|
|
|
Na. Ustaadh A. S. Fundi Waislamu wanaruhusiwa kufanya hivyo kwa kauli ya Allah (s.w.) katika Quran Takatifu isemayo:- :Basi pigana katika njia ya Allah. Hukalifishwi ila nafsi yako (uwezo wako). Na wahimize Waislamu (waende) huneda Allah akauia mashamulio ya waliokufuru. Na Mwenyezi Mungu ndiye mkali wa kushambulia na mkali wa kuadhibu". Suratun Nisaa (4:84). Endelea... Tumekwishaona kuwa nia hasa ya Wanatawhiid, ambao ni Waislamu wacha-Mungu ni kuleta amani, utuliv u, umoja, mshikamano miongoni mwa Waislamu wenyewe na wafuasi wa dini nyinginezo. Na kwa kufanya hivyo wamechagua kupinga aina zote za dhuluma, unyanyasaji, ugomvi, dharau, ukiukaji sharia, uvunjaji katiba, na maovu yote yawayo. Lakini kinyume kabisa na nia hii nzuri ya wanatawhiid; wapo watu waliokula njama kuwateza nguvu waumini hawa kwa kuvuruga juhudi zao zote nzuri, kwa makusudi kabisa. Kuna watu binafsi waliojitolea kushindana na Wacha-Mungu hawa; yapo pia makundi ya watu, vyama, taasisi, mashirika, na mataifa yenye nia hiyo hiyo. Nia ya njama zao ni kuwadhulumu Wanatawhiid hawa wasipate fursa ya kutumia haki yao ya kuulingania Uislamu kikamilifu. Katika njama yao hiyo wametunga, kama tulivyoeleza katika sehemu ya mwanzo ya makala haya, majina mabaya mabaya na kuwapachika Wanatawhiid hawa. Wanawaita "mujahidina" kwa maana ya Waislamu wanaoeneza dini yao kwa nguvu ya upanga na ugomvi bila ya kuwa na hoja zenye nguvu. Au kuwaita "Waislamu wa siasa kali", wakiwa na maana ya Waislamu wasiopenda amani bali fujo na vurugu tupu. Wengine huwaita "Waislamu wenye itikadi kali" wakimaanisha Waislamu wanaong’ang’ania mafunzo ya Kiislamu ya kizamani, yaliyopitwa na wakati. Baadhi yao huwaita "fundamentalists" walikuwa na maana ya watu wenye kushikilia"dogma." Mambo yanayoaminika tu kibubusa bila kuwa na maelezo yenye mantiki juu yake. Lakini kwa matumizi za makala hii nimechagua kujenga hoja zangu na uchambuzi wangu wa kina juu ya maana ya "fundamentalists" kama ilivyotolewa na kiongozi wa ngazi ya juu kabisa wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania. Nimechagua kukita hoja zangu kwake kwa sababu inawakilisha vizuri dhana potofu ya kambi ya Wapinzani wa Tawhiid kama nitakavyofafanua katika nukta kadhaa huko mbele. Neno "fundamentalist" au "fundamentalism" lilianza kutumiwa na wanasiasa Ulimwenguni mara baada ya Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia, mwaka 1922 huko Ulaya. Tazama: "Websters Ninth New Collegiate Dictionary" (1984). Neno hilo lilipewa Wakristo wanaofuata fikra za Kiprotestanti za kusisitiza ufafanuzi wa kimsingi wa maandiko ya asili ya Biblia, ambayo ndiyo uti wa mgongo wa mafunzo ya maisha ya Kikristo. Wataalamu wa historia ya thelojia wanaeleza kuwa: Msimamo huu wa "kifundamentalist" ulitokana na misimamo ya Martin Luther (1983-1546); aliyekuwa kasisi wsa Kijerumani aliyehoji mambo mbalimbali ya imani na ibada za Kikatoliki. Baada ya kukosa majibu ya kuridhisha viongozi wa juu wa Kanisa Katoliki walimfukuza "ukasisi" na "kumvua" ukatoliki. Akawa "excommunicated" na akaitwa "protestant" (aliyeasi, aliyekana, aliyekaidi, aliyekataa) wa Kanisa Katoliki. Martin Luther, aliandika kitabu kiitwacho: "Here I stand" kuelezea misimamo yake ya kukana mambo yasiyo na msingi wa maandiko ya Biblia yanayofanywa na viongozi wa Kanisa Katoliki. Na tangu hapo mlango wa uhuru wa mawazo katika dini ukafunguka na matokeo yake ndio kuzaliwa kwa mapote na madhehebu (denominations) mbalimbali katika dini ya Kikristo. Kanisa la mwanzo ndilo hilo Kanisa la Kilutheri lilliloanza 1521, na mengine mengi yakafuata baadaye na hadi leo bado yanazaLiwa. Kwa hiyo, kutokana na ukweli huu wa kihistoria; ni Waprotestanti (Wakristo wasiokuwa Wakatoliki) ndiyo wenye asili ya "ufundamentalism" na ndiwo hasa "fundamentalists." Lakini kwa kuwa kanisa Katoliki linawafuasi wengi zaidi duniani kuliko makanisa mengineyo; limejipa haki kukosoa fikra zote za kidini zinazopingana na fikra za viongozi wa kanisa Kakatoliki. Popote walipo watakosolewa, wawe "Jehova Witness", Wagidioni, Walokole, Wasabato, au wengineo wasiokuwa hao. Na pia kwa kuwa Wakatoliki wana serikali kuu ya Kanisa mjini Vaticano (Ialia) yenye nguvu kubwa juu ya majimbo yake kote duniani, bila kujali mipaka ya kijiografia; limeweza kuathiri maamuzi mengi ya kisiasa duniani kote. Miongoni mwa mataifa yaliyoathirika na fikra hii ya "fundamentalism" ni taifa la Marekani. Taifa hili limeshabikia sana neno hili, hadi limeweza kushawishi kimabavu mataifa mengine makubwa kufuata misimamo yake. Marekani, kwa kutumia jeuri ya utajiri ulionao, teknolojia ya kisasa na jeshi lenye silaha za maangamizi, limejipa "upolisi" na "skauti mkuu" na "mlinzi" wa hicho kinachoitwa "demokrasia". Marekani imejipa usimamizi wa kuilinda demokrasia isiharibike, bali iendeshwe kama wanavyotaka wao. Na ndiyo hawa (Marekani) waliolipa maana mbaya sana neno "fundamentalism", na ndiyo "waliolihamisha (transplanted) mahali pake na kuwapachika Wanatawhiid, Waislamu wacha-Mungu ambao ni wanaharakati, wenye nia nzuri ya kuleta amani na utulivu duniani. Machoni mwa Marekani na washabiki wake, "fundamentalists" ni Waislamu wagomvi, waharibifu, wauaji, wamwaga damu burebure, wasiopenda maendeleo, wasiopenda demokrasia, wanaopenda vitisho (intimidation), kutia wasiwasi watu (terrorists). Hii ndiyo tafsiri mpya ya neno "fundamentalism." Kwa maana hii hii, ndiyo maana viongozi wa Kikatoliki na makanisa mengine humu nchini wamekuwa wakali sana dhidi ya serikali yetu kuishinikiza iwadhibiti Wahubiri wa Kiislamu na hasa wafanyao "mihadhara ya Biblia", wakiwadhania kuwa ni "fundamentalists." Nasema "wakiwadhania kwa vile, wahubiri hawa hawana lolote la "ufundamentalism". Kwani, watu wa mihadhara hawana lengo lingine ila kuwarejesha Wakristo katika maandiko ya asili. Na mada zao ni pamoja na; Dini Moja, Mungu Mmoja, Utume wa Nabii Issa, Kufufuka kwa Yesu, Dhambi ya Asili, Uislamu Ndani ya Biblia, "Utoto" wa Yesu kwa Mungu, Usahihi (authenticity) wa Biblia nakadhalika. Kanisa Katoliki hapa nchini limeweka wazi kabisa msimamo wake juu ya "Uislamu kama dini" na "Waislamu wenye msimamo mkali". Soma jinsi kasisi mashuhuri sana alivyojenga fikra zake dhidi ya Waislamu wenye isfiqama (stounch) ambao ni wacha-Mungu Wanatawhiid na wanaharakati anasema: "Katika kutafakari historia ya uhusiano kati ya Ukristo na Uislamu, ni sharti kuzingatia tofauti iliyopo kati ya Uislamu kama dini na Waislamu wenye msimamo mkali wa kidini (Muslim Fundamentalists). Kwa Waislamu wenye msimamo mkali wa kidini: uchumi, siasa na dini ni mambo yasiyoweza kutenganishwa. Ndiyo sababu kila mahali unaposhamiri Uislamu wenye msimamo mkali Matokeo ni chokochoko dhidi ya dini nyingine, uhasama na mauaji ya wote wenye kuleta upinzani iwe katika dini, siasa au uchumi." (msisitizo ni wangu). ....itaendelea toleo lijalo
|
Maoni yetu: Umakini wa Wabunge unatia wasiwasi AGIZO LA MANISPAA KUPEWA MAJINA YA
WANAFUNZI WA KIKATOLIKI
Madai ya Ali Ameir kuhusu Chuki yakanushwa
Mwanamuziki Nyota CAT STEVENS asimulia alivyosilimu Watakiwa kuacha kuwatuma watoto mitaani
Kijana wa Kibarbaig aliyejitolea kupigania
dini yake
'Waislamu wenye sisa kali'
MAKALA: Maisha ya ndoa kwa Muislamu
- 2
Mjibuni Mwinjilisti Kusupa msitukane
Vigogo wahusishwa na madawa ya kulevya
Z'bar
Da’awa Handeni yashika kasi
Kongamano la vijana wa
Kiislamu Masjid Nuur Dar
Mashairi - uzawa wa Mtume (S.A.W)
|