|
|
|
Na. Kassim Juma Wito umetolewa kwa baadhi ya waalimu wa madrasa Jijini kuacha tabia ya kuwatuma wanafunzi wao kuzunguka mitaa mbali mbali kwa lengo la kuomba pesa zinazodaiwa kuwa za ujenzi na uendelezaji wa madrasa hizo. Wito huo umetolewa na Waislamu kadhaa waliofika ofisi za gazeti hili wiki hii kueleza hisia zao kuhusiana na hali iliyoshamiri hivi sasa Jijini. Akizungumza kwa uchungu baada ya kuwaona watoto kadhaa wa madrasa wakiwa wamebeba visanduku wakipita mitaani katikati yaJiji,Ustaadh Mahmoud mkazi wa Ilala amesema tabia hiyo sio nzuri na inaaibisha Uislamu. Aidha Ustaadh huyo amesema kwamba amefadhaishwa mno kuwaona watoto wenye umri kati ya miaka minane (8) na 15 wakiranda mitaani huku wakiwa wamebeba visanduku vichwani. Ameongeza kusema kuwa visanduku hivyo vilivyofungwa kwa kufuli vina matundu juu yake ambayo wachangiaji hutumbukiza pesa kupitia humo. Imeelezwa kuwa baada ya makusanyo ya pesa ya siku nzima, visanduku hivyo hupelekwa kwa waalimu ambao imedaiwa kuwa ndiyo wenye funguo za kufuli hizo. Katika waraka ambao ameuandika kuelezea jambo hili na ambao nakala yake aliiwasilishwa gazeti hili, Ustaadh Mahmoud ameileza hali hiyo kuwa ni ya kuudhalilisha Uislamu na kwamba hadhani kama wazazi wa watoto hao wanafahamu lolote. "Parents bring their children to madrassa to have them educated and teachers accept them for that purpose", ameandika ustaadh huyo kwa lugha ya Kingereza akiwa na maana kwamba wazazi huwapeleka watoto wao madrassa ili wakapate elimu na walimu huwapokea watoto hao kwa lengo hilo. Akizungumzia taabu wanazozipata watoto hao katika zoezi hilo la ukusanyaji wa pesa, ustaadh Mahmoud amezitaja kuwa ni pamoja na kutembea umbali mrefu juani kupitia maduka mengi iwezekanavyo. Amesema kuwa watoto wanafanya kazi hiyo nzito huku wakiwa na njaa, kiu na uchovu hali ambazo ameeleza huathiri afya zao, masomo na tabia kwa ujumla. Ustaadh Mahmoud amesema katika utafiti wake kuhusu jambo hili amegundua kwamba pamoja na ugumu wa zoezi hilo makusanyo hayo huambulia kiasi kidogo sana cha pesa ambacho hakizidi shilingi 1500 kwa siku. Ustaadh Mahmoud amewataka Waislamu hususan wale wenye wasaa wa mali kuchangia ili kuboresha madrasa sambamba na kuwawezesha waalimu kuendesha maisha yao. "Waalimu wanabuni mbinu hizi ili kuwawezesha kuhudumia vyema madrasa zao, tusimamishe hali hii kwa kupeleka michango na sadaqa zetu kila mara, amesisitiza Ustadh huyo. Aidha ameiomba Juwakuta itayarishe orodha ya madrassa zote Jijini ili watakaokuwa tayari kutoa sadaqa na michango wasipate ugumu na ili iweze kufika kwa walengwa kwa urahisi. Vile vile amekitaka chombo hicho kiwe na utaratibu wa kutembelea madrasa mara kwa mara ili kujua maendeleo yaliyofikiwa na matatizo yanayozikumba. |
Maoni yetu: Umakini wa Wabunge unatia wasiwasi AGIZO LA MANISPAA KUPEWA MAJINA YA
WANAFUNZI WA KIKATOLIKI
Madai ya Ali Ameir kuhusu Chuki yakanushwa
Mwanamuziki Nyota CAT STEVENS asimulia alivyosilimu Watakiwa kuacha kuwatuma watoto mitaani
Kijana wa Kibarbaig aliyejitolea kupigania
dini yake
'Waislamu wenye sisa kali'
MAKALA: Maisha ya ndoa kwa Muislamu
- 2
Mjibuni Mwinjilisti Kusupa msitukane
Vigogo wahusishwa na madawa ya kulevya
Z'bar
Da’awa Handeni yashika kasi
Kongamano la vijana wa
Kiislamu Masjid Nuur Dar
Mashairi - uzawa wa Mtume (S.A.W)
|