AN-NUUR
Na.159 Rabi' Awal 1419, Julai 24 - 30, 1998
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Chakula na lishe 
 
Mlo kamili 

Na Mujahiid Mwinyimvua 

NENO mlo kamili katika makala hii lina maana ya chakula cha kutosha na chenye virutubisho (viinilishe) vyote muhimu kwa ukuaji na ustawisha wa mwili wa mwanadamu. Lugha ya Kiingereza, chakula cha aina hiyo hujulikana kama balanced diet. 

Virutubisho muhimu katika mlo kamili ni wanga, protini, mafuta/oil, vitamin, madini, maji na nyuzinyuzi (ronphage/dietary fibres). 

Mwili wa mwanadamu unahitaji virutubisho vyote nilivyovitaja hapo juu ili uweze kukua na kustawi vizuri. Kwa maneno mengine, ukosefu wa baadhi ya virutubisho hivyo huathiri ukuaji na ustawi wa mwili hasa kwa watoto wadogo. Kwa hiyo, ninaomba wananchi kulima au kufanyakazi (au biashara) kwa bidii ili tuweze kuwana chakula cha kutosha au tuweze kuwa na fedha za kununua chakula ambacho ni mlo kamili. 

Virutubisho vya wanga tunaweza kuvipata kwa wingi katika vyakula kama vile ugali (wa mahindi, muhogo, ulezi, mtama, uwele, n.k.) wali, mkate, ndizi, chapati, maandazi, vitumbua, viazi, mihogo, mahindi. 

Katika vyakula nilivyovitaja hapo juu, virutubisho vingine kwa mfano vitamini, madini, nyuzinyuzi, mafuta, vinapatikana katika vyakula hivyo, lakini kwa kiasi kidogo. 

Virutubisho vya protini navyo vinapatikana kwa wingi katika vyakula kama vile nyama ya kila aina, samaki, maharage, kunde, choroko, maziwa (ya mama na ya wanyama), mayai, senene, n.k., katika vyakula hivi vya protini, virutubisho vingine pia vinapatikana. 

Kwa upande wa virutubisho vya mafuta, tunavipata kwa wingi katika vyakula vyenye sura na majina mbalimbali kwa mfano siagi (blue band, Tand bond, n.k), Mpishi, Korie, Moproco. 

Hata hivyo, ninawashauri wananchi wafanye uchambuzi kuhusu mafuta ya kupikia kwa sababu baadhi ya mafuta yaliyopo katika maduka si mazuri. Makala hii haikusudii kutoa sifa za mafuta mazuri au kuyataja yapi mabaya. 

Virutubisho vya vitamini vinapatikana kwa wingi katika vyakula kama vile matunda na mboga za majani za aina mbalimbali. 

Kwa mfano, machungwa, embe, mananasi, ndizi mbivu, mchicha, matembele, kisamvu, bilinganya, kabichi, majani ya kunde na ya maboga. 

Madini yanapatikana kwa wingi katika vyakula kama vile dagaa, samaki, nyama, vyakula vinavyotokana na mimea, n.k. 

Maji ni kirutubisho kilicho muhimu kwa kazi mbalimbali mwilini. Baadhi ya watu wana tabia ya kunywa maji pale tu wanaposikia kiu. Jambo hili si zuri. 

Kwa mujibu wa kanuni za chakula na lishe ni lazima kunywa maji kila unapokula chakula. 

Hata hivyo, ni vema ikakumbukwa kuwa, maji yanaweza kupatikana katika sura mbalimbali, kwa mfano maji asili (pure water), kwenye soda, maziwa, n.k. 

Kwa maneno mengine, kama utakula chakula na kunywa soda inatosha vile vile ni vema ikakumbukwa kuwa soda, maziwa au kinywaji kingine kisichokuwa maji asili huwa hakiondoshi kiu. Kwa sababu vinywaji hivyo huongeza ‘solute’ katika mwili 

Napenda kuimalizia makala yetu kwa kusisitiza kwamba, mwili wa binadamu unahitaji virutubisho vyote tulivyoviona hapo juu. 

Hivyo basi, ni makosa kuridhika na mlo wa ainamoja kila siku, kwa mfano ugali na maharage, hauna matunda wala mboga za majani. 

Hata hivyo, ninajua kuwa umaskini ni adui mkubwa wa upatikanaji wa mlo kamili (chakula bora). Hivyo basi, wenye wasaa wawakumbuke wenzi wao wanaokula mlo mmoja tu au kukosa kabisa. 

Vile vile serikali iongeze nguvu katika suala zima la kuondoa umasikini kwa wananchi wake. 
 

Juu 
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI 

Maoni yetu: Umakini wa Wabunge unatia wasiwasi 

AGIZO LA MANISPAA KUPEWA MAJINA YA WANAFUNZI WA KIKATOLIKI 
Na Mwandishi wetu, Morogoro 

Madai ya Ali Ameir kuhusu Chuki yakanushwa 
Na Mwandishi wetu 

AN-NUUR  kwenye Internet 

Mwanamuziki Nyota CAT STEVENS asimulia alivyosilimu 

Watakiwa kuacha kuwatuma watoto mitaani 
Na. Kassim Juma 

Kijana wa Kibarbaig aliyejitolea kupigania dini yake 
Na. Ali Njuki 
 
MAKALA: Zanzibar na tamasha la filamu
Na Said Mzee

'Waislamu wenye sisa kali'
Na. Ustaadh A. S. Fundi 

MAKALA: Maisha ya ndoa kwa Muislamu - 2
Ustaadh Khamis Suleyman Nassoro, Usangi, Mwanga - Kilimanjaro

Pongezi hizi za nini?

Mjibuni Mwinjilisti Kusupa msitukane 
Na Paskal Msemakweli

BARUA YA WAZI KWA WABUNGE

Vigogo wahusishwa na madawa ya kulevya Z'bar
Na Mwandishi Wetu

Da’awa Handeni yashika kasi
Na Ibn Muhammad

Kongamano la vijana wa Kiislamu Masjid Nuur Dar
Na Mwandishi Wetu

Mafunzo ya Quran 

Barua za wasomaji 

Mashairi - uzawa wa Mtume (S.A.W)

Habari za Madrasa 

Masomo 

Chakula na Lishe 
  

 
 Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita