AN-NUUR
Na.161 Rabiul Thani 1419, Agosti 7-13, 1998
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Wanawake Arusha watakiwa kutafuta elimu 

Na Habiba Swedi, Arusha 

MWALIMU wa akina mama katika Madrasatul-Hidaya ya mjini hapa (Arusha), Ustadha Maryam Salim Ally, amewashauri Wanawake wa Kiislamu nchini kutafuta elimu ili kupata radhi ya Mwenyezi Mungu  

Aliyasema haya alipokuwa katika mahojiano ya ana kwa ana na mwandishi wa habari hizi alipomtembelea katika madrasatul-Hidaya, iliyopo kijijini Ererai kata ya Sombetini, Wilaya ya Arusha mjini. 

Aliendelea kusema kuwa, akinamama wa Kiislamu, wanayasahau majukumu yao kutokana na ukosefu wa elimu ya dini yao. 

Katika kutoa ushauri huo, Ustadha Maryamu amesema kwamba ni kwa njia ya elimu tu, ndipo akina mama wataweza kujenga mioyo ya dini na hivyo kulea familia katika maadili mazuri ya dini ya Kiislamu. 

Amefafanua kwamba, hata kama mama anahangaika na utafutaji riziki kwa familia yake, na kwamba utafutaji huo ni mgumu, bado mama huyo anashauriwa kutenga japo saa moja ya kujielimisha.Ustadha Maryamu aliongeza kuwa, hata Mtume Muhammad (s.a.w.) zama zake, alitoa da’awa huku akihangaika kutafuta riziki. 

Aliasa kuwa; riziki ya mja inatolewa na Mwenyezi Mungu, na lau kama inapatikana kwa taabu tena kidogo kidogo, mama asikate tamaa. 

"Ajibidiishe kuitafuta riziki hiyo huku akimwamini mola wake kuwa atamfungulia, na imani hii itamjia mama huyu, endapo tu ana elimu ya dini", alisema Ustadha Maryam. 

Alimalizia kwa kuzidi kutoa ushauri kuwa; elimu ya dini yake, itamfanya mama wa Kiislamu, kukabiliana na madhila yote yaliyopo katika jamii, na hatoyumbishwa juu ya jambo lolote; kwani ndani ya Qur’ani kunapatikana kila kitu, akiwa na maana kuwa, Qur’ani ni mwongozo na akaongeza kuwa ufafanuzi unapatikana pia katika hadithi za Mtume (s.a.w.). 
 
 

Tamsa Tanga yapata viongozi wapya 

Na Masoud Mohamed 

JUMUIYA ya wanafunzi wa Kiislamu Tanzanhia (TAMSA) mkoa wa Tanga imepata uongozi mpya baada ya ule wa zamani kumaliza muda wake mwezi uliopita. 

Uongozi huo ulipatikana katika mkutano mkuu wa mwaka uliofanyika tarehe 28 Julai kwenye Shule ya Sekondari ya Jumuiya. 

Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa kwa kina ni pamoja na uimarishaji wa somo la maarifa ya Kiislamu na mavazi ya heshima (hijaab) mashuleni. Kutokana na kukosekana kwa ushirikiano kutoka BAKWATA; TAMSA imeazimia kufikia malengo yake kwa kushirikiana na Jumuiya ya Waalimu wa Kiislamu Tanga (JUWAKITA) badala yake. 

Akitoa nasaha zake amiri wa JUWAKITA; Ustadh Khamis Hussein Shemtoi, alipongeza taratibu za kudumisha vikao vya kikatiba vya TAMSA. Hili alisema linaendana na agizo la Qur’an (3:159) ambalo linahimiza "Shuura". Pia aliwataka viongozi wapya wa TAMSA kuwa wasimamizi wazuri wa wenzao kuhakikisha wanasoma na kufaulu vizuri. 

Waliochaguliwa ni: 

(1) Ustadh Sudi Ahmed (Shule ya Popatlal) - Mwenyekiti 

(2) Ustadh Chambuso R. Ramadhani (Jumuiya Sec.) M/kiti Msaidizi 

(3) Ustadh Ali Abbasi (Popatlal) - Mweka Hazina 

(4)Ustadh Athman Ibrahim (Usagara) - Katibu Mkuu 

(5) Ustadh Ali Seif) 

(6) Ustadh Kaimu Mwanjia) (Si wanafunzi) - Makatibu watendaji. 
 

Juu 
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI  

Waislamu hawatokubali kusingiziwa mambo 
Na Mwandishi wetu 

Serikali ya Sudan yadhamiria kuleta amani ya kudumu 
Na Mwandishi Wetu 

Mwalimu alaumiwa kuwashawishi watoto waingie ulokole 
Na Badru Kimwaga 

Wanawake Arusha watakiwa kutafuta elimu 
Na Habiba Swedi, Arusha 

Tamsa Tanga yapata viongozi wapya 
Na Masoud Mohamed 

Mjue Dr. Abuu Ameena Philips: Mwanaharakati aliyewasilimisha askari 3000 wa Amerika 

Duniani kwa ufupi 

Barua ya Ofisa Elimu ina agenda nyuma yake 
Na Mussa Ally Morogoro 

Nabii Isa Mwana wa Maryamu ni Yesu huyo huyo!! 

Kuanzishwa ‘Islamic Club’ ni ajenda ya siri inayoweza kuhatarisha amani Tanzania 

Agenda ya siri 
Na. Hassan Kimangale 

Hatua ya Rais kutengua uteuzi wa Parole ni ya kizalendo 
Na J. R. Msuya 

Serikali iwahurumie raia wake 
Na BADRU KIMWAGA  

Wanawake  Waislamu  Wilayani Masasi waanzisha Jumuiya 
Na Yousouf  S. Kayungilo, Masasi 

Kuhifadhika kwa mwanamke ni kuhifadhika kwa jamii 
Na Zuhra Tajiri 

Waislamu  wekezeni kwenye kheri -Mwinyi 
Na Mwandishi Wetu, Tanga 

Biashara ya ufuska yavamia Z’bar Polisi uchwara’ wanufaika 
Na Rajab Rajab 

Asimamishwa uongozi kwa kutoa fat’wa ya Hitma 
Na Nadhiru Ishengoma Wetu , Kahama 

Aqswa waazimia kufuata Qur’an na Sunna 
Na Mwandishi Wetu 

Mafunzo ya Quran  

Barua za wasomaji  

Mashairi - uzawa wa Mtume (S.A.W)  

Masomo  

Chakula na Lishe  
  

 

 
 Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita