|
Na. 057 Jumatano Julai 19 - 25, 2000 |
|
|
|
|
|
Jenerali Ulimwengu amgonga nyundo Mkapa
MWENYEKITI mpya wa Baraza la Michezo nchini (BMT), Jenerali Twaha Ulimwengu amesema, katu Baraza hilo halitofanya shughuli zake kwa upendeleo dhidi ya klabu yoyote ikiwemo Yanga au chama chochote cha michezo nchini. Akizungumza katika uzinduzi wa Baraza hilo jana katika hoteli ya Peacock jijini, Ulimwengu alisema, japo yeye ni mfurukutwa wa hasimu mkubwa wa Yanga, timu ya Simba, kamwe hatolitumia Baraza hilo kuibeba timu yake. "Mimi nilikuwa kiongozi na mwanachama wa Simba kila mmoja anafahamu, sasa Yanga wasidhani kwamba Baraza hili (BMT) limetekwa na Simba, hapana", alitania. "Lakini pia hata Yanga nao wamo BMT, mfano Mkambi (Juma), Tenga (Lodger) kwa hiyo Yanga wasiwe na wawasi", aliongeza dhihaka na kusababisha hadhara kuangua kicheko. Mkambi na Tenga ni wajumbe wa BMT mpya. Awali ya Mwenyekiti huyo wa BMT, alizungumza Waziri wa Elimu na Utamaduni Prof. Juma Kapuya ambaye aliwataka viongozi na wajumbe wa Baraza hilo kutumia uwezo wao wote chini ya kanuni na sheria za Baraza kuhakikisha michezo inapanda chati nchini. Ulimwengu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Habari Corporation inayomiliki magazeti ndugu na Dimba alielezea jinsi Marais wa nchi ambazo zimefanikiwa katika michezo walivyo makini katika sekta hiyo. Alitoa mfano wa Rais Eduardo dos Santos wa Angola ambaye alisema hufungua michezo nchini mwake na kuisimamia mwenyewe mpaka anapoifunga, kitu ambacho Ulimwengu amedai kimesaidia kuinua michezo nchini Angola hususan soka. Utaratibu huo wa Rais Santos wameeleza wanamichezo
ni tofauti na unaotumiwa na Rais Mkapa wa Tanzania ambapo hivi karibuni
alifungua michezo ya wanafunzi wa sekondari (UMISETA) Mkoani Mwanza na
kujiondokea zake, halafu Rais Salmin wa Zanzibar akaifunga baadaye.
ALIYEKUWA kocha mchezaji wa klabu ya Simba ya Dar es Salaam, Hassan Affif amedai kwamba klabu hiyo ina nafasi kubwa mwaka huu ya kutwaa ubingwa wa soka Tanzania bara. Akizungumza na NASAHA mapema wiki hii mjini Dar es Salaam, Affif amedai kitakachoipa Simba ubingwa ni kutokana na kusheheni wachezaji wenye vipaji vy ausakataji gozi. Utabiri huo mnono wa Affif kwa wanachama na wapenzi wa Simba nchini umekuja katika wakati ambao klabu hiyo ya mtaa wa Msimbazi imekuwa ikigawa dozi nene kwa timu pinzani zinazoshiriki ligi kuu ya nane bora Tanzania bara. "Kwa kweli Simba ina wachezaji wengi wazuri ambao nadhani kama klabu itawatumia vizuri, basi nina hakika watachukua ubingwa mwaka huu amedai. Wachezaji hao ambao Affif amewataja kuwa na vipaji visivyo vya kawaida ni Steven Mapunda, Said Maulid, Wicklef Ketto, Patrick Betwel na Bakari Malima. Affif ambaye kwa sasa ni kocha mkuu wa timu ya daraja la pili nchini Qatar ya Istiqama, tathmini yake inaonyesha kuwa timu ya Kajumulo na Mtibwa zinaungana na Simba kucheza ligi ya Muungano Tanzania. Kadhalika Affif amesuuzwa na mfumo wa uchezaji wa timu ya Simba wa "Horizontal" kutoka Brazil ambao pia unatumiwa na timu ya Kajumulo. Aidha, Affif aliyestaafu kuicheza Simba mwanzoni mwa miaka ya 1990 amesema mtani wa Simba, Yanga inaweza kufanya maajabu hata ya kutwa bingwa licha ya kuonyesha mchezo mbovu. |
YALIYOMO
Tahariri
Cheyo kuendeleza ‘mfumo Kristo’ Rushwa katika kura za maoni: 'CCM isitafute mchawi' CUF yakanusha propaganda za waraka Wanachama wa CUF kortini Kilwa KINYANG’ANYIRO CHA UBUNGE: CCM Temeke wamtaka Bazaar 'Wanafunzi Lindi wamshughulikia Mkuu wa Shule aliyewazuia kuswali' Milioni moja zachangwa kujenga madrasa USHAURI NASAHA
MAKALA
MAKALA
MIPASHO NASAHA
Kalamu ya Mwandishi
MAKALA
MAKALA
Burudani/Muziki
LISHE
|
|
|
|
|