|
|
|
Na Yousouf S. Kayungilo, Masasi WANAWAKE wa Kiislamu mjini Masasi wameanzisha jumuiya yao kwa lengo la kukutana pamoja na kujifunza ili kuzijua kikamilifu haki zao zilizobainishwa na Allah (SWT) katika Qur’an kupitia Mtume (s.a.w.) na kuepuka propaganda za ki-taghoot zinazoenezwa ulimwengu mzima kwa kivuli cha maazimio ya mkutano wa Beijing kuhusu haki za wanawake na kudai usawa. Aidha, wanawake hao wametoa wito kwa wanawake Waislamu kote nchini kushikamana na mwongozo sahihi wa Uislamu na kuepuka propaganda hizo zenye lengo la kuwakufurisha wanawake wa Kiislamu. Katika tamko lao baada ya masomo yao ya jioni wamehoji kwa kusema hao wanaojiita watetezi wa usawa na haki za wanawake mbona matatizo yakiwapata wanawake wa Kiislamu hawainua midomo yao kusema chochote? Na kuongeza kuwa haki za wanawake wa Kiislamu zimebainishwa vizuri katika Qur’an na Sunah sahihi ya Mtume (s.a.w.), hivyo kamwe hawakubali kuyumbishwa, na kwamba ni jukumu la wanawake wote nchini kushikamana na mwongozo huo kikamilifu ili kuzijua haki zazo. Aidha, wamesema, wanawake wengi kwa kupuuza kwao mwongozo wa Uislamu, wamekuwa wakiishi kinyume kabisa na Uislamu, kama kutembea uchi, kushiriki maonyesho ya urembo, kujiuza miili yao kwenye mabaa, madanguruo, n.k. Sasa jukumu lao ni kuzinduka na kujielimisha kama Qur’an na Hadithi za Mtume (s.a.w.) zinavyosisitiza; wamesisitiza wanawake hao. Wanawake hao wa mjini Masasi wametoa pongezi zao kwa vikundi vya akina mama Waislamu wa Songea, Iringa, Morogoro, Dar es Salaam, Tanga, Dodoma na Mwanza kwa jitihada zao za kumkomboa mwanamke wa Kiislamu, na wametoa wito kwa wanawake wa Kiislamu wa mikoa mingine kuiga mfano huo. Pia wamepongeza juhudi za viongozi wa Al-Azizu Islamic Centre kwa ushauri wao mzuri ambao umefanikisha kuanzishwa kwa jumuiya yao nchini ya Taasisi ya Al-Azizu Islamic Centre. Jumuiya hiyo ya akinamama wa Kiislamu Masasi imewasihi Masheikh wetu kuwa wasiziminye ndimi zao kwa kubainisha sheria ya Allah (SWT) na kumfumbia macho adui wa Allah anayepinga kutekelezwa sharia yake katika jamii. Aidha, wamesema, Masheikh wetu wasitoe msisitizo wao mkubwa katika kuwatii masheikh, mawalii na masharifu tu wakati wanaiacha jamii ya Kiislamu inateketea kwa kukosa nafasi katika nyanja muhimu. Wakisisitiza nasaha yao wamesema, Masheikh wauweke Uislamu mbele ya kitu kingine chochote, wasijiweke vifua mbele kuwa vigingi vya kuzuia kusimama kwa Uislamu, wafahamu wao ni binadamu, mauti yapo mlangoni kuwapeleka akhera, huko hakuna zaidi ila pepo na moto, hakuna yeyote atakayenufaika na cheo chake, ila ucha Mungu wake. Hivyo ni bora kwao historia iwakumbuke kama watetezi wa Uislamu kuliko historia kuwakumbuka kama vikwazo vya maendeleo ya Uislamu. Aidha, wamesema wana muunga mkono Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Sheikh Omar Bafadhil kwa msimamo mzuri aliouonyesha wa kutetea haki za Uislamu na Waislamu, na kuwataka masheikh wote wa mikoa kuiga mfano huo mwema wa kutokuwa na woga katika kusema ukweli. Mwisho wametoa wito kwa mashirika ya Kiislamu ya ndani na nje ya nchi na wafadhili binafsi kuwasaidia ili kuimarisha umoja wao, pamoja na shughuli za ki-da’wa pia wana mipango ya kujishughulisha na shughuli za kijamii ili kujiletea maendeleo yao kama kushona, kufuma, n.k. hivyo wenye nia ya kuwasaidia mashine za kushonea, kufuma, kudarizi, n.k.Wanawakaribisha.si. Waliochaguliwa kuiongoza jumuiya hiyo nikama ifuatavyo:- Mwenyekiti -Bi. Halima Hassan, M/Kiti Msaidizi - Bi. Shadida Suleiman, Katibu -Bi. Asiya Hassan, Katibu Msaidizi - Bi Amina Maiwa, *Mtunza Hazina - Bi. Fadina Awadh, Mtunza Hazina Msaidizi - Bi. Rahma Millanzi. |
Waislamu hawatokubali kusingiziwa
mambo
Serikali ya Sudan yadhamiria kuleta
amani ya kudumu
Mwalimu alaumiwa kuwashawishi watoto
waingie ulokole
Wanawake Arusha watakiwa
kutafuta elimu
Tamsa Tanga yapata viongozi
wapya
Mjue Dr. Abuu Ameena Philips: Mwanaharakati aliyewasilimisha askari 3000 wa Amerika Barua ya Ofisa Elimu ina agenda nyuma
yake
Nabii Isa Mwana wa Maryamu ni Yesu huyo huyo!! Kuanzishwa ‘Islamic Club’ ni ajenda ya siri inayoweza kuhatarisha amani Tanzania Agenda ya siri
Hatua ya Rais kutengua uteuzi wa
Parole ni ya kizalendo
Serikali iwahurumie raia wake
Wanawake Waislamu Wilayani
Masasi waanzisha Jumuiya
Kuhifadhika kwa mwanamke ni kuhifadhika
kwa jamii
Waislamu wekezeni kwenye
kheri -Mwinyi
Biashara ya ufuska yavamia
Z’bar Polisi uchwara’ wanufaika
Asimamishwa uongozi kwa kutoa
fat’wa ya Hitma
Aqswa waazimia kufuata Qur’an
na Sunna
Mashairi - uzawa wa Mtume (S.A.W)
|