|
|
| Serikali
ya Sudan yadhamiria kuleta amani ya kudumu
Na Mwandishi Wetu Serikali ya Sudan imesema kwamba ni nia yake kufanya kila iwezalo kuleta amani ya kudumu Kusini mwa Sudan. Aidha imesema kwamba inasikitishwa sana na hali mbaya ya njaa na huduma nyingine za kijamii inayowakabili wananchi katika baadhi ya maeneo Kusini mwa Sudan. Akiongea na waandishi wa habari ofisini mwake Agosti 5, Balozi wa Sudan nchini Bw. Kuol Alor amesema kwamba hali ya watu katika baadhi ya maeneo Kusini mwa Sudan ni ya kutisha. Amesema baadhi ya watu wanakufa kwa ajili ya njaa. Hali hii mbaya amesema ni matokeo ya vita vinavyoendelea kati ya majeshi ya serikali na waasi wa SPLA. Ni kwa kuzingatia hali hiyo Balozi Kuol Alor amesema kwamba ufumbuzi wa tatizo hilo hauwezi kupatikana kama hakuna usimamishwaji wa vita katika eneo lote na wakudumu. Kwa kuzingatia wajibu wake kwa wananchi wake; serikali ya Sudan; imetoa tangazo la kusimamisha vita na kuitaka SPLA nayo ifanye hivyo hivyo ili kuwanusuru wananchi wa Sudan wanaoteseka. Amesema kwamba kusimamisha vita kwa wakati huu mazungumzo ya amani yakiendelea huko Ethiopia ni kutilia nguvu azma yake na umakini wake katika mazungumzo hayo ili kuleta amani ya kudumu. Ujumbe wa Serikali ya Sudan katika mazungumzo hayo unaongozwa na Waziri wake wa Mambo ya Nje, Dk. Mustafa Othman Ismail wakati ule wa SPLA unaongozwa na mmoja wa makamanda wake wa ngazi za juu kabisa. Wakati juhudi za mazungumzo ya amani yakiendelea katika nyakati tofauti toka serikali ya Hassan El Bashir kushika madaraka; juhudi pia zimekuwa zikifanyika kuandaa katiba mpya. Bw. Alor alisema kwamba katiba hiyo ilijadiliwa na wananchi wa Sudan waliondani na hata wale wanaoishi nje ya Sudan na kisha kupigiwa kura ambapo ilipitishwa kwa 96.7% ya kura na kusainiwa na Rais Juni 30, 1998. Kwa mujibu wa katiba hiyo Balozi Kuol Alor amesema kwamba wananchi wa Kusini wana haki ya kuamua baada kipindi cha mpito cha mika minne, kuamua ama kubaki kama sehemu ya Sudan au kujitenga. Na kwamba uamuzi huo utafikiwa kwa njia ya kura ya maoni (referandum). Akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua endapo kuna nguvu kutoka nje zinazochangia kudumu kwa vita hivyo; Balozi Alor alisema kwamba ni wazi kama kusingekuwa na nguvu kutoka nje SPLA isingeweza kudumu katika vita hivyo. Hata hivyo hakuitaja nchi yoyote wala jinsi nchi za nje zinavyohusika. |
Waislamu hawatokubali kusingiziwa
mambo
Serikali ya Sudan yadhamiria kuleta
amani ya kudumu
Mwalimu alaumiwa kuwashawishi watoto
waingie ulokole
Wanawake Arusha watakiwa
kutafuta elimu
Tamsa Tanga yapata viongozi
wapya
Mjue Dr. Abuu Ameena Philips: Mwanaharakati aliyewasilimisha askari 3000 wa Amerika Barua ya Ofisa Elimu ina agenda nyuma
yake
Nabii Isa Mwana wa Maryamu ni Yesu huyo huyo!! Kuanzishwa ‘Islamic Club’ ni ajenda ya siri inayoweza kuhatarisha amani Tanzania Agenda ya siri
Hatua ya Rais kutengua uteuzi wa
Parole ni ya kizalendo
Serikali iwahurumie raia wake
Wanawake Waislamu Wilayani
Masasi waanzisha Jumuiya
Kuhifadhika kwa mwanamke ni kuhifadhika
kwa jamii
Waislamu wekezeni kwenye
kheri -Mwinyi
Biashara ya ufuska yavamia
Z’bar Polisi uchwara’ wanufaika
Asimamishwa uongozi kwa kutoa
fat’wa ya Hitma
Aqswa waazimia kufuata Qur’an
na Sunna
Mashairi - uzawa wa Mtume (S.A.W)
|