AN-NUUR
Na.161 Rabiul Thani 1419, Agosti 7-13, 1998
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Waislamu wekezeni kwenye kheri -Mwinyi

Na Mwandishi Wetu, Tanga 

WAISLAMU nchini wamehimizwa kutumia mali zao kwenye mambo yote ya kheri kama yalivyo katika sharia. 

Ushauri huo ulitolewa na Rais Mstaafu wa Tanzania, Sheikh Ali Hassan Mwinyi mara baada ya sala ya Ijumaa katika ufunguzi wa Msikiti wa Boraska hapo tarehe 24 Julai, 1998 ikiwa ni sehemu ya shukrani kwa wale wote waliofanikisha ujenzi wake. 

Akinukuu aya za Qur’an na tafsiri zake alisema kila anayetoa mali yake kwa ajili ya shughuli za kuufaa umma wa Kiislamu, huwa amewekeza na atarajie faida kubwa. Tofauti na uwekezaji katika biashara za maslahi ya kidunia, ubia na Mwenyezi Mungu (s.w.) hauhitaji mikataba wala mashahidi; alisema. 

Pamoja na kutokuwepo kwa mambo hayo aliwahakikishia Waislamu kutokukosa malipo wanayoyatarajia kwa vile ahadi za Allah (s.w.) hazikhalifu. 

Mapema katika khutba ya Ijumaa Ustaadh Ali Zubeir aliwatakaWaislamu waitumie misikiti ipasavyo katika kuiendeleza na kuilinda jamii ya Kiislamu. Alisema pamoja na kwamba ardhi yote ni msikiti, lakini bado Mtume (s.a.w.) kitu cha mwanzo alichofanya alipohamia Madina ni kujenga Msikiti ili iwe ni kituo cha harakati. 

Akisikilizwa na mamia ya waumini, wengi wao wakiwa wawakilishi wa misikiti na taasisi; Sheikh Mwinyi alionya juu ya tabia ya matumizi mabaya ya misikiti, kunakopelekea kuwadhuru waumini badala ya kuwanufaisha. 

Msikiti wa Boraska ni mmoja wa misikiti mizuri na mikubwa katika mji wa Tanga.Upo jirani kabisa na hoteli ya Kitalii ya Mkonge, katika eneo ambalo halikuwa na msikiti wowote kwa karibu kilometa moja. Wengi wa waasisi wake ni mawaziri na mameneja wastaafu wa Serikali. 

Kutokana na ukubwa wake, waasisi wake kuwa ni watu wenye uelewa mzuri, na ukaribu wake na hoteli kubwa, baadhi ya waumini wametoa matumaini ya Masjid Boraska kuwa kituo cha kweli kwa maendeleo ya Uislamu Tanga na nchi nzima kwa ujumula. Zaidi ya hilo utatoa fursa nzuri kwa watalii wa Kiislamu na wajumbe wa semina mbalimbali zinazofanyikia Mkonge kupata muda mzuri kwa ajili ya Ibada zao za kila siku. 

Pamoja na kutokuwepo kwa mambo hayo aliwahakikishia Waislamu kutokukosa malipo wanayoyatarajia kwa vile ahadi za Allah (s.w.) hazikhalifu. 

Mapema katika khutba ya Ijumaa Ustaadh Ali Zubeir aliwatakaWaislamu waitumie misikiti ipasavyo katika kuiendeleza na kuilinda jamii ya Kiislamu. Alisema pamoja na kwamba ardhi yote ni msikiti, lakini bado Mtume (s.a.w.) kitu cha mwanzo alichofanya alipohamia Madina ni kujenga Msikiti ili iwe ni kituo cha harakati. 

Akisikilizwa na mamia ya waumini, wengi wao wakiwa wawakilishi wa misikiti na taasisi; Sheikh Mwinyi alionya juu ya tabia ya matumizi mabaya ya misikiti, kunakopelekea kuwadhuru waumini badala ya kuwanufaisha. 

Msikiti wa Boraska ni mmoja wa misikiti mizuri na mikubwa katika mji wa Tanga.Upo jirani kabisa na hoteli ya Kitalii ya Mkonge, katika eneo ambalo halikuwa na msikiti wowote kwa karibu kilometa moja. Wengi wa waasisi wake ni mawaziri na mameneja wastaafu wa Serikali. 

Kutokana na ukubwa wake, waasisi wake kuwa ni watu wenye uelewa mzuri, na ukaribu wake na hoteli kubwa, baadhi ya waumini wametoa matumaini ya Masjid Boraska kuwa kituo cha kweli kwa maendeleo ya Uislamu Tanga na nchi nzima kwa ujumula. Zaidi ya hilo utatoa fursa nzuri kwa watalii wa Kiislamu na wajumbe wa semina mbalimbali zinazofanyikia Mkonge kupata muda mzuri kwa ajili ya Ibada zao za kila siku. 
 

Biashara ya ufuska yavamia Z’bar

Polisi uchwara’ wanufaika 

Na Rajab Rajab 

BIASHARA ya kuuza mwili inaofanywa na wanawake imengia kwa vishindo katika Visiwa vya Zanzibar na kuanza kuogopesha wenyeji wa mji huo. 

Mwandishi wa habari hizi aliyetembelea Visiwa hivyo hivi karibuni aliweza kuwashuhudia wasichana wengi wakifanya biashara hiyo katika mitaa mbali mbali ya mji wa Zanzibar hususan eneo la Tarumbeta. 

Wakina dada hao mara nyingi wamekuwa wakifanya mawindo yao maeneo ya Mahoteli kwa kukaa karibu na hoteli hizo kusubiri wateja wanaokwenda kujiburudisha hotelini hapo. 

Aidha, imegundulika kuwa wasichana hao pindi wanapompata wateja hao (wanaume) wanakwenda kumaliza biashara yao katika viwanja vya Golf ambapo ni sehemu imetengwa maalum na serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa ajili ya viwanja mbalimbali vya mapumziko. 

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa wanawake hao hutoza kuanzia shilingi 1,500 mpaka shilingi 3,000 ambapo wenyewe staili ya malipo hayo wanaita chap-chap. 

Baada ya kuona biashara hii ya ufuska inawachanganyia kina dada hao kuna baadhi ya wanaume ambao wanajifanya ni Polisi na kuwavizia wanawake hao wanapopata wateja na wanapokuwa katika shughuli yao wanajifanya wanakwenda kuwakamata na kudai hongo ambapo mara nyingi mwanaume anatoa ili kuepusha shari ya kupelekwa Polisi. 

Vile vile baada ya kuona biashara hiyo inakwenda vizuri wanaume hao (Polisi bandia) wamejenga urafiki na wanawake hao ambapo mwanamke akipata mwanaume mmoja lazima robo ya mapato yake amgawie jamaa hao. 

Mwandishi wa habari hizi alifanikiwa kumhoji mmoja wa machangudoa hao aitwaye Aisha Abdallah ambaye amesema kwamba analazimika kufanya shughuli hiyo katika mazingira magumu kwa vile Polisi wa SMZ hawapendi wafanye biashara hiyo ndio maana wanashirikiana na wale wanaume kwa ajili ya kuwalinda. 

Pia changudoa huyo anasema kuwa wanamtumia wanaume hao endapo mteja anayekuwa naye anataka kuwadhulumu malipo waliyopatana. 

"Mara nyingi sana wanatusaidia kutetea hela zetu, lakini wanatunyonya sana katika mapato kwani sisi tunafanya kazi kubwa kuwaridhisha wateja wetu lakini wanataka kila fedha inayoingia tugawane," alisema dada huyo wa Kizanzibar. 

Vile vile mwandishi wa habari hizi alifanikiwa kuongea na "Polisi uchwara mmoja" katika eneo la Tarumbeta majira ya saa 5.30 usiku ambaye alikataa kutaja jina lake kudai kama kuna siku wanaingiza si chini ya shilingi 15,000. 

Hii shughuli ndiyo inayotufanya tuishi hapa Zanzibnar hivyo siku biashara ikiwa mzuri hususan kukiwa na muziki katika eneo la CCM Social Hall Maisara basi tunaingiza mpaka shilingi 20,000kwa siku", alijigamba Polisi uchwara huyo. 

Alipobanwa zaidi kuhusu idadi yao jamaa huyo alisema wapo zaidi ya sita na wanasema kazi yao saa 3:30 usiku na humaliza saa 7.00 usiku. 
 

Asimamishwa uongozi kwa kutoa fat’wa ya Hitma

Na Nadhiru Ishengoma Wetu , Kahama 

SHEIKH wa Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga Sheikh Kassimu Kangeta alivuliwa uongozi huo tangu januari 9, mwaka huu na uongozi wa BAKWATA Wilayani kwa madai ya kutoa Fat’wa inayodaiwa kuwa potofu juu ya suala la kuwaombea dua Maiti (Hitima). 

Katika barua yenye kumbu. No. BKT/KH/UL/40/35 iliyosainiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya utendaji Wilaya ya Kahama ilimtaka Sheikh Kassim kuacha wadhifa huo kwa mujibu wa kifungu cha katiba ya Bakwata Namba 111 sehemu ya pili. 

Ilidaiwa kuwa Sheikh Kassim alipotosha fat’wa za ndoa ambazo haikueleza alisema nini juu ya ndoa na pia Waislamu kuleta dua ya Qunut katika swala ya Alfajiri huko Isaka. 

Barua hiyo imeongeza kusema kwamba Sheikh Kassimu alijibu maswali juu ya swala ya Iddil Adhliha na funga ya Ramadhani kwamba Waislamu wanatakiwa kufuata Saudi Arabia, fat’wa ambayo ilipingana na kauli aliyotoa Sheikh wa Mkoa katika msikiti wa Ijumaa. 

Hata hivyo haikueleza ni fat’wa ipi aliyoitoa Sheikh wa mkoa). 

Aidha, barua hiyo ilikuwa ina madai mengi yakiwemo ya kutoa fat’wa za duwa (nyiradi) za baada ya swala za faradhi kwamba zisisomwe kwa sauti na kwamba alishinikiza uchaguzi ufanyike wa kumchagua Sheikh wa Wilaya ya Bukombe kinyume cha katiba ya BAKWATA. 

Kufuatia kusimamishwa kwa Sheikh Kassim Waumini wamekuwa wakiuliza kosa alililofanya. 

Wanadai kwamba kama Sheikh alitoa fat’wa potofu haikuwa na haja ya kumfukuza uongozi bali ilikuwa ni juu yao BAKWATA kutoa fat’wa sahihi zitakazofuta zile alizotoa Sheikh Kassim. 
 

Aqswa waazimia kufuata Qur’an na Sunna

Na Mwandishi Wetu 

UMOJA wa vijana Masjid Aqswa wameazimia kufuata Qur’ani na Suna ya Mtume (s.a.w.) katika maisha yao ya kila siku kwa kuifanya Qurani na Mwenendo wa Mtume (s.a.w.) kuwa ndio dira ya kuendeshea Jumuiya hiyo.  

Azma hiyo ya vijana ilifikiwa katika shughuli ya kuwachagua viongozi wa umoja huo iliyofanyika msikitini hapo hivi karibuni. 

Aidha, vijana hao wamejiwekea mchango maalum kwa mwezi kwa kila mmojawao kuchangia mfuko ili uweze kutumika katika kusaidia masuala mbali mbali katika Uislamu. Pia vijana wameazimia kuanzisha shule ya awali (chekechea) hapo mipango itakapokamilika. 

Juu 
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI  

Waislamu hawatokubali kusingiziwa mambo 
Na Mwandishi wetu 

Serikali ya Sudan yadhamiria kuleta amani ya kudumu 
Na Mwandishi Wetu 

Mwalimu alaumiwa kuwashawishi watoto waingie ulokole 
Na Badru Kimwaga 

Wanawake Arusha watakiwa kutafuta elimu 
Na Habiba Swedi, Arusha 

Tamsa Tanga yapata viongozi wapya 
Na Masoud Mohamed 

Mjue Dr. Abuu Ameena Philips: Mwanaharakati aliyewasilimisha askari 3000 wa Amerika 

Duniani kwa ufupi 

Barua ya Ofisa Elimu ina agenda nyuma yake 
Na Mussa Ally Morogoro 

Nabii Isa Mwana wa Maryamu ni Yesu huyo huyo!! 

Kuanzishwa ‘Islamic Club’ ni ajenda ya siri inayoweza kuhatarisha amani Tanzania 

Agenda ya siri 
Na. Hassan Kimangale 

Hatua ya Rais kutengua uteuzi wa Parole ni ya kizalendo 
Na J. R. Msuya 

Serikali iwahurumie raia wake 
Na BADRU KIMWAGA  

Wanawake  Waislamu  Wilayani Masasi waanzisha Jumuiya 
Na Yousouf  S. Kayungilo, Masasi 

Kuhifadhika kwa mwanamke ni kuhifadhika kwa jamii 
Na Zuhra Tajiri 

Waislamu  wekezeni kwenye kheri -Mwinyi 
Na Mwandishi Wetu, Tanga 

Biashara ya ufuska yavamia Z’bar Polisi uchwara’ wanufaika 
Na Rajab Rajab 

Asimamishwa uongozi kwa kutoa fat’wa ya Hitma 
Na Nadhiru Ishengoma Wetu , Kahama 

Aqswa waazimia kufuata Qur’an na Sunna 
Na Mwandishi Wetu 

Mafunzo ya Quran  

Barua za wasomaji  

Mashairi - uzawa wa Mtume (S.A.W)  

Masomo  

Chakula na Lishe  
  

 

 
 Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita