AN-NUUR
Na.161 Rabiul Thani 1419, Agosti 7-13, 1998
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Mjue Dr. Abuu Ameena Philips  

Mwanaharakati aliyewasilimisha askari 3000 wa Amerika 

MENGI yameripotiwa juu ya kusilimu kwa wanajeshi 3000 wa Marekani katika Jangwa la Saudi Arabia wakati wa vita vya Ghuba. 

Hata hivyo ni ripoti chache zinazoeleza ni akina nani waliokuwa kichocheo cha kusilimu kwa wanajeshi hao. 

Ni Kawaida katika kazi ya Da’awa (kuwaita watu katika haki) kwamba hakuna anayefanya tendo hili au lile kwa lengo la kupata sifa bali yote huachiwa Allah kuwa mlipaji. Labda hiyo ndiyo sababu iliyowafanya wafanya harakati hiyo kuwa kimya. 

Dk. Abu Ameena Bilal Phillips ni mmoja wa wanaharakati wachache ambao mara kwa mara walikuwa wakizungukia vikosi vya jeshi la Marekani nchini Saudi Arabia kulingania Uislamu kwa wanajeshi wa jeshi hilo. 

Wakati vikosi hivyo vikipambana kuyaondoa majeshi ya Iraq nchini Kuwait, Dk. Phillip alikuwa akizunguka huko na kule katikati ya vikosi vya Marekani, akilenga kuung’oa ukafiri katika nyoyo za wanajeshi hao wa taifa kubwa lakini duni kimaadili. 

Dr. Abu Ameena Bilali Phillips ni mzaliwa wa Jamaica, hivi sasa ni mhadhiri wa chuo kikuu cha Kimarekani Jijini Dubai, Muungano wa Falme za Kiarabu (UAE). 

Historia ya Abu Amina 

Ingawa alizaliwa nchini Jamica, Dr. Abu Amina anasema alisomea nchini Canada, alipata shahada ya kwanza katika biochemistry. 

Kwa kuwa anatoka katika familia ya Kikristu, maisha yake ya awali aliishi kama Mkristu. 

Wakati akiendelea na masomo yake nchini Canada, alitokea kuvutiwa na itikadi ya Kikomunist. Ni katika kipindi hicho hicho alishuhudia mivutano na mapambano katika mabweni ya Wanafunzi wa kiamerika. Mivutano hiyo ilitokana na ubaguzi wa rangi, Wamarekani weupe wakiwabagua weusi. 

"Nilikerwa na maisha haya, niliamua kwenda China kuona maisha ya Kikomunist, nilivutiwa na baadhi ya mambo katika itikadi hiyo". Kwa hiyo niliamua kuingia kwenye ukomunist nikiwa na tamaa kwamba huenda huko kuna mgawanyo sawia wa kiuchumi, anasema Abu Ameena alipokuwa akihojiwa na gazeti la Islamic Voice hivi karibuni mjini Bangalore nchini India. 

Aliporejea nchini Canada akitokea China Abu Ameena anasema moja kwa moja alijiunga na chama cha Kikomunist. Hata hivyo hakuridhishwa na undani wa ukomunist. 

"Maisha ya viongozi wa Itikadi hiyo hayana nidhamu. Nilisita kujitoa katika chama hicho kwa sababu kulikuwa na matarajio kwamba baada ya mapinduzi mambo huenda yakawa sawa":, anasema Dr. Abu Ameena na kuongeza kuwa alitaka kurejea nchini China kuchukua mfaunzo ya vita vya msituni. Hata hivyo Wachina hawakuwa tayari kumpokea. 

"Hili liliniongezea chuki kwa ukomunist, nikajitoa." 

Kusilimu. 

Baada ya kujitoa kwenye ukomunist, Dr. Phillips alibakiwa na hangaiko la moyo huku akichukizwa na dhulma iliyoshamiri. Aliuona ukomunist kama ni mbinu ya wajanja wachache wanaoziteka nyara akili za watu ili wawatumie kufikia malengo yao. 

Wajanja hao wanaojifaragua kutaka kuweka mfumo "sawia" huku wakificha makucha ya tamaa na ulafi wao, hawakuweza kukidhi haja ya Dr. Abu Ameena. Baada ya kugundua siri hiyo Dr. Phillips anasema: 

"Miongoni mwa wanafunzi waliokuwa katika kundi letu, ni madada wawili ambao walishasilimu wakati huo. Kaka zao halikadhalika walisilimu kitambo. Nilisoma kitabu cha Elijah Muhammad juu ya uislamu, hakikunivutia kwa sababu kilikuwa kimejaa chuki dhidi ya watu weupe. Sikuwa tayari kuwaitakidi watu weupe kwamba ni mashetani. Huu haukuwa Uislamu sahihi. 

Kitabu ambacho kilikuwa na athari kubwa kwangu kilikuwa, Islam:The Misunderstood religion" kilichoandikwa na Muhammad Qutb. Hiki kilinifahamisha kwamba Uislamu ni mkamilifu, kwa kweli kilivuta mno akili zangu." 

Kitabu chengine ni "Towards Understanding Islam" kilichoandikwa na Maulana Abul Ala Maududi ambacho kilinipa mtazamo mpana na mwelekeo sahihi wa Uislamu. 

Vile vile nilisoma vitabu vya historia na nikafahamu nafasi ya Uislamu katika kuyakomboa mataifa ya Kiafrika kutoka ukoloni wa nchi za Ulaya. Nilikuja kufahamu kumbe Uislamu haumfundishi mtu kumgeuzia shavu la pili yule ampigaye shavu moja. Kuanzia hapo nikasimama imara kuutetea uislamu. Haukupita muda mrefu huo hatimaye nilisilimu mwaka 1972 

.... Itaendelea toleo lijalo 

Juu 
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI  

Waislamu hawatokubali kusingiziwa mambo 
Na Mwandishi wetu 

Serikali ya Sudan yadhamiria kuleta amani ya kudumu 
Na Mwandishi Wetu 

Mwalimu alaumiwa kuwashawishi watoto waingie ulokole 
Na Badru Kimwaga 

Wanawake Arusha watakiwa kutafuta elimu 
Na Habiba Swedi, Arusha 

Tamsa Tanga yapata viongozi wapya 
Na Masoud Mohamed 

Mjue Dr. Abuu Ameena Philips: Mwanaharakati aliyewasilimisha askari 3000 wa Amerika 

Duniani kwa ufupi 

Barua ya Ofisa Elimu ina agenda nyuma yake 
Na Mussa Ally Morogoro 

Nabii Isa Mwana wa Maryamu ni Yesu huyo huyo!! 

Kuanzishwa ‘Islamic Club’ ni ajenda ya siri inayoweza kuhatarisha amani Tanzania 

Agenda ya siri 
Na. Hassan Kimangale 

Hatua ya Rais kutengua uteuzi wa Parole ni ya kizalendo 
Na J. R. Msuya 

Serikali iwahurumie raia wake 
Na BADRU KIMWAGA  

Wanawake  Waislamu  Wilayani Masasi waanzisha Jumuiya 
Na Yousouf  S. Kayungilo, Masasi 

Kuhifadhika kwa mwanamke ni kuhifadhika kwa jamii 
Na Zuhra Tajiri 

Waislamu  wekezeni kwenye kheri -Mwinyi 
Na Mwandishi Wetu, Tanga 

Biashara ya ufuska yavamia Z’bar Polisi uchwara’ wanufaika 
Na Rajab Rajab 

Asimamishwa uongozi kwa kutoa fat’wa ya Hitma 
Na Nadhiru Ishengoma Wetu , Kahama 

Aqswa waazimia kufuata Qur’an na Sunna 
Na Mwandishi Wetu 

Mafunzo ya Quran  

Barua za wasomaji  

Mashairi - uzawa wa Mtume (S.A.W)  

Masomo  

Chakula na Lishe  
  

 

 
 Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita