|
|
|
Na Ibn Muhammad Imefahamika kupitia Sheikh wa Wilaya Sheikh Abubakar kuwa uhamasishaji kwa ajili ya Uislamu wilayani Handeni katika sku za karibuni umeshika kasi vizuri. Akitoa mfano, amesema kwa sasa msikiti mkuu wa Chanika umeteua vijana 6 ili wazunguke katika vijiji vya jirani na mji wa Handeni ambako hali imeonekana kudorora. Ili kuepuka kusumbuliwa Sheikh alikataa kuwataja majina vijana hao. Katika msikiti huo huo kuna darsa la watoto ambao hufundishwa mambo mbali mbali kama vile Imani, Hadithi na Tawhid. Pia kila jioni akinamama nao hukusanyika katika darsa lao. Kutokana na shughuli hizo imeelezwa na Sheikh Abubakar kuwa tayari katika baadhi ya vijii Waislamu wameanza kukataa kuswalishwa na maimamu wenye kuvaa hirizi. Wakati huo huo habari kutoka Maulid ya mji ya kuzaliwa Mtume s.a.w. tarehe 6 mwezi wa saba, zinaeleza kuwa Maulid hayo yalifana sana. Katika hadhara hiyo Ustadh Hamim Ali Boza na Ustadh Ali Adam walipewa jukumu la kuiamsha jamii. Kwa upande wao waliwataka Waislamu kuhamasika katika kutikia miito ya Kiislamu sawa na vile walivyoitikia kwenda kwenye Maulid ya Bagamoyo ambapo magari kumi ya abiria yalikodiwa kwa kila mmoja kutoa shilingi 7,000. Utayari wa kuchangia ulitakiwa usiishie kwenye kusafiri kuitia wito tu bali hata katika ujenzi wa vituo vya jamii vya Kiislamu kwenye maeneo yao pia. Waislamu wa Chanika walipewa changamoto ya wao
pia kuwa huru kuitangaza imani yao kama ambavyo Wakristo wamefanya kwa
kuchnga bao na kuliandika Yesi ni Mfalme wa Chanaika ambalo lipo kwa muda
katikati ya mji.
Na Mwandishi Wetu Vijana wa Wakiislamu nchini waahidi kuendeleza mapambano dhidi ya wanao dhulumu haki zao, hayo yalisemwa na v ijana waliokutana katgika kongamano mkaalum lilifanyika katika Msikti wa Sinza kuanzia Julai 9-11, 1998. Wakitoa salamu zao katika kongamano hilo, wawakilishi wa vijana toka mikoa mbalimbali walisisitiza Waislamu kutokurudi nyuma katika kupambana na dhulma nchini na kuahidi kuulinda ushindi waliokwisha upata. Akizungumza katika kongamano hilo, ustadhi Ilunga Kapungu kutoka Mwanza alisema kwamba msimamo ulioonyeshwa na v ijana katika matukio mbalimbali ni ushindi unaostahiki kulindwa, "akitolea mfano alisema, "adha ya maguruwe ilipozidi katika miaka ya hivi karibuni, vijana wa Kiislamu Mwanza na Dar es Salaam walisimama kuondoa uovu kwa mikono yao." Katika kongamano hilo, vijana wa Kiislamu walipata fursa ya kupokea wasia kutoka kwa wazee maarufu miongoni mwa wale waliokamatwa kwa tuhuma za kuendesha mihadhara iliyosema Yesu si Mungu. Wazee hao ni Sheikh Chata (78) toka Msikiti wa Mtambani na Sheikh Katambo (85) toka Msikiti wa Baitil Mugadasi, Kimara Baruti, Dar es Salaam. Walialikwa rasmi katika kongamano hilo kuzungumzia mateso waliyofanyiwa wakiwa mahabusu. Akitoa wosia wake, Sheikh Chata alisxema kwamba ingawa kaonewa kwa kuteswa na kuwekwa mbali na familia yake lakini kafarajika sana kwa ....... mateso hayo kwa sababu ya kuamini kwake kwamba Yesu si Mungu na dini ya haki ni Uislamu, hivyo aliwahusia vijana wa Kiislamu nchini kutokuteteleka na msimamo huo. Kauli hiyo ya kijasiri na yenye msimamo toka kwa mzee wa miaka (78) iliwasisimua sana vijana kiasi cha kuwafanya akina mama ambao walifarajika kwa wasia na kutaka aendelee kuzungumza pale alipomaliza kusema, mara baada ya kumaliza kuzungumza mzee Chata, vijana walisikika wakitoa ahadi kwamba hawataruhusu tena mzee wa Kiislamu kukamatwa kwa ajili ya kupigania dini yao wakati wao wapo. Katika kongamano hilo mada mbalimbali ziliwasilishwa kuhusu hali ya Waislamu na dini yao. Katika mada ya ufunguzi, Mwenyekiti wa Masjid Nuur Sheikh Waziri Mkobo, alisisitiza kcuwa Waislamu wamewajibikiwa kuwadhibiti madhalimu ili kuleta amani na utulivu nchini. Naye Sheikh Omari Kundecha kutoka Msikiti wa Islamic Centre, Magomeni alisifu na kupongeza msimamo wa kijasiri ulionyeshwa na akina mama wa Kiislamu nchini, katika kadhia ya mabucha (93) na hivi karibuni Mwembechai , aliwataka Waislamu wanaume kwa kwa nawake kushikamana na kuendeleza msimamo huo. Katika mada, "wasia wa Sheikh Hassan bin Ameir kuhusu elimu" iliyotolewa na Ustadhi Salimu toka Ukonga Jijini Dar es Salaam, aliwataka Waislamu nchini kuwalea vyema vijana wao ili waweze kuijenga jamii imara. Ustadhi Salimu alisema kwamba msimamo ulioonyeshwsa na vijana wa Kiislamu nchini katika kupigania dini yao ni Ishara ya walezi wazuri, na akataka malezi hayo yaimarishwe. Kongamano hilo lilifungwa na Katibu Mkuu wa Baraza
Kuu, Sheikh Abasi Kilima ambaye aliwataka vijana wakatekeleze maazimio
waliyoyapata katika kongamano huko waendako.
|
Maoni yetu: Umakini wa Wabunge unatia wasiwasi AGIZO LA MANISPAA KUPEWA MAJINA YA
WANAFUNZI WA KIKATOLIKI
Madai ya Ali Ameir kuhusu Chuki yakanushwa
Mwanamuziki Nyota CAT STEVENS asimulia alivyosilimu Watakiwa kuacha kuwatuma watoto mitaani
Kijana wa Kibarbaig aliyejitolea kupigania
dini yake
'Waislamu wenye sisa kali'
MAKALA: Maisha ya ndoa kwa Muislamu
- 2
Mjibuni Mwinjilisti Kusupa msitukane
Vigogo wahusishwa na madawa ya kulevya
Z'bar
Da’awa Handeni yashika kasi
Kongamano la vijana wa
Kiislamu Masjid Nuur Dar
Mashairi - uzawa wa Mtume (S.A.W)
|