|
Na. 057 Jumatano Julai 19 - 25, 2000 |
|
|
|
|
|
UDP, TLP wathibitisha hisia
za Waislamu kuwa
MWENYEKITI wa chama cha UDP Bwana John Cheyo
ameamua kujitoa katika ushirikiano wa vyama vya upinzani vya CUF na CHADEMA.
Kutokana na msimamo wa kile alichodai kupinga sera za jino kwa jino na
udini zinazotawala umoja huo. Madai ya Bw. Cheyo kuhusu UDINI yameungwa
mkono wa Katibu Mkuu wa TLP Bwana Harold Jaffu kwa kusema kuwa "huu ni
umoja wa kiini macho. CHADEMA imewasaliti wanachama wake kwa kuendeleza
udini, kwani Makani (Bob Makani Mwenyekiti wa CHADEMA) ni Mwislamu na jina
lake la kwanza ni Mohamed"!
KWA muda mrefu, ni CCM ndiyo tuliyoizoea kusikia ikiendesha kampeni dhidi ya Waislamu na Uislamu wao. Katibu Mkuu wa CCM Bwana Philip Mangula ndiyo kinara wa kampeni dhidi ya Waislam. Kwa mfano wakati wa uchaguzi mdogo wa wabunge wa majimbo ya Ubungo na Temeke Mangula alidai kuwa Waislamu wanahongwa kofia na kanzu ili wasiipe kura CCM. Kama vile hiyo haitoshi, Philip Mangula huyo huyo mara kwa mara amekuwa akidai bila kutoa ushahidi kuwa misikiti inatumiwa na CUF kuendesha kampeni dhidi ya CCM. Kwahiyo msimamo wa sasa ulionyeshwa na Bwana John Cheyo wa UDP na Bwana Harold Jaffu wa TLP, CCM sasa imepata washirika wa kuendesha propaganda dhidi ya Waislamu na Uislamu wao. Bwana John Cheyo anawaona Waislamu ni watu hatari kama petroli wasiofaa kuwekwa pamoja katika nafasi za uongozi wa Tanzania. Kwa maana nyingine Uislamu ni kero inayohatarisha amani ya Tanzania. Kwa maneno yake kama alivyonukuliwa na gazeti la Mwananchi la tarehe 13 Jula, 2000 Cheyo alidai kuwa "kama vyama vilivyounga na vitashinda katika uchaguzi mkuu ujao basi safu yote ya uongozi wa juu itakuwa imeshikwa naWaislamu jambo ambalo ni HATARI". Kauli hii ya John Cheyo si ya kuibeza hata kidogo. Kwa sababu inahatarisha umoja wa kitaifa uliojengwa katika misingi ya kuaminiana baina ya Waislamu na Wakristo. Waislamu watakuwa na wataendelea kuwa ni raia wa ajabu kama wataendelea kukaa misikitini mwao na kulalamika tu kuwa wanabaguliwa bila ya kuchukua hatua "positive" za kupamba na ubaguzi huo. Kila Mwislamu na kila Mtanzania mwenye akili timamu anapaswa kuishughulisha akili yake kutafakari muelekeo wa nchi yetu. Kauli kama za waheshimiwa John Cheyo, Harold Jaffu na Philipo Mangula zinaipeleka pabaya Tanzania. Matamshi ya viongozi hao wa kitaifa wa UDP, TLP na CCM yanapaswa kuhesabiwa na kurekodiwa kuwa ni msiba mkubwa kwa Waislamu. UDP na TLP kwa sura ya haraka haraka vinaonekana kuwa ni vyama vya upinzani vimeamua kuisaidia CCM kujenga mpaka wa sumu unaowatenganisha Waislamu na wasio kuwa Waislamu katika kuaminiana katika nafasi za uongozi Tanzania. Kwa mujibu wa msimamo wa UDP, TLP na CCM sasa havitakuwa busara wala hekima au subira Waislamu kukaa kimya, kuomba dua misikitini na kuwaacha wakristo washike idara zote nyeti za serikali wakiamini kuwa iko siku hali itarekebishwa. Kama UDP, TLP na CCM hawawaamini Waislamu kwanini Waislamu wawaamini Wakristo? Tanzania hakuna chama cha Waislamu peke yao wala chama cha Wakristo peke yao. Kwa hiyo serikali na idara zake kuongozwa naWakristo walio wengi na lazima kuwa hiyo haikutokea kwa bahati mbaya. Imefanywa hivyo kwa sababu Wakristo wa aina ya John Cheyo , Harold Jaffu naWakristo walio wengi ndani ya CCM wameona kuwa Waislamu ni watu hatari, kero inayoweza kuhatarisha amani. Sasa hakuna cha Muislamu mujahidina wala mwislamu jina wote kwa CCM, UDP na TLPni watu hatari. Kilichomponza Mheshimiwa Bob Makani Mwenyekiti wa CHADEMA naye kuhesabiwa kuwa anaendeleza udini (Uislamu) ni jina lake la kwanza kuitwa Mohamed na wala sio kuingia msikitini. Hivyo wale wanaodhani kuwa CCM na washirika wake wa UDP na TLP wanawataka waislamu jina waende wakamuulize Mheshimiwa Bob Makani nini kilichumponza. Harufu ya udini (Uislamu) aliyoisikia Bwana John Cheyo katika ushirikiano wa CUF na CHADEMA si harufu nzuri bali ni harufu mbaya. Kwa hiyo harufu hiyo havitoki kwa wanaoswali pekee yao bali hata wasioswali kwa kuwa hao ni Waislamu wanatoa harufu hiyo hiyo mbaya ya udini (Uislamu) Inaposemwa udini maana yake ni Uislamu ndiyo maana Wabunge waliopinga ruhusa ya Waislamu kuvaa hijab hawakuitwa Wabunge wenye udini. Kwa sababu wao walikuwa wanapambana na Uislamu. Lakini wale waliosapoti ruhusa ya Waislamu kuvaa hijab waliitwa watu wenye udini, yaani wenye Uislamu. Waislamu wanayodhima ya kufuta dhana ya makruseda wa CCM, UDP na TLPya kuuona Uislamu ni kero inayohatarisha amani ya nchi. Ni wajibu wa kila Mwislamu sasa kudai mabadiliko ya katiba ya Jamhuri ya Muungano kuweka utaratibu wa mgawanyo wa madaraka kwa kuzingatia usawa utakaoleta uwiano wa kimadaraka na kiuwakilishi kwa Waislamu na Wakristo. Hii itasaidia kufuta dhana yaUislamu kuonekana kuwa ni kero inayoweza kuhatarisha Amani ya Tanzania. |
YALIYOMO
Tahariri
Cheyo kuendeleza ‘mfumo Kristo’ Rushwa katika kura za maoni: 'CCM isitafute mchawi' CUF yakanusha propaganda za waraka Wanachama wa CUF kortini Kilwa KINYANG’ANYIRO CHA UBUNGE: CCM Temeke wamtaka Bazaar 'Wanafunzi Lindi wamshughulikia Mkuu wa Shule aliyewazuia kuswali' Milioni moja zachangwa kujenga madrasa USHAURI NASAHA
MAKALA
MAKALA
MIPASHO NASAHA
Kalamu ya Mwandishi
MAKALA
MAKALA
Burudani/Muziki
LISHE
|
|
|
|
|