu sana katika kukabiliana na karne ya ishirini na moja Miladiya ambayo inaelezwa kuwa ni karne ya sayansi na teknolojia.

Maendeleo haya ya mawasiliano yakitumiwa vilivyo yanaweza kuleta ufanisi mkubwa katika da’wa na juhudi za kupambana na ueneaji wa dhana potofu. Na kadiri tunavyoendelea kuishi katika wakati huu wa mlipuko wa mawasiliano, ndivyo inavyokuwa ni lazima kwa wanada’wa kushajiisha matumizi ya njia za kisasa kabisa za mawasiliano, ikiwemo njia ya Internet.

Kwa kuzingatia umuhimu huu, juhudi zimefanywa kwa kuanzisha kituo cha Internet (web site) kwa ajili ya taarifa za Kiislamu na Waislamu wa Tanzania kilichopewa jina la Islam Tanzania. Mahali hapa panaweza kufikiwa kwa anuani hii: http://www.islamtanzania.org/.

Malengo makuu na ya muda mrefu ya mradi wa Islam Tanzania ni:- 

  • Kuwa kituo cha rejea kwa ajili ya taarifa sahihi zinazohusu Waislamu wa Tanzania kwa jamii ya kimataifa
  • Kuwa jukwaa la Waislamu wa Tanzania kutoa maoni yao na kubadilishana habari kuhusiana na matukio mbali mbali yanayogusa maisha na maendeleo yao
  • Kuwa fursa ya kuwasiliana miongoni mwa Waislamu wa vituo mbalimbali. 

  • Miongoni mwa taarifa zilizomo ni pamoja vitabu vyote vya Ahmed Deedat, vitabu vyote vya Sahihi Bukhari, tafsiri mbalimbali za Qur'an, anuwani za Taasisi mbalimbali za Kiislamu duniani, kaseti za Qur'an (ukitaka kusikiliza).

Katika kurasa za kituo hiki, kutakuweko na mkusanyiko wa makala zilizoandikwa kuhusiana na masuala mbali mbali juu Uislamu na Waislamu wa Tanzania kama vile Historia, Siasa, Elimu, Uchumi na matukio ya kila siku ya kijamii. Baadhi ya makala ambazo zinaweza kusomwa na watakaopitia mtandao huo katika anuani tuliyoitaja nni hizi zifuatazo: Waraka wa Abu Aziz wa kurasa 53 kwa lugha ya Kiingereza na Waraka wa Abu Azizi kwa lugha ya Kiswahili.. Jengine la kufurahisha ni kuwa kituo hiki kinahifadhi katika Internet toleo la Gazeti la AN-NUUR kila wiki. Anuani ya ukurasa wa AN-NUUR ni hii ifuatayo: http://www.islamtanzania.org/an-nuur/index.html. Kwa hatua hii ya kuliweka Gazeti la AN-NUUR katika internet, inatarajiwa kuwa ujumbe wake utaweza kuwafikia watu wengi zaidi ndani na nje ya Tanzania. Tayari matoleo kadhaa ya AN-NUUR yamo na yameshaanza kusomwa ulimwenguni kote.

Utekelezaji wa malengo ya mradi wa Islam Tanzania unahitaji ushirikiano wa kila Muislamu wa Tanzania mwenye fursa na nia ya kuitambulisha dini na jamii yake ya Kiislamu. Kwa hivyo, mchango wa makala unakaribishwa kutoka kwa mtu yeyote mwenye kuwatakia mema Waislamu wa Tanzania. Aidha, Watanzania wote wenye fursa za mtandao wa Internet kupitia mtandao huo na kutoa maoni yao ili kuboresha huduma zilizokusudiwa. Yoyote atakayependa kuchangia au kutoa maoni yake juu ya yale yanayopatikana katika kurasa za Islam Tanzania awasiliane na AN-NUUR au na wahudumu wa kituo cha mtandao kwa anuani hii ya Internet: webmaster@islamtanzania.org.

Juu 
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI 

Maoni yetu: Umakini wa Wabunge unatia wasiwasi 

AGIZO LA MANISPAA KUPEWA MAJINA YA WANAFUNZI WA KIKATOLIKI 
Na Mwandishi wetu, Morogoro 

Madai ya Ali Ameir kuhusu Chuki yakanushwa 
Na Mwandishi wetu 

AN-NUUR  kwenye Internet 

Mwanamuziki Nyota CAT STEVENS asimulia alivyosilimu 

Watakiwa kuacha kuwatuma watoto mitaani 
Na. Kassim Juma 

Kijana wa Kibarbaig aliyejitolea kupigania dini yake 
Na. Ali Njuki 
 
MAKALA: Zanzibar na tamasha la filamu
Na Said Mzee

'Waislamu wenye sisa kali'
Na. Ustaadh A. S. Fundi 

MAKALA: Maisha ya ndoa kwa Muislamu - 2
Ustaadh Khamis Suleyman Nassoro, Usangi, Mwanga - Kilimanjaro

Pongezi hizi za nini?

Mjibuni Mwinjilisti Kusupa msitukane 
Na Paskal Msemakweli

BARUA YA WAZI KWA WABUNGE

Vigogo wahusishwa na madawa ya kulevya Z'bar
Na Mwandishi Wetu

Da’awa Handeni yashika kasi
Na Ibn Muhammad

Kongamano la vijana wa Kiislamu Masjid Nuur Dar
Na Mwandishi Wetu

Mafunzo ya Quran 

Barua za wasomaji 

Mashairi - uzawa wa Mtume (S.A.W)

Habari za Madrasa 

Masomo 

Chakula na Lishe 
 

 

 
 Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita