|
|
| Agenda ya
siri
Na. Hassan Kimangale KATIKA toleo la tarehe 5 Julai 1998, Gazeti la Sunday Observer lina makala ya Ludovick Ngatara yenye kichwa cha habari Agenda ya Siri Katika Kilabu cha Kidini inaweza kuashiria mwisho wa amani Tanzania Ludovick amelaumu sana kuundwa kwa kilabu ya Dar es Salaam Islamic Club kwamba hatima yake ni kuleta Jihadi nchini. Alitoa hoja yake kwa kuonyesha migogoro ya Mwembechai, Algeria, Afghanistan na Sudan. Anasema kuanzishwa kwa club hiyo ni gia kubwa ya kutekeleza mbinu za OIC za Jihad.. Bila sababu za msingi Ludovick akamshambulia Rais wa Awamu ya Pili, lugha ya Kiswahili; kwamba ni matokeo ya utumwa wa Waarabu na kutolea mfano wa majina ya Kitwana na Mwinyi kwamba ni ya kitumwa na kwamba wakati kilabu ya DIC inafunguliwa serikali na chama tawala cha CCM vinafanya njama za kufunga makanisa likiwemo la Mchungaji Kakobe lililostawi nchi nzima. Mwisho wa makala yake aliuliza swali iwapo tutafungua tena milango kwa utumwa mambo leo kwa njia ya ushabiki wa kidini. Makosa ya Ludovick Kama ilivyo kawaida ya waandishi wanachama wa chama cha waandishi Wakristo huandika uongo ili kuvuruga sahihi wa mambo. Kwa bahati njema uongo wao haudumu. Hebu tuzitazame hoja zake kitaalamu. (a) Utumwa: Wakristo kwa miongo mingi ya miaka wamedanganywa kwamba Uislamu una husiana na utumwa. Lakini hakuna hata kiongozi mmoja wa Kiislamu (wa dini, sheikh, imam au khalifa) aliyejihusisha na utumwa. Kinyume chake, meli zilizochukua watumwa zilikuwa na majina ya Yesu, Bikira Maria n.k. Si hivyo tu Papa mtakatifu alikuwa akiziwekea mikono ya baraka ili zisafirishe watumwa salama, kuombea misafara ya utumwa ilikuwa ni sehemu ya kazi ya Papa husika na utumwa. Msomaji wangu nataka ujaribu kuelewa utumwa uendeshwao na Wakristo na kama upo ule endeshwao na ofisi za Kiislamu. Waislamu hawajapata kuendesha utumwa.lamu lakini utumwa uliendeshwa Kikristo. Nchi za Caribean na Marekani walikojaa watu wengi weusi, hawakupelekwa na Waislamu bali ni waumini ambao kuthibitisha ukereketwa wao meli za kubebea watumwa zilikuwa na majina ya Yesu na Maria. Hiyo ndiyo fedheha kubwa miongoni mwa fedheha za Ukristo. Kama Ludovick hajui historia aende tuisheni lakini asiandike Pumba. (b) Migogoro ya kidini Algeria hakuna mgogoro wa kidini. Kuna mgogoro wa kisiasa. Sioni kama kuna dini moja inayokandamiza dini nyingine kama chanzo cha mgogoro. Tatizo lililopo Algeria ni kwamba watu wa huko walipigia kura chama cha siasa cha FIS kiliposhinda kikanyimwa madaraka na waroho wachache wa madaraka. Jambo hilo lilipotokea Nigeria dunia nzima inaishinikiza Nigeria ikabidhi madaraka kwa walioshinda lakini Algeria wanawalaumu walioshinda uchaguzi. Ludovick anaweza kunieleza ni kwanini? Sudan na Afghanistan hakuna tofauti na hali ya Angola na Msumbiji. Garang ni mroho wa madaraka kama alivyo Savimbi. Dunia sasa inambana Savimbi, kwanini hawambani Garang. Sudan hakuna mgogoro wa kidini hakuna anayezuiwa kuabudu atakavyo. Wakristo hawakatazwi kuabudu wala kushika madaraka. Balozi wa Sudan nchini hapa ni Mkristo hadi leo. Garang anapigania nini, wezi wasikatwe mikono? Ana wasiwasi gani na adhabu hiyo kwani yeye ni mwizi? Msomaji wangu, migogoro ya kidini inayojulikana na wanasayansi za jamii kwamba ni ya kidini halisi wa kwanza ni ule wa Ireland. Pale wanagombana si kwa siasa bali kwa Ukatoliki na Uprotestanti. Julai 12, 1998 Wakatoliki wenye roho mbaya wamewachoma moto watoto watatu nyumbani kwao kwa kuzuiwa wasipitishe maandamano yao kwa Waprotestanti. Hao ni Waislamu? Kwa nini Ludovick hulitolei mfano hili? Kule Uganda kuna Walokole wanaodai wametumwa na Yesu chini ya Mchungaji Konyi aliyepokea toka kwa Mlokole Lakwena, na genge lao hilo laitwa "Jeshi la Waokovu wa Bwana". Kwa nini Ludovick hawataji hawa ambao wanaongozwa na Biblia katika vita yao. Kule Bosnia Waserb (Waprotestanti) kwa roho mbaya tu walilenga kuwamaliza Waislamu. Dunia ilikaa kimya hadi walipoona Waislamu wanashinda ndipo ikaingia kinafiki nafiki. Ile ilikuwa vita ya kumaliza Waislamu. Ludovick anajua haya lakini anatolea mifano siasa badala ya dini, ili kuulaumu Uislamu huku akificha dhulma ya Ukristo. Serikali ya Mkapa na CCM ya Mkapa si sehemu ya Uislamu kama inataka kufuta kikundi chochote cha kidini haifanyi kwa kuamriwa na Uislamu. Kwanza nataka ujue kwamba Waislamu hawana chuki na Kakobe wala kanisa lake. Ni Kanisa katoliki lenye chuki na Kakobe kwa sababu anavuna waumini wengi wa kanisa hilo. Ludovick amegusia tena kadhia ya Mwembechai. Waandishi wa Kikristu wanatatizo kubwa ingawa si wote. Ni wagumu sana kuelewa na wepesi kusahau. Hawa wana azimio lao la kupambana na Uislamu kwa njia ya kalamu. Chanzo cha vurugu ni hawa waandishi. Walikubaliana kuiita mihadhara ya Kiislamu kuwa ni ya kashifa kwa Ukristo. Walipoambiwa watoe ushahidi wa kashifa hizo mahakamani hawana. Muislamu anatakiwa kuamini na kutamka hadharani kuwa Mungu ni mmoja, Yesu si Mungu wala Mwana wa Mungu. Wakristo wakawa wanapinga matamshi hayo. Ndipo Waislamu wakawaomba ndugu zao Wakristo wanaopinga wajitokeze hadharani ili wajadiliane ‘kisomi’. Watoe hoja za utatu, Uungu wa Yesu n.k. Yote haya yanafanyika katika kumuandaa Mwanadamu na karne ya 21 ambayo watu wajinga wanaoamini Dogma watakuwa kwenye wakati mgumu. Wakristo kwa maelfu wakaitikia mwito huo na kila mihadhara hiyo inapokuwepo idadi ya wanaohudhuria ni kubwa sana na watu huipenda wakaulizana kwa utulivu na mpango. Kuna kuwepo na Mwenyekiti na wahadhiri kama mihadhara yoyote ya kawaida. Katika mihadhara hii Wakristo wameshindwa kuthibitisha hadi sasa: (a) Uungu wa Yesu (b) Uana Mungu wa Yesu (c) Ukombozi unaotokana na Ekaristi takatifu (d) Yesu alikuwa mtu wa dini gani. Waislamu wamethibitisha kuwa:- (a) Hakuna utatu, Mungu ni mmoja (b) Yesu si Mungu bali ni nabii. (c) Yesu na manabii wote walikuwa Waislamu (d) Dini ya kweli ni Uislamu . "Rewrite the Bible" na ya Kimangale "Yesu rewrite the Bible katika weekend magazine 1991) Wakristo wengi walisilimu na wakawa wakali sana kukemea dhana potofu hapa ndio mwanzo wa tatizo. Wakereketwa ambao huendeshwa na hisia wakadhani wao wana binaadamu wanao waita "watu wao" wakasema watu wetu wanatukimbia na kuingia katika Uislamu. Mkutano wa Maasikofu kule Kenya uliohusisha Maaskofu wa Afrika yote wakasema mihadhara isipodhibitiwa basi, Ukristo utakufa kifo cha kawaida. Hapo ndipo waandishi wakapewa jukumu la kuutangaza Uislamu kwa majina ya kutisha "wenye siasa kali". Sidhani kama wana hiyo siasa. Mihadhara ikaitwa "yenye kashifa". Wakiambiwa njooni mthibitishe kashfa hizo hawana ushahidi. Katiba ya nchi inaruhusu Waislamu kusema Yesu si Mungu, hakuna utatu na kuingia peponi kwa Ekarist ni ndoto. Maasikofu walipoona katiba inawaunga mkono Waislamu, Biblia inawaunga mkono na sheria zinawaunga mkono, wakaamua kuwatumia waumini wao wakereketwa katika serikali watumie nguvu za dola kuwakamata Waislamu na kuwafungulia mashtaka. Ludovick alipaswa kujua kwamba Waislamu waliokamatwa kwa kosa la kukashifu dini ilishindikana kuwapeleka mahakamani kwa sababu:- (a) Anayekashifiwa huomba jina lake lisafishwe. Si serikali kumshitaki mtu aliyekashifu. Maaskofu kama walikashifiwa hawatakwenda kwa Rais bali mahakamani na kudai fidia kwa kukashifiwa. Kwa vile hakuna kashifa hawakwenda kule mahakamani. (b) Hakuna kashifa kisheria kwa kusema Yesu si Mungu. Ni uhuru wa kutoa mawazo. Baada ya njama hizo kushindikana ulipangwa mpango wa kuleta vurugu sehemu za mihadhara ili ipigwe marufuku kutokana na vurugu. Sisi Waislamu waliarifiwa na vyombo vyao wajitahadharishe na mpango huo wa Wakristo wakereketwa ndani ya dola. Utakumbuka gazeti moja lilikuwa linatoa tahadhari maalumu ya suala hilo. Waliposhindwa wakawataka waandishi Wakristo wazushe kuwa kila mhadhara unapofanyika kulikuwa na matusi na fujo. Utakumbuka yule mwandishi wa Mwanza alipotakiwa asitbitishe fujo alizoandika akashindwa na akatakiwa aombe radhi. Liliposhindikana, serikali ikatumia polisi bila kuungwa mkono na katiba ya nchi na sheria wakawa wanavamia kila penye mhadhara. Kwa kawaida polisi wanatakiwa wapokee malalamiko. Mlalamikaji atoe maelezo kwa maandishi. Mlalamikiwa apelekwe kwenye vyombo vya sheria na polisi hao. Kwa mihadhara si hivyo Polisi wakawa ndio walalamikaji, wakamataji na majaji. Wakaadhibu na kuua. Ingawa polisi wanakwenda pale kuwakamata wanaoendesha mihadhara. Wanaofanya fujo ni hao polisi halafu wanaokamatwa wanafunguliwa mashtaka ya kufanya fujo ni Waislamu. Wao wanadhani Waislamu ni wajinga hawaoni mtindo huo wa ukereketwa. Upendeleo: Hivi karibuni kumetokea vurugu za kidini huko Arusha na Makanisa kuchomwa moto wenye makanisa hayo wanasema ni uchochezi wa moja ya kanisa lisilo la Kilokole. Hata hivyo hakuna F.F.U. waliopelekwa na kuua watu huko. Wakati wa tatizo la Bucha za nguruwe lilipotokea, huko Arumeru Kaaya na wenzake walikuwa kwenye tatizo la kidini ambalo lilifikia makanisa, nyumba kuchomwa na watu kuuana. Hatukuona aliyekamatwa hadi leo yaani vurugu zile hazikuwa na watu wa kukamata! Polisi walipokujamkamata Magezi walifika muda wa swala ili wakimkamata watu wafanye fujo wakamatwe na kushitakiwa kwa kufanya fujo. Walipomchukua bila ya fujo hawakuridhika kwa sababu lengo halikutimia walirudi tena na kufanya fujo. Hivi wanawake waliokuwa ndani msikitini wamejificha kulikuwa na haja ya kuwapiga na kuwakatalia dhamana? Hapo pia Ludovick haoni mkono wa sheria na serikali unavyoingiliwa? Serikali hiyo inaondoa chuki au inapandikiza chuki? Kikundi cha Biblia ni jibu walikamatwa lakini kwa adabu sana na kupewa dhamana haraka haraka. Hiyo ndiyo njia ya kuleta amani? Chuki Athumani hakuwekwa pale hospitalini bila matibabu na huku amefungwa pingu kwa bahati mbaya. Lengo lilikuwa kuwaonyesha Waislamu kwamba atakaye usema sana Ukristo atajuta kuzaliwa. Inawezekanaje Rais aamuru watoto waachiwe na mtu asiye na nguvu "mahali" azuie kuachiwa kwa Chuki na abaki kazini. Hivi ni kweli Mkuu wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam hakuwa na habari na mahabusu Chuki? Kwanini hakutekeleza agizo la Rais? Je amewajibikaje kwa jambo hilo? Waislamu waliokamatwa waliwekwa mahabusu kwa miezi mingi bila ya dhamana baada ya "kizuizi" hicho wameachiwa kwa kuwa hawana hatia wengine ni wanawake wa umri ambao mtu yeyote mwanye akili timamu asinge fikiria kuwakamata. Lakini wamewekwa ndani sio kwa kuwa ni wahalifu la bali kuonyesha nguvu za dola dhidi ya Uislamu. Ludovick na wenzake wajue hakuna agenda ya siri, kuna mapambano dhidi ya dhulma na ukandamizwaji wa Waislamu nchini. |
Waislamu hawatokubali kusingiziwa
mambo
Serikali ya Sudan yadhamiria kuleta
amani ya kudumu
Mwalimu alaumiwa kuwashawishi watoto
waingie ulokole
Wanawake Arusha watakiwa
kutafuta elimu
Tamsa Tanga yapata viongozi
wapya
Mjue Dr. Abuu Ameena Philips: Mwanaharakati aliyewasilimisha askari 3000 wa Amerika Barua ya Ofisa Elimu ina agenda nyuma
yake
Nabii Isa Mwana wa Maryamu ni Yesu huyo huyo!! Kuanzishwa ‘Islamic Club’ ni ajenda ya siri inayoweza kuhatarisha amani Tanzania Agenda ya siri
Hatua ya Rais kutengua uteuzi wa
Parole ni ya kizalendo
Serikali iwahurumie raia wake
Wanawake Waislamu Wilayani
Masasi waanzisha Jumuiya
Kuhifadhika kwa mwanamke ni kuhifadhika
kwa jamii
Waislamu wekezeni kwenye
kheri -Mwinyi
Biashara ya ufuska yavamia
Z’bar Polisi uchwara’ wanufaika
Asimamishwa uongozi kwa kutoa
fat’wa ya Hitma
Aqswa waazimia kufuata Qur’an
na Sunna
Mashairi - uzawa wa Mtume (S.A.W)
|