AN-NUUR
Na.159 Rabi' Awal 1419, Julai 24 - 30, 1998
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
TAHARIRI

Serikali ijibu tuhuma hizi

Wiki iliyopita gazeti hili liliripoti juu ya hali ya wasiwasi iliyojitokeza mjini Morogoro baada ya wananchi kuona nakala ya barua inayowaagiza wakuu wa shule za msingi kupeleka majina ya wanafunzi Wakatoliki kwa Mkurugenzi wa Elimu.

Wasiwasi wa wananchi hao umejengeka juu ya dhana kwamba huenda agizo hilo likawa linahusiana kwa namna moja au nyingine na mitihani ya darasa la saba inayotarajiwa kufanywa hivi karibuni.

Kabla ya tukio hili Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu lilikuwa limemwandikia barua Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kuhoji kuwepo taarifa kwamba Kanisa Katoliki lina Tume ya Mageshi ya vita, mpaka leo Mhe. Waziri Bw. Ali Ameri hajajaaliwa kupata fursa ya kujibu.

Lakini jingine ni kwamba agizo hili la Mkurugenzi wa Elimu kwa waalimu wakuu (ambalo limetekelezwa bila kuhoji) linakuja wakati ndio kwanza Waislamu wanarejea kutoka maziarani (Makaburini) kuwazika wenzao waliopigwa risasi pale Mwembechai baada ya Paroko wa Kanisa Katoliki kuikemea na kuiagiza Serikali iwachukulie hatua wale aliodai kwamba wanamtukana Yesu.

Aidha agizo hilo limekuja huku wananchi wakishuhudia Kadinali Pengo kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki nchini akipewa ulinzi, na itifaki ya kiserikali katika ziara zake mikoani.

Yote haya kwa ujumla wake yanakuja katika mazingira ambayo tayari yapo malalamiko toka kwa Waislamu kwamba wamedhulumiwa na kunyimwa haki zao; lakini pia yanatokea katika mazingira ambayo tayari utafiti na machapisho ya wataalamu mbali mbali kama yale ya Dk. John Sivalon yanaonyesha kwamba Kanisa Katoliki lina hadhi ya pekee katika serikali kiasi kwamba wakati mwingine ni vigumu kutofautisha lipi ni la kanisa na lipi ni la Serikali.

Hayapo mengi ya kusema juu ya hali hii; lakini labda kukumbusha tu kwamba vikao rasmi vya chama vilikaa na vyombo vya habari kuzua zogo Waziri mmoja ambaye ni Marehemu sasa alipotoa dokezo kwamba mfumo wa elimu uchunguzwe kuona ni kwanini sehemu moja ya jamii inaonekana kuwa nyuma. Aliitwa mdini na kuandamwa.

Wakati wakiyatafakari yote haya, wanasubiri ufafanuzi, maelezo, majibu na kauli ya serikali.

Wakati wamekumbwa na wasiwasi juu ya hatma ya watoto wao walio katika shule za msingi, tunarejea kauli yetu kwamba Waislamu wameuliwa na wauaji wapo mtaani hawajakamatwa. Watoto, wazee na mama zao wameteswa na kudhalilishwa, wahusika hawajafikishwa mahakamani au kuwajibishwa.

Maadhali Serikali yetu imedai kwamba haina dini haimdhulumu wala kumuonea mtu na kwamba ni Serikali ya Uwazi na Ukweli inayofuata sheria. Sifa zote hizi zinalazimisha kuwepo kwa Tume ya uc hunguzi juu ya madai ya Waislamu na wale waliowaua Waislamu wakamatwe wafikishwe mahakamani.

Juu 
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI 

Maoni yetu: Umakini wa Wabunge unatia wasiwasi 

AGIZO LA MANISPAA KUPEWA MAJINA YA WANAFUNZI WA KIKATOLIKI 
Na Mwandishi wetu, Morogoro 

Madai ya Ali Ameir kuhusu Chuki yakanushwa 
Na Mwandishi wetu 

AN-NUUR  kwenye Internet 

Mwanamuziki Nyota CAT STEVENS asimulia alivyosilimu 

Watakiwa kuacha kuwatuma watoto mitaani 
Na. Kassim Juma 

Kijana wa Kibarbaig aliyejitolea kupigania dini yake 
Na. Ali Njuki 
 
MAKALA: Zanzibar na tamasha la filamu
Na Said Mzee

'Waislamu wenye sisa kali'
Na. Ustaadh A. S. Fundi 

MAKALA: Maisha ya ndoa kwa Muislamu - 2
Ustaadh Khamis Suleyman Nassoro, Usangi, Mwanga - Kilimanjaro

Pongezi hizi za nini?

Mjibuni Mwinjilisti Kusupa msitukane 
Na Paskal Msemakweli

BARUA YA WAZI KWA WABUNGE

Vigogo wahusishwa na madawa ya kulevya Z'bar
Na Mwandishi Wetu

Da’awa Handeni yashika kasi
Na Ibn Muhammad

Kongamano la vijana wa Kiislamu Masjid Nuur Dar
Na Mwandishi Wetu

Mafunzo ya Quran 

Barua za wasomaji 

Mashairi - uzawa wa Mtume (S.A.W)

Habari za Madrasa 

Masomo 

Chakula na Lishe 
 

 

 
 Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita