|
|
|
Qur’an katika lugha ya Kipanjapi New Delh, India TAFSIRI mpya ya Qur’an tukufu kwa lugha ya Kipanjapi imezinduliwa nchini India, Juni 28, mwaka huu. Tafsiri hiyo yenye kurasa 1240 ilizinduliwa na Rais wa Jamaat Islami, Maulana Sirajul Hassan katika sherehe fupi iliyohudhuriwa na watu kadhaa mashuhuri wa mjini Malerkota mkoani Punjap. Kwa mujibu wa ripoti kutoka nchini India, kazi ya kutafsiri Qur’an katika lugha hiyo iliwachukua wafasiri miaka mitano kuweza kuikamilisha. Tafsiri hiyo mpya ya Qur’an itafahamika kwa jina la Qur’an Majeed Anuwad Te Sankhep Teeka Sahiit. Miongoni mwa waliopewa nakala za mwanzo (Complimentary) za tafsiri
hiyo ni bwana Surjeeta Singh Barnala, waziri wa kilimo na ushirika wa India.
Semina kuhusu uongozi wa Kiislamu Kuala, Lumpur. Chuo Kikuu cha Kiislamu nchini Malaysia, kitaandaa semina ya siku kumi kuhusu uongozi wa Kiislamu. Lengo la Semina hiyo itakayaoanza Agosti 15 mwaka huu, imeelezwa kuwa ni kutoa mafunzo ya uongozi na uendeshaji wa kazi ya Da’awah. Miongoni mwa waalikwa wa semina hiyo ni pamoja na wafanyabiashara na wanaharakati wa Kiislamu sehemu mbalimbali. Mwenyekiti wa semina hiyo atakuwa Prof. Dk. Hassan Omar Kasule.
Mkutano wa Kiislamu Teheran, Iran. Mkutano mkubwa utakaojadili umoja miongoni mwa Waislamu duniani, utafanyika mjini Teheran nchini Iran kuanzia Julai 10 hadi 12 mwakani. Katika mkutano huo zitawasilishwa mada mbali mbali ambazo zote zitalenga kwenye umoja na mshikamano wa Waiislamu duniani kote. Baadhi ya mada hizo zimetajwa kuwa ni pamoja na kanuni za msingi za Uislamu, ufufuo, hadhi na utu wa mwanaadamu, mageuzi ya kijamii na utatuzi wa migogoro. Islamic Volice.
|
Waislamu hawatokubali kusingiziwa
mambo
Serikali ya Sudan yadhamiria kuleta
amani ya kudumu
Mwalimu alaumiwa kuwashawishi watoto
waingie ulokole
Wanawake Arusha watakiwa
kutafuta elimu
Tamsa Tanga yapata viongozi
wapya
Mjue Dr. Abuu Ameena Philips: Mwanaharakati aliyewasilimisha askari 3000 wa Amerika Barua ya Ofisa Elimu ina agenda nyuma
yake
Nabii Isa Mwana wa Maryamu ni Yesu huyo huyo!! Kuanzishwa ‘Islamic Club’ ni ajenda ya siri inayoweza kuhatarisha amani Tanzania Agenda ya siri
Hatua ya Rais kutengua uteuzi wa
Parole ni ya kizalendo
Serikali iwahurumie raia wake
Wanawake Waislamu Wilayani
Masasi waanzisha Jumuiya
Kuhifadhika kwa mwanamke ni kuhifadhika
kwa jamii
Waislamu wekezeni kwenye
kheri -Mwinyi
Biashara ya ufuska yavamia
Z’bar Polisi uchwara’ wanufaika
Asimamishwa uongozi kwa kutoa
fat’wa ya Hitma
Aqswa waazimia kufuata Qur’an
na Sunna
Mashairi - uzawa wa Mtume (S.A.W)
|