AN-NUUR
Na.159 Rabi' Awal 1419, Julai 24 - 30, 1998
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Kijana wa Kibarbaig aliyejitolea kupigania dini yake

Na. Ali Njuki

Tanzania ni nchi yenye eneo kubwa na ina makabila mengi. Kuna makabila yaliyoendelea kijamii na kiuchumi pia, lakini tunayo makabila machache mpaka sasa hivi hayajawa tayari kushirikiana na wenzao kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya aina yeyote.

Mfano mzuri ni kabila la Watindiga ambao huishi katika milima iliyopo Wilayani Karatu na Mbulu Mkoani Arusha. 

Kabila hilo halishughuliki kwa kilimo wala ufugaji bali wao ni wataalamu wa uwindaji na jambo lolote la maendeleo kwao ni mwiko, kwani hula mizizi ya mimea na nyama wanazowinda huko maporini.

Pia kuna Wabarbaig, hawa shughuli yao kubwa ni ufugaji na kwasababu hiyo ya ufugaji lazima kuhamahama ili kukidhi haja ya malisho na maji ya mifugo yao.

Tofauti na Watindiga, Wabarbaig wao wanapenda maendeleo yoyote yale. Tunao Madaktari, wanauchumi, wakulima pia tumekuwa hata na Maustadhi. Hilo si ajabu kwetu kwani Qur’an ilishatuambia kuwa, "Haya ni maelezo yaliyowazi kwa watu (wote) na uongozi na mawaidha kwa wamchao. (Mwenyezi Mungu) (3:138).

Ustadh Rashid Sera ni mmoja kati ya vijana wa kabila hili waliopania kuendeleza Uislamu kwa hali na mali kama anavyoeleza allipokuwa akiongea na mwandishi wsa habari hizi huko kijijini Qang’nded - Mang’ola Wilayani Karatu ambapo kuna Wabarbaigv wengi. "Ndipo huku kuwafikishia ujumbe ndugu zangu Wabarbaig kwani tangu nimeanza shughuli hizi za Daa’wa sijafika huku na vijijini wanahitaji Wahadhiri zaidi kuliko mjini kwenye wahadhiri wengi", alimaliza.

Akizungumzia jinsi alivyosilimu na matatizo aliyoyapata baada ya kusilimu Ustadh Rashid alisema, "Nilisilimu kwaka 1988 pale Keko Mwanga kwa wahadhiri wa kikundi cha Al-mallidi mbele ya ustadh Mazinge na wenzake. Lakini kilichofuatia kutoka kwa Ndugu yangu ni kupigwa, kulazimishwa kunywa pombe na kubwa zaidi ni siku moja aliamua kuniua kabisa. Lakini Allah alinisaidia nikasalimika, hata hivyo ndugu yangu aliniambia hakuna Mwislamu kwenye ukoo wetu wa Qawog’."

Ustadh Rashid baada ya miaka minne ya mateso, manyanyaso toka kwa ndugu yake ambaye anaendesha Bar na mgahawa ndani ya Uwanja wa Sabasaba Kilwa Road Dar es Salaam, aliondoka na kuhifadhiwa katika msikiti wa Kipata kwa miezi miwili kabla ya kuhamia kwa Bw. Mohamed Yusufu Dodoma na baadaye kuanza masomo ya dini kwa Sheikh Nassoro Bhacho Zanzibar kabla ya kujiunga na shughuli za Dawa ambazo ndizo anazofanya sasa.

"Nimefanya Daawa sehemu nyingi lakini sitoacha kwani ndiyo kazi yangu isipokuwa nategemea kuendelea na masomo nikipata mdhamini", alisema ustadh.

Juu 
 

YALIYOMO
 
 

TAHARIRI 

Maoni yetu: Umakini wa Wabunge unatia wasiwasi 

AGIZO LA MANISPAA KUPEWA MAJINA YA WANAFUNZI WA KIKATOLIKI 
Na Mwandishi wetu, Morogoro 

Madai ya Ali Ameir kuhusu Chuki yakanushwa 
Na Mwandishi wetu 

AN-NUUR  kwenye Internet 

Mwanamuziki Nyota CAT STEVENS asimulia alivyosilimu 

Watakiwa kuacha kuwatuma watoto mitaani 
Na. Kassim Juma 

Kijana wa Kibarbaig aliyejitolea kupigania dini yake 
Na. Ali Njuki 
 
MAKALA: Zanzibar na tamasha la filamu
Na Said Mzee

'Waislamu wenye sisa kali'
Na. Ustaadh A. S. Fundi 

MAKALA: Maisha ya ndoa kwa Muislamu - 2
Ustaadh Khamis Suleyman Nassoro, Usangi, Mwanga - Kilimanjaro

Pongezi hizi za nini?

Mjibuni Mwinjilisti Kusupa msitukane 
Na Paskal Msemakweli

BARUA YA WAZI KWA WABUNGE

Vigogo wahusishwa na madawa ya kulevya Z'bar
Na Mwandishi Wetu

Da’awa Handeni yashika kasi
Na Ibn Muhammad

Kongamano la vijana wa Kiislamu Masjid Nuur Dar
Na Mwandishi Wetu

Mafunzo ya Quran 

Barua za wasomaji 

Mashairi - uzawa wa Mtume (S.A.W)

Habari za Madrasa 

Masomo 

Chakula na Lishe 
 
 

 
 Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita