|
|
|
NAPENDA kumkumbusha ndugu yangu Bwana Augustine Mwinuka kuhusu mada Nabii Issa na Yesu hawahusiani" aliyoitoa katika gazeti la Msemakweli Toleo la 18 la tarehe 5-11-Julai, 1998, Bwana Mwinuka amejaribu kumwambia Bwana Muhib Saidi kwamba hajui kusoma na si Muhibu tu bali Waislamu wote wanahitaji msaada wake wa kusomeshwa. Pili amejiita kwamba yeye ni mtu wa kujibu, hivyo tumuulize yeye. Atufundishe elimu ya kiroho ambayo hatunayo. Ungana na A. NGOWI katika makala yake akijibu madai hayo. Lakini mimi nasema hivi ndugu yangu Mwinuka yeye ndiye anayehitaji Da’wah tena inaonyesha kwamba anahitaji msaada wa Waislamu ili wamuelimishe zaidi. Kwa sababu Wakristo wengi kuanzia Papa, Makadinali, Maaskofu, Mapadri, Wachungaji na waumini wote wa Kikristo wanakiri kwamba Issa (a.s.) ndiye Yesu. Kwa sababu Waislamu tunasema Issa (a.s.) si Mungu, na hakusulubiwa kwa maneno hayo Wakristo hutuambia kwamba tunakashifu kwa usemi huo ni dhahiri kwamba Issa (a.s.) ndiye Yesu. Huu ni utangulizi tu wa kumfahamisha Bwana Mwinuka pamoja na Wakristo wote wanaokataa kwamba Issa (a.s.) si Yesu. Bwana Mwinuka katika kuonyesha kwamba Issa (.a.s.) na Yesu ni tofauti ameainisha mambo sita, hayo ni (1) jina (2) ukoo (3) kuumwa (4) kuzaliwa (5) utume (6) matendo yao kwa mambo haya 6. Mada hii imerefushwa sana na mimi nitamfundisha moja baada ya moja kama alivyopanga ili aelewe vilivyo kwamba Issa na Yesu ni Mtu yule yule na pia ajue kwamba Waislamu wanayo elimu ambayo si ya kubabaisha. Hoja ya kwanza iliyotolewa na Mwinuka ambayo yeye anaona kwamba Issa (a.s.) si Yesu ni hii ya jina na hapa hapa namnukuu kama alivyoandika, ameandika hivi! Kimatamshi jina la Yesu kwa Kiarabu ni YASU. Hivyo ndivyo aitwavyo na Waarabu. Wakristo tangu zama za kabla ya Muhammad na ndivyo aitwavyo ndani ya Injili ya Kiarabu iliyotafsiriwaWaraa bin Naufal bin Asad kabla ya utume wa Muhammad (sahihi Muslim hadith 30). Haya ndio mafundisho ya Bw. Mwinuka kwamba Wakristo wenzake wa Kiarabu walimwita Bw. Yesu, YASU kwa maelezo haya ni kwamba Mwinuka anatufahamisha kwamba Yesu ndiye YASU kwa hilo (tunamuunga mkono) tunakubaliana naye, hakuna tofauti kama alivyodai. Waarabu Wakristo walimwita YASU badala ya Yesu na Waislamu ni Isa.Namnukuu tena usemi wake wa pili ameandika hivi! Jina la Issa linatokana na jina AYASI lenye maana ya wekundu uliozidiana na weupe (Badawi, Vol 1 ukibo) kwa maana hiyo jina la Yesu ni mwokozi wa Issa ni wekundu na weupe. Hii huoni kuwa ni tofauti? Bwana Mwinuka anauliza swali na mimi namjibu kwamba hakuna tofauti kwa sababu ametufahamisha kwamba AYASI ndio inayozaa Issa au kwa maana nyingine ni kwamba tafsiri ya AYASI ni Issa kama vile Father maana yake baba bado hajafundisha kitu ila anajichanganya mwenyewe! Lakini amejaribu kujenga hoja kwamba Issa maana yake ni Wekundu na Weupe hapa napanda kumfundisha kwamba Bwana Yesu ni wa ukoo wa Daudi na Daudi alikuwa nabii Mathayo 1.1 - Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daudi mwana wa Ibrahim. Aya hii inatufundisha kwamba bwana Yesu ni wa ukoo wa Daudi yaani ametoka katika tumbo la Daudi. I Samweli 16! 11-13 kisha Samweli akamwambia Yesu, watoto wako wote wapo hapa? Naye akasema, amesalia mdogo wao, na tazama, anachunga kondoo. Basi Samweli akamwambia Yesu. Tuma watu, wamlete, kwa sababu hatutaketi hata atakapokuja huku. Basi akatuma mtu, naye akamleta kwao, naye alikuwa mwekundu, mwenye macho mazuri, na umbo lake lilikuwa la kupendeza. Bwana akasema, ondoka, umtie mafuta, maana huyu ndiye. Ndipo Samweli akaitwaa pembe yenye mafuta, akautia kati ya ndugu zake na roho ya Bwana ikamjilia Daudi kwa nguvu tangu siku ile. Basi Samweli akaondoka, akaenda zake Rama. Wimbo ulio bora 5! 10- Mpendwa wangu ni mweupe, tena mwekundu mashuhuri miongoni mwa elfu kumi. Aya hizi mbili zinatufundisha sifa za Nabii Daudi ambaye ndiye wa ukoo mmoja na Yesu kwa hiyo Bwana Yesu amechukuwa jina la Wekundu wa weupe kutoka kwa Nabii Daudi. Kwa maana hiyo hakuna tofauti yoyote kati ya Issa (a.s.) na Yesu. Nabii Daudi amefanywa kuwa masihi na Samweli kwa idhini ya Mungu, hali kadhalika na Issa (Yesu) amefanywa masihi na kuitwa hivyo sasa tuisome Qur’an 3.45 - Kumbukeni waliposema malaika Ewe Maryam! Mwenyezi Mungu anakupa habari njema za (kumzaa mtoto bila ya mume, bali kwa kutamkwa) neno tu litokalo kwake (la kukwambia "zaa" ukazaa pasina kuingiliwa) Jina lake ni Masih, Isa mwana wa Maryamu, mwenye hishima katika dunia na akhera, na miongoni mwa waliopelekwa mbele ya Mwenyezi Mungu. Wakristo wote wanakubali na kuamini kwamba Bwana Yesu ni Masih, na Qur’ani imetufahamisha kwamba Masih ndiye Issa mwana wa Mariyamu kwa maana hii mtu ni yeye yule, sasa nakuuliza Waingereza wanamwita Jesus jee huyu ni nani? Kati ya Isa, Yesu, Yasu? Fahamu kwamba lugha ya Kiarabu inafanana na lugha ya Kiarau lugha hii ni lugha dada ya Kiarabu hivyo, zinafanana Issa hutamkwa na Waarabu na Isai hutamkwa na Bani Israil (wana wa Israil) ambao hutumia lugha ya Aramic. Bwana Yesu alikuwa anaitwa Yehoshua lakini Wayunani walishindwa kuita Yehoshua wakaita Yesu. Kwa hiyo waliacha Ho na shua wakakata Yesu sasa ninakushangaa wewe kutoa tafsiri ya Yesu kwamba ni mwokozi wakati neno lenyewe limekosewa kutamkwa. Hivi sasa atakaporudi bwana huyo tunayemwita Yesu halafu tumuite Yesuu, Yesuu, Yesuu sidhani kwamba ataitikia kwa sababu jina hilo halitambui. Hakuna jina Yesu katika Israel bali utakuta jina Yoshua, Ishaya, Yona, Isaya, Isai, Yakobo, lakini Yesu si jina la Kiisrael. Lakini sisi Waislamu hayo hayatupi tabu kuyatumia, sisi tunaita Yesu au Jesus kwa kuwaridhisheni nyingi ili tuweze kuwasiliana kwa hilo tunalokusudia kulizungumzia kama vile Mtume Musa mnavyomwita Moses jee unadhani kwamba kama akija leo atakubali kuitwa Moses? Hali kadhalika huyu mwanafunzi wa Yesu mnaemwita Petro hili si jina lake bali ni jina la kupanga tu alilopewa na Warumi lakini sisi hatuwezi kusema kwamba Warumi wana-Petro wao na sisi tuna Simon Bar Yona wetu, na huyu Simon bar Yona ni ukoo wa Yesu. Mathayo 16:16 - Simon Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliyehai. Yesu akajibu akamwambia, Heri wewe Simon Bar Yona kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali baba yangu aliye mbinguni. Elewa hapa bwana Yesu kama mwalimu mwema anatufundisha kwamba Petro jina lake halisi Simon bar-Yona, sasa nyie muiteni mpendavyo lakini mtuambie hapa tuna maana ya Simon bar-Yona basi tutawasikiliza kwa hilo hilo mpendalo. Ndio maana sisi Waislamu tunasema huyo mwitae Yesu ni Issa (a.s.) tusigombanie jina tugombanie mtu mtarajiwa. Tunakubali Yesu ni mwokozi lakini si maana ya jina Yesu bali hiyo ndio kazi yake aliyojia duniani kuokoa, Mathayo 1:21. UKOO Bwana Mwinuka anasema ukoo pia unamsaidia kufundisha kwamba Yesu si Isa - (a.s.) ameandika hivi! Qur’an inasema Mariam aliyemzaa Issa ni binti wa Imran (Imran 35 na Al-TGahym 12). Pia inaongeza kuwa Mariam alikuwa dada ya Haruni (Mariam 28). Biblia inasema dada ya Haruni ni Mariam wala si Mariam (kutoka 15:20). Biblia bado inaeleza kuwa Mariam dada yake Haruni hajawahi kuzaa maisha yake yote. Biblia inaeleza kuwa Yesu wa Biblia amezaliwa na Mareiam wa ukoo wa Daudi (Mathayo 1:18-20). Kwa sababu Bwana Mwinuka ameeleza habari za ukoo sidhani kama anajua nini maana ya ukoo au anajua ile kwa sababu amejengeka katika majina hivyo anapata tabu sana tofauti ya Miriamu na Mariam. Pia ametoa ushahidi katika Qur’ani kwa kutumia sura 3 tofauti zinazozungumzia utukufu wa Mama Mariam kwa hivyo ni vizuri nizinukuu halafu tutaona anakataa nini. Aaliimran 3:35 - Kumbukeni aliposema mke wa Imrani (Baba yake Mariyam katika kumwomba Mola wake) "Mola wangu! Nimeweka nadhiri kwako aliyemo tumboni mwangu kuwa wakfu (wa kutumikia mambo ya dini) basi nikubalie. Bila shaka wewe ndiye usikiaye na ujuaye. Aya hii inatufundisha kwamba mke wa bwana Imrani alipopata mimba ya Mama Mariyam alimuomba Mungu kwamba mtoto atakayemzaa awe mtumishi wa dini ya Mwenyezi Mungu asiwe na kazi nyingine yoyote. Aya hii ndivyo inavyoelezea. Sasa tusome aya nyingine Surat Mariam 28. Ewe dada yake Haruni! Baba yako hakuwa mtu mbaya wala mama yako hakuwa asharati. Aya hii hasa ndiyo bwana Mwinuka ameijengea hoja kwamba Haruni alikuwa na dada yake ambaye alikuwa anaitwa Miriam, ambaye hakuzaa maishani mwake. Vipi tena tusikie Mariyam amezaa? Hapa ndipo penye somo lenyewe la kuamini kwamba Yesu ndiye Issa au siye! Mwinuka umezungumzia ukoo kama kielelezo chetu hasa kwa jina Maryamu na Miriam dada yake Haruni. Tunafahamu kwamba ukoo wa Bwana Yesu unaanzia kwa mtume Yakobo ambaye alizaa watoto kumi na mbili lakini hoja yako ya Haruni na Miriam aliyezaa ndugu yangu haufahamu tafadhali soma. Luka 1:5 - Zamani za Herode, mfalme wa Uyahudi, palikuwa na kuhani mmoja jina lake Zakaria, wa zamu ya Abaya na mkewe alikuwa mmojawapo wa uzao wa Haruni, jina lake Elisabeti. Uzao ndio ukoo uliouzungumzia sasa aya aliyoitoa ya kutoka 15:20. Hiyo ilikuwa ikizungumzia zama hizo kabla ya mama yake Yesu na Yesu mwenyewe. Na ukoo huwa hauishi wote bali huendelea lakini aya inayofuata inatueleza kwamba hao asili yao ni matasa. Luka 1:7 - Nao walikuwa hawana mtoto, maana Elizabeti alikuwa tasa, na wote wawili ni wazee sana. Kwa hiyo lawama uisomayo katika sura Mariam 28 ni sahihi kwa sababu akina Harun wote walikuwa wacha-Mungu na Mzee Zakaria, Mama Elisabeti ambaye ndiye ndugu ya mama Marioamu hao ni ukoo huohuo uliofuata mila na desturi za ibada ya uch-Mungu tangu zama za Harun, ndio walishangazwa na Mariamu kuzaa bila ya mume. Sasa tusome Aya hii nayo Qur’an 66:12 Na Mariamu mtoto wa Imrani aliyejihifadhi nafsi yake na tukampulizia humo roho yetu (inayotokana na sisi) kna akayasadikisha maneno ya Mola wake, na vitabu vyake, na alikuwa miongoni mwa, wanyenyekevu (wakubwa). Aya hii inatufundisha kwamba pamoja na mke wa mzee Imrani kuomba dua ya kuzaa mtoto mwema, kweli alimzaa mtoto mwema ambaye ni mama Mariyam. Lakini kwa sababu Mungu huwa hampi unabii mwanamke basi mwanamke huyo mwenye asili ya ufasa alizaa klwa uwezo wa Mungu mtoto wa kiume ambnaye ni nabii Issa a.s. au Yesu. Ndipo pale aya inaposema na Mariyam mtoto wa Imran aliyejihifadhi nafsi yake (kuwa mcha-Mungu) tukampulizia humo Roho yetu ni nani hiyo aliyepatikana kwa kupuliziwa Roho ya Mungu ni nani hiyo aliyepatikana kwa kupuliziwa Roho ya Mungu ni Issa a.s. ambaye nyinyi mnamwamini. |
Waislamu hawatokubali kusingiziwa
mambo
Serikali ya Sudan yadhamiria kuleta
amani ya kudumu
Mwalimu alaumiwa kuwashawishi watoto
waingie ulokole
Wanawake Arusha watakiwa
kutafuta elimu
Tamsa Tanga yapata viongozi
wapya
Mjue Dr. Abuu Ameena Philips: Mwanaharakati aliyewasilimisha askari 3000 wa Amerika Barua ya Ofisa Elimu ina agenda nyuma
yake
Nabii Isa Mwana wa Maryamu ni Yesu huyo huyo!! Kuanzishwa ‘Islamic Club’ ni ajenda ya siri inayoweza kuhatarisha amani Tanzania Agenda ya siri
Hatua ya Rais kutengua uteuzi wa
Parole ni ya kizalendo
Serikali iwahurumie raia wake
Wanawake Waislamu Wilayani
Masasi waanzisha Jumuiya
Kuhifadhika kwa mwanamke ni kuhifadhika
kwa jamii
Waislamu wekezeni kwenye
kheri -Mwinyi
Biashara ya ufuska yavamia
Z’bar Polisi uchwara’ wanufaika
Asimamishwa uongozi kwa kutoa
fat’wa ya Hitma
Aqswa waazimia kufuata Qur’an
na Sunna
Mashairi - uzawa wa Mtume (S.A.W)
|