AN-NUUR
Na.159 Rabi' Awal 1419, Julai 24 - 30, 1998
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
MASHAIRI
Uzawa wa Mtume Muhammad (s.a.w.)
 

Bismillahi Karima, mwanzoni nalitamka,
Jina lake Muadhama, Mola aliyetukuka,
Mwenye wingi wa neema, na huruma kadhalika,
Umefika twakumbuka, uzawa wa Muhammad.

Sikuye ya kuzaliwa, Muhammad imefika,
Kote inashangiliwa, Dunia inachemka,
Mtume tuloletewa, uzaziwe twakumbuka,
Umefika twakumbuka, uzawa wa Muhammad.

Kumi mbili iligota, wenye ndovu ule mwaka,
Ni mwezi mfungo sita, kazaliwa kule Makka,
Nuru yake ikimeta, kama taa akiwaka,
Umefika twakumbuka, uzawa wa Muhammad.

Ni Mtume Muhammad, mjumbe asiye shaka,
Ametumwa na Wadudi, umma uje nasihika,
Naye kafanya juhudi, Uislamu wawika,
Umefika twakumbuka, uzawa wa Muhammad.

Muhammad nuru njema, katushushia Rabuka,
Tena kwetu ni Rehema, hana wa kufananika,
Mtume mwenye hekima, na sifa za kutosheka,
Umefika twakumbuka, uzawa wa Muhammad.

Muhammad hakuacha, Islamu kumeguka,
Waziwazi hakuficha, kutupa mwanga haraka,
Katufundisha kumcha, Rabi anayepasika,
Umefika twakumbuka, uzawa wa Muhammad.

Muhammad kiigizo, tumwige pasi kuchoka,
Ametuletea nguzo, tano zinahesabika,
Halali na makatazo, humo hayakufichika,
Umefikatwakumbuka, uzawa wa Muhammad.

Kumbukumbu nzuri kwake, ni ibada kuzishika,
Wanaume Wanawake, tuzingatie mipaka,
Mipaka tusiivuke, Mwenyezi akaudhika,
Umefika twakumbuka, uzawa wa Muhammad.

Tama twaomba Rabia, mjaze nyingi baraka,
Maswahaba wake pia, wape ya kunufaika,
Nasi tuongoze njia, ya kwenda pa kuongoka,
Umefika twakumbuka, uzawa wa Muhammad.

Kassim Miraji,
S.L.Posta 25578,
DARE SALAAM.
 

Juu 
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI 

Maoni yetu: Umakini wa Wabunge unatia wasiwasi 

AGIZO LA MANISPAA KUPEWA MAJINA YA WANAFUNZI WA KIKATOLIKI 
Na Mwandishi wetu, Morogoro 

Madai ya Ali Ameir kuhusu Chuki yakanushwa 
Na Mwandishi wetu 

AN-NUUR  kwenye Internet 

Mwanamuziki Nyota CAT STEVENS asimulia alivyosilimu 

Watakiwa kuacha kuwatuma watoto mitaani 
Na. Kassim Juma 

Kijana wa Kibarbaig aliyejitolea kupigania dini yake 
Na. Ali Njuki 
 
MAKALA: Zanzibar na tamasha la filamu
Na Said Mzee

'Waislamu wenye sisa kali'
Na. Ustaadh A. S. Fundi 

MAKALA: Maisha ya ndoa kwa Muislamu - 2
Ustaadh Khamis Suleyman Nassoro, Usangi, Mwanga - Kilimanjaro

Pongezi hizi za nini?

Mjibuni Mwinjilisti Kusupa msitukane 
Na Paskal Msemakweli

BARUA YA WAZI KWA WABUNGE

Vigogo wahusishwa na madawa ya kulevya Z'bar
Na Mwandishi Wetu

Da’awa Handeni yashika kasi
Na Ibn Muhammad

Kongamano la vijana wa Kiislamu Masjid Nuur Dar
Na Mwandishi Wetu

Mafunzo ya Quran 

Barua za wasomaji 

Mashairi - uzawa wa Mtume (S.A.W)

Habari za Madrasa 

Masomo 

Chakula na Lishe 
 

 

 
 Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita