|
|
| Mwanamuziki
Nyota CAT STEVENS asimulia:
Yote ninayokusudia kuyasema tayari mnayafahamu
yote (yaani mafundisho ya Uislam), kuthibitisha kile ambacho tayari mnakijua
nao ni ujumbe wa Mtume (s.a.w) aliopewa na Mwenyezi Mungu - nayo ni Dini
ya kweli. Sisi kama wanaadam tumepewa akili na wajibu ambavyo vinatufanya
tuwe bora kuliko viumbe wengine. Mwanaadam ameumbwa awe Khalifa wa Mwenyezi
Mungu katika ardhi hii na ni muhimu kwetu kutambua haja ya sisi wanadam
kujitenga na yale yote yenye kupotosha ili maisha yetu hapa duniani yawe
ni matayarisho kwa ajili ya maisha ya kesho akhera; na yeyote atakayechezea
maisha haya basi asitarajie kuwa atapata maisha mengine [hapa duniani]
kwa sababu imekwisha semwa ndani ya Qur’an el Majid kuwa wakati mwanadamu
atakapoletwa Siku ya Hukumu (Kiyama), atasema, "Ee Mola, turejeshe [duniani]
na utupe umri mwingine [ili tutende yaliyo mema]" Naye Mola atasema, nikikurejesheni
(duniani) mtafanya vile vile (uovu/uasi kama mwanzo).
Makuzi yangu ya Awali kidini Nililelewa katika ulimwengu huu wa kisasa wa anasa tele na maisha ya kujifakharisha. Nilizaliwa katika familia ya kikristu lakini sisi (Waisaaml) tunafahamu kuwa kila moto huzaliwa katika dini yake ya asili ambayo ni Uislam), bali ni wazazi wake ndio ambao humgeuza kuwa dini hii au ile [mbali na Uislam] [hivyo] nami nilipewa dini hii (Ukristu) na nikakua hivyo. Nilifundishwa kuwa Mwenyezi Mungu yupo, lakini hakuna mawasiliano ya moja kwa moja na Mwenyezi Mungu, hivyo ni lazima upitie kwa Yesu, na kwa kweli Yesu ndiye mlango kwenda kwa Mungu. Kwa kiasi fulani niliikubali dhana hii, lakini sikuikubali kijumla jumla. Nilikuwa nikiziangalia sanamu za Yesu; baadhi
yake zilikuwa na mawe tu na wala zisizo na uhai "Na walipokuwa wakisema
kuwa Mungu ni watatu, ilinichanganya zaidi lakini sikuweza kuhoji. Niliamini
kwa kiasi fulani, kwa sababu ilinibidi kuihesimu imani ya wazazi wangu.
Nyota wa Muziki wa Pop Kidogo kidogo nilianza kujitenga na makuzi malezi ya dini hii, nilianza kupiga muziki. Nilitaka niwe mwanamuziki nyota (mashuhuri). Mambo yote yale niliyoyaona katika filamu na pia katika vyombo vya habari yalinivutia sana, na pengine nikawa ninafikiria kuwa huyu ndiye mungu wangu (jambo hili ndilo ninalotakiwa nilitumikie katika maisha yangu), lengo langu likawa ni kujipatia fedha nyingi. Nilikuwa nina ndugu wa baba yangu ambaye alikuwa na gari zuri sana "Saafi", nilijisemea, "amefanikiwa", alikuwa na pesa nyingi. Watu waliokuwa karibu yangu walinifanya nione kuwa hivyo ndivyo mambo yalivyo, (mambo ya) ulimwengu huu ndio ilikuwa Mungu wao. Nikaamua kuwa haya ndiyo yatakuwa maisha yangu, kujipatia pesa nyingi, kuishi maisha ya ‘maraha’. Viigizo vyangu ikawa ni wanamuziki nyota wa muziki wa Pop, nilianza kutunga nyimbo, lakini ndani ya nafsi yangu nilikuwa nina hisia za utu, hisia kwamba nikipata utajiri nitawasaidia wanaadam wenye matatizo (lakini, kama isemavyo katika Qur’an wanadamu huwa tunachukua ahadi, (ya kutoa katika njia ya Mwenyezi Mungu, lakini tunapofanikiwa huking’ang’ania kile tulichojaaliwa na kukifuja kwa uroho). Kilichotokea ni kwamba nikawa mtu maarufu sana,
nilikuwa ningali kijana mbichi (teenager), jina langu na picha zangu
vilitamba katika vyombo vyote vya habari. Walinikuza kuliko hali halisi
nami nikapenda hivyo, na njia pekee ya kufnya hivyo ni kuwa mlevi (wa pombe
na vidonge).
Kulazwa Hospitalini Baada ya mwaka mzima wa mafanikio ya kifedha na maisha ya ‘maraha’, nilijikuta nimeambukizwa ugonjwa wa T.B (Kifua kikuu) na nikalazimika kulazwa hospitalini. Hapa ndipo nilipoanza kutafakari. Ni nini kilikuwa kinanitokea?. Hivi mimi ni mwili tu na lengo langu katika maisha ilikuwa ni kukidhi tu mahitaji ya mwili huu?. Nikabaini kuwa janga hili (ugonjwa wa T.B) ilikuwa ni rah’ma niliyopewa na Allah, ilikuywa ni fursa ya kunifungua macho, "kwa nini nipo hapa, kwa nini nipo kitandani, na nikaanza kutafuta majibu. Wakati huo nilitokea kuvutika sana itikadi za kimashariki nikaanza kusoma na jambo la kwanza nililokuja kuwa hadhari nalo ni kifo na kwamba roho haifi bali huendelea kuwepo. Nikajihisi kuwa nimeanza kushika njia ya heri na mafanikio makubwa kabisa. Nikaanza kufanya meditation na kula mboga za majani tu. Nikawa ninaamini juu ya dhana ya "amani na nguvu ya ua" na hii ilikuwa ni jambo la ujumla. Lakini nilichokuja kuamini hasa ni kuwa mimi sikuwa mwili tu, na hadhari hii ilinijia pale hospitalini. Siku moja nilikuwa ninatembea na mvua ikaanza kuninyeshea. Nilikimbilia sehemu kujihifadhi na hapa ikanibanikia, "Hebu kidogo, mwili wangu unalow", mwili wangu unaniambia ninalowa. Hii ilinifanya nifikirie msemo kuwa mwili ni kama punda ambaye inabidi afundishwe ni wapi anatakiwa kwenda, vinginevyo punda huyo atakupeleka kule anakotaka yeye kwenda. Nikabaini kuwa nina hiyari, ambayo ni zawadi tunayopewa na Mwenyezi Mungu. Kutoka dini ya Mashariki [Uislam] nilikuwa nikisoma habari mpya iliyonihimiza kufuata yale ayapendayo Mwenyezi Mungu. Mpaka wakati huo nilikuwa nimechoshwa na Ukiristu. Nikaanza tena kupiga muziki na safari hii ni muziki ambao ulitoa fikra na hisia zangu mwenyewe. Ninakumbuka maneno moja ya nyimbo zangu usemao, "Afadhali ningejua, afadhali ningejua ni nini kinachounda Pepo, ni nini kinachounda Jahanamu". Hivi nitakufahamu wewe (uliyeumba Pepo na Jahanamu) nikiwa kitandani pangu, au nikiwa katika chumba cha mahabusu kilichojaa vumbi hali ya kuwa (watu) wengine wanafaidi katika hoteli kubwa kubwa’, [kwa fikra hii kuniingia akilini] hapa nikafahamu kuwa nipo katika Njia Sahihi (Dini ya Kweli). Pia niliandika wimbo mwingine ‘Njia ya Kumjua Mwenyezi Mungu’. Nikatokea kuwa maarufu zaidi katika ulimwengu wa muziki. Kwa kweli nilikuwa na wakati mgumu kwa sababu nilikuwa ninazidi kutajirika na kupata umaarufu na wakati huo huo nikihangaika kujua haki kisha nikafikia mahali ambapo niliona kuwa itikadi ya kibuddha ndiyo sahihi na bora kuliko zingine, lakini bado sikuwa tayari kuachan na mambo ya kidunia na sikuwa tayari kuwa mtawa na kujitenga na jamii. Nikajaribu kuipitia tena Biblia lakini sikuweza
kupata cha kunifaa. Wakati huo sikuwa nikijua lolote juu ya Uislamu, kisha
nikatokewa na kile ambacho mimi nilikiona kama ni muujiza.Kaka yangu aliwahi
kutembelea msikiti mmoja huko Jerusalem na alivutiwa sana na hali iliyokuwepo
hapo, kwa upande mmoja msikiti huo ulionyesha uhai (kwa mahudhurio makubwa
mno ya maumini tofauti na makanisa na masinagogi ambayo yalikuwa matupu),
na kwa upande mwingine ni hali ya utulivu na amani iliyotawala mahali hapo.
Qur’an Ndugu yangu huyo aliporudi London, alileta tafsiri moja ya Qur’an, ambayo alinipa mimi. Yeye hakuwa amesilimu, lakini alionyesha kuhisi(kubaini) kitu ndani ya Uislamu, na alifikiri mimi nami ninaweza kubaini kitu. Na nilipokipokea kitabu hicho [Qur’an] ambacho ni mwongozo mbao ungenifafanulia kila jamb; Mimi ni nani? Ni nini lengo la maisha? Uweli ni upi na ni kweli ipi itadumu, na ni nini asili yangu?) Hapo nilibaini kuwa hii ndiyo Dini ya Kweli - dini si katika maana ambayo watu wa Magharibi (wasio Waislamu) wanaelewa, maana ambayo kwao wao dini ni kitu cha wazee tu. Sikuwa mshabiki, bali awali nilikuwa nimekanganyikiwa kati ya roho na mwili. Baadaye nilibaini kuwa mwili na roho havikutengana na ukitaka kuwa mcha-Mungu si lazima uende milimani, [bali] yatupasa kufuata amri ya Mwenyezi Mungu na hapo tutapata daraja kubwa [ya ubora] zaidi hata ya malaika. Kitu cha kwanza nilichotaka kujua ilikuwa ni kuwa Muislamu (kusilimu). Nilibaini kuwa kila kitu ni mali ya Mwenyezi Mungu, ambaye yeye usingizi haumshiki. Ndiye Yeye aliyeumba kila kitu. Baada ya kubaini hivi, fahari niliyokuwa nayo ilianza kunitoka kwa sababu mpaka hapa niliona kuwa Mwenyezi Mungu hakuniumba hivi hivi (pasipo lengo maalum) bali lengo la kumbwa kwangu ilikuwa ni kujinyenyekeza kwa kufuata mafundisho yaliyo sahihi na kamili ambayo ndiyo dini tunayoifahamu ya Al-Islam. Kufikia hapa nilianza kuitambua imani yangu, na kwa kuisoma Qur’an nilijihisi kuwa mimi nilikuwa ni Muislmu. Hivi sasa nimebaini kuwa Mitume wote walioletwa na Mwenyezi Mungu walileta ujumbe ule ule. (Ikiwa ni hivyo) kwa nini basi Wayahudi na Wakristo watofautiane? Nikafahamu jinsi Wayahudi walivyomkataa Yesu kuwa ni Masihi na kwamba walikuwa wamebadili neno la Mwenyezi Mungu. Hata Wakristo hawaelewi mafundisho ya Mwenyezi Mungu na wanamwita Yesu kuwa ni mwana wa Mungu. [Hakika] kila kitu (ndani ya Qur’an) kilionyesha kuwa ni cha maana (manufaa) sana. (Basi) huu ni uzuri wa Qur’an; inakutaka wewe kutazama mambo kadhaa na (kisha) kutafakari, na sio uabudu jua au mwezi bali umwabudu Yeye Mmoja (s.w.) ambaye ameumba kila kitu. Qur’an inakutaka uangalie jua na mwezi na maumbile ya ulimwengu kwa ujumla. Je unaona ni jinsi gani jua linatovyofautiana na mwezi? . Umbali toka duniani mpaka katika jua na umbali toka duniani mpaka katika mwezi ni tofauti lakini vitu hivi viwili kwetu sisi vinaonekana kuwa na ukubwa sawa sawa, na wakati mwingine kimoja huonekana kukizidi kingine. Hata pale wanaanga mbalimbali wanapokwenda anga za juu, wakaona jinsi anga ilivyo kubwa mno na dunia ikaonekana ni kitu kidogo sana kikielea ndani ya anga hiyo, huwa wanabadilika na kuwa wacha-Mungu sana, kwa sababu huwa wameona Dalili za [kuwepo kwa] Allah. Nilipoisoma zaidi Qur’an, nilikuta inazungumzia
sala, huruma na kutoa sadaka. Nilikuwa bado sijawa Muislam, lakini nilijiona
kuwa jibu sahihi la masuala yangu ni Qur’an, na Mwenyezi Mungu ameniletea,
nikaihifadhi vizuri. Lakini Qur’an hiyo hiyo inazungumzia watu wa daraja
tofauti tofauti. Nikaanza kuielewa Qur’an katika daraja nyingine (yaani
daraja la waumini), ambapo Qur’an inasema, "wale waliioamini wasifanye
makafiri kuwa ni marafiki zao na waumini (wao kwa wao) ni ndugu". Hivyo
kufikia hapa nikatamani kukutana na ndugu zangu Waislam.
Kusilimu Kisha niliamua kusafiri kwenda Jerusalem (kama alivyofanya ndugu yangu). Huko Jerusalam, nilikwenda msikitini na kuketi chini. Mwanamume mmoja aliniuliza shida yangu. Nilimuambia kuwa mimi ni Muislam. Akaniuliza jina langu nikamwambia ‘Stevens’. Alikanganyikiwa. Kisha nilijiunga na wengine tukaswali ingawa sikuswali sawa sawa. Niliporudi mjini London, nilikutana na dada mmoja akiitwa Nafisa. Nilimweleza ninataka kusilimu na alinielekeza katia msikiti wa New Regent. Hii ilikuwa ni mwaka 1977, kiasi cha mwaka mmoja na nusu baada ya kuipata ile Qur’an. Sasa nilibaini kuwa ni lazima niondokane na fahari niliyokuwa nayo, niepukane na Iblis na nielekee upande mmoja tu (kufuata Uislam). Hivyo siku moja ya Ijumaa, baada ya sala ya Ijumaa nilikwenda kwa Imam na nikatamka shahada (kalima) mikononi mwake. Mimi hapa ni mtu niliyejitwalia sifa kemkem na utajiri (kama mwanamuziki). Lakini kutaka uongofu kulinifanya nitapetape na sikutulia mpaka nilipoonyeshwa Qur’an. Sasa ninaona ninaweza kuwasaliana na Mwenyezi Mungu moja kwa moja tofauti na hali ilivyo katika Ukristu na pia katika dini zingine. Kama alivyopata kunieleza mama mmoja wa Kihindu, ‘wewe huwaelewi Wahindu, sisi tunamwamini Mungu mmoja, [bali] tunavitumia vitu hivi (sanamu) kwa ajili tu ya kupata mazingatio’. Kile alichokuwa akisema mama huyu ni kwamba ili kumfikia Mungu yampasa mtu kuunda washirika [wa Mungu], na masanamu hayo ndiyo yana lengo hilo. Lakini Uislam umeondoa vikwazo hivi vyote, [na ] kitu pekee chenye kumtofautisha mu’umini na kafiri ni Salat. Huu (Salat) ni utaratibu wa mtu kujitakasa. Mwisho ninapenda kusema kuwa kile ninachokifanya [nimekusudia] ni katika kutafuta radhi za Allah, na ninakuombeeni mpate imani [zaidi] kutokana na historia hii ya maisha yangu. Kadhalika ninapenda kusisitiza kuwa sikuwahi kukutana na Muislam yeyote [kwaajili ya mazungumzo ya dini] kabla sijasilimu. Nilisoma Qur’an na nikabaini kuwa hakuna mtu aliyemkamilifu, [isipokuwa] Uislam NDIO KAMILI na kama tukiigiza mwenendo wa Mtukufu Mtume (s.a.w.) tutafaulu. Tumuombe Allah atupe uwongofu tufuate njia [mwenendo] wa Umma wa Muhammad (s.a.w). Ndugu yenu katika Uislam Yusf Islam (Kabla ya kusilimu akiitwa Cat Stevens) *** **** ***
|
Maoni yetu: Umakini wa Wabunge unatia wasiwasi AGIZO LA MANISPAA KUPEWA MAJINA YA
WANAFUNZI WA KIKATOLIKI
Madai ya Ali Ameir kuhusu Chuki yakanushwa
Mwanamuziki Nyota CAT STEVENS asimulia alivyosilimu Watakiwa kuacha kuwatuma watoto mitaani
Kijana wa Kibarbaig aliyejitolea kupigania
dini yake
'Waislamu wenye sisa kali'
MAKALA: Maisha ya ndoa kwa Muislamu
- 2
Mjibuni Mwinjilisti Kusupa msitukane
Vigogo wahusishwa na madawa ya kulevya
Z'bar
Da’awa Handeni yashika kasi
Kongamano la vijana wa
Kiislamu Masjid Nuur Dar
Mashairi - uzawa wa Mtume (S.A.W)
|