AN-NUUR
Na.161 Rabiul Thani 1419, Agosti 7-13, 1998
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Mwalimu alaumiwa kuwashawishi watoto waingie ulokole

Na Badru Kimwaga 

WAZAZI kadhaa wa watoto wasomao masomo ya ziada (tuisheni ) kwa mwalimu mmoja huko Mburahati, wamemlalamikia mwalimu huyo kutokana na tabia yake ya kuwashawishi watoto hao kubadili dini au dhehebu kumfuata mwalimu huyo ambaye ni Mlokole. 

Wakiongea na gazeti hili Jijini juzi, wazazi hao kwa nyakati tofauti wamesema kuwa mwalimu huyo anayejulikana kwa jina moja tu la Dan, anayefundisha kwa sasa katika kanisa la Assemble of God la Mburahati Barafu, huwa akiwalazimisha watoto hao ambao husoma shule za msingi kubadili dini zao kutoka Uislamu hadi Ukristo au kutoka dhehebu jingine na kuwa Mlokole kwa maneno ya ushawishi. 

Mmoja wa mzazi ambaye mtoto wake alikumbwa na vishawishi vya mwalimu huyo na kubadili dhehebu, Bwana Andrew Thomas, amesema kuwa mwalimu huyo ambaye hajulikani anafundisha shule gani Jijini, alimfanya mwanae Catherine mwenye umri wa miaka kumi na tatu aliye darasa la 6 kubadili dhehebu kutoka Roman . Catholic (RC) na kuwa mfuasi wa Assemble of God, maarufu kwa jina la Walokole. 

Amesema kuwa yeye kama mzazi wa mtoto huyo amechukizwa na tabia ya mwalimu huyo ambaye mara ya kwanza alikuwa anafundisha tuisheni katika maeneo ya karibu na Uwanja wa KIFA, kando ya Baa ijulikanayo kwa jina la Fontane, iliyoko huko Mburahati. 

Mzazi huyo na mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Mama Sikitu alidai pia hata mtoto wake Bakari Mohamed anayefundishwa na mwalimu huyo, alishawahi kumuelezea jinsi Mwl. huyo anapomaliza kufundisha masomo ya tuisheni, huanza kuwapa sera za Okoka uokolewe na damu ya Yesu, ambapo ni kinyume na makubaliano ya ufundishaji wa tuisheni hizo. 

Hata hivyo uchunguzi wa gazeti hili kwa muda wa wiki moja uliweza kung’amua kuwa huyo anayedaiwa kuwa Mwalimu (yaani Dan, haijulikani kama ni Dunstan au Daniel) hana taaluma ya ualimu, isipokuwa ni mhitimu wa elimu ya sekondari . 

Mwaka 1995 na 96 alikuwa anafundisha wanafunzi wa sekondari huku akisubiri matokeo ya mtihani wake wa Kidato cha Sita. 

Baada ya Majibu kutoka na matokeo kuwa mabaya wanafunzi hao walimkimbia. 

Inasemekana baada ya matokeo hayo alianza kufundisha wanafunzi wa shule za msingi, baada ya wale wa sekondari kumkimbia na ndipo alipoanza kuwarai watotowaingie dini au madhehebu yake, . 

Mwandishi wa habari hizi alifika eneo linalodaiwa kutumiwa kwa "Tuisheni" hiyo, hata hivyo hakuweza kuwasiliana na mwalimu huyo kwa kile kilichoelezwa na wahusika wa mahala hapo kwamba huwa hapatikani nyakati za mchana 
 

Juu 
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI  

Waislamu hawatokubali kusingiziwa mambo 
Na Mwandishi wetu 

Serikali ya Sudan yadhamiria kuleta amani ya kudumu 
Na Mwandishi Wetu 

Mwalimu alaumiwa kuwashawishi watoto waingie ulokole 
Na Badru Kimwaga 

Wanawake Arusha watakiwa kutafuta elimu 
Na Habiba Swedi, Arusha 

Tamsa Tanga yapata viongozi wapya 
Na Masoud Mohamed 

Mjue Dr. Abuu Ameena Philips: Mwanaharakati aliyewasilimisha askari 3000 wa Amerika 

Duniani kwa ufupi 

Barua ya Ofisa Elimu ina agenda nyuma yake 
Na Mussa Ally Morogoro 

Nabii Isa Mwana wa Maryamu ni Yesu huyo huyo!! 

Kuanzishwa ‘Islamic Club’ ni ajenda ya siri inayoweza kuhatarisha amani Tanzania 

Agenda ya siri 
Na. Hassan Kimangale 

Hatua ya Rais kutengua uteuzi wa Parole ni ya kizalendo 
Na J. R. Msuya 

Serikali iwahurumie raia wake 
Na BADRU KIMWAGA  

Wanawake  Waislamu  Wilayani Masasi waanzisha Jumuiya 
Na Yousouf  S. Kayungilo, Masasi 

Kuhifadhika kwa mwanamke ni kuhifadhika kwa jamii 
Na Zuhra Tajiri 

Waislamu  wekezeni kwenye kheri -Mwinyi 
Na Mwandishi Wetu, Tanga 

Biashara ya ufuska yavamia Z’bar Polisi uchwara’ wanufaika 
Na Rajab Rajab 

Asimamishwa uongozi kwa kutoa fat’wa ya Hitma 
Na Nadhiru Ishengoma Wetu , Kahama 

Aqswa waazimia kufuata Qur’an na Sunna 
Na Mwandishi Wetu 

Mafunzo ya Quran  

Barua za wasomaji  

Mashairi - uzawa wa Mtume (S.A.W)  

Masomo  

Chakula na Lishe  
  

 

 
 Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita