|
Na. 057 Jumatano Julai 19 - 25, 2000 |
|
|
|
|
|
S.L.P. 72045, Dar es Salaam Tume, PCB na vyama vya siasa mmekiona mliochoandaliwa Oktoba? Kwa kipindi cha wiki tatu zilizopita tumeshuhudia zoezi la upigaji kura za maoni kwa wanaoomba kugombea udiwani kwa tiketi ta CCM. Siku chache zijazo zoezi la aina hiyo litafanyika kwa wale wanaoomba kugombea ubunge. Katika zoezi la upigaji kura za maoni madiwani hizo vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti vurugu nyingi zilizotokea ikiwemo rushwa ya fedha kwa wapiga kura, kuhonga kwa akina mama, wanachama kwenda kupiga kura katika maeneo ambayo sio yao na kadi za wanachama kutumiwa katika matawi zaidi ya moja. Katika vurugu hizo kumejitokeza makundi ya watoa rushwa na wala rushwa. Katika hao waliohongwa wapo waliokula rushwa na wakakubali kutoa kura zao kwa wahongaji na pia wako waliokula rushwa na wakakataa kuwapa kura waliowahonga. Pamoja na kuwa hizi zilikuwa ni kura za maoni lakini makundi haya ndio yatakayopiga kura katika uchaguzi utakaofanyika mwezi Oktoba. Makundi ambayo yameingia kwenye kupiga na kupigiwa kura yakitokea kwenye kura za maoni zilizotawaliwa na vurugu na rushwa. Nini kinatarajiwa kupatikana kwa Tume yauchaguzi, Taasisi ya Kuzuia Rushwa nchini (PCB) na vyama vya siasa kutokana na makundi hayo? Je, Tume ya uchaguzi haioni kuwa hizi kura za maoni ni maandalizi ya watu kuibiwa kura zao katika uchaguzi mkuu, na vile vile Tume hiyo haioni kura vitendo vya watu kuchukizwa na rushwa iliyojitokeza katika kura za maoni mpaka watu kupiga na wengine kuchoma maboksi ya kura kama ilivyotokea kwa Wamasai kule Arusha ni ishara kuwa wananchi hao hawatakaa kimya pale watakapogundua kura zao zimeibiwa? Ikumbukwe kuwa watu hawa wamekwishawekewa vizuizi kuwa kwenda mahakamani mpaka uwe na shilingi milioni tano ambazo wao hawana. Tume lazima ifahamu kuwa watu hawa kama walivyofanya katika kura za maoni hawataenda mahakamani bali watakuja na jino kwa jino (yaani kutokubali kuibiwa kura). Kwa upande wa PCB, je, hawaoni athari ya kuvinyamazia vitendo hivi vya ulaji rushwa katika kura ya maoni ni kupelekea nchi hii kuongozwa na wala rushwa? Watu ambao wataingia madarakani kwa rushwa si ndio hao hao watakaoendeleza ulaji wa kodi za wananchi? Je, mtu ambaye anatumia fedha nyingi apate udiwani kazi ambayo haina mshahara anategemea kurudisha fedha hizo kwa njia gani kama sio kula mali ya umma? Na vyama vya siasa navyo lazima vijifunze kuwa kuweka mtu anaetegemea kuingia mafdarakani kwa rushwa hakusaidii kwani wapo waliohonga na hawakuambulia kitu katika kura za maoni. Ndio maana kura hizo zilibatizwa kuwa ni kura za hisani kwani watu wamepewa fedha na hawakuwapigiakura hao waliowahonga. Ndio maana hata kada wa siku nyingi wa CCM, Bwana Paulo Sozigwa, amelaumu kuwa katika chama chake watu wasiuzika wamepigiwa kura. Hivyo, tunamalizia kwa kusema kuwa kunyamazia mambo hayo hakuna tija kwa taifa wala kwa vyama vya siasa bali ni hasara ambazo zinashiria kuwa Oktoba mambo hayatakuwa shwari. |
YALIYOMO
Tahariri
Cheyo kuendeleza ‘mfumo Kristo’ Rushwa katika kura za maoni: 'CCM isitafute mchawi' CUF yakanusha propaganda za waraka Wanachama wa CUF kortini Kilwa KINYANG’ANYIRO CHA UBUNGE: CCM Temeke wamtaka Bazaar 'Wanafunzi Lindi wamshughulikia Mkuu wa Shule aliyewazuia kuswali' Milioni moja zachangwa kujenga madrasa USHAURI NASAHA
MAKALA
MAKALA
MIPASHO NASAHA
Kalamu ya Mwandishi
MAKALA
MAKALA
Burudani/Muziki
LISHE
> > |
|
|
|
|