NASAHA
Na. 057 Jumatano  Julai 19 - 25, 2000
Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita
MIPASHO NASAHA

Mwanasiasa wa kisasa 

Na Abu Halima Sa Changwa

SA CHANGWA: Ndugu watazamaji, hii ni Television ya Mpasho ikiwajia moja kwa moja kutoka Nasaha. Leo tunawaletea tamthilia iitwayo "Mwanasiasa wa Kisasa". Katika Tamthilia hii tutaona jinsi Toti alivyopewa mtihani na wazazi wake na jinsi alivyoufanya. Karibuni sana (Tabasamu). 

Nyumbani kwa Baba Toti. Baba Toti na Mama Toti wanaonekana. Baba Toti anapanga vitu kadhaa mezani, huku Mama Toti akiwa anamuangalia. 

BABA TOTI: Leo nataka kujua kijana wetu Toti atakuwa nani akishaondoka hapa nyumbani. Vitu vyote hivi naviweka hapa ili avikute, halafu nitagundua atakuwa nani kutokana na kitu atakachochagua. Akichukua hizi pesa, basi atafanya kazi benki. Akichukua hii Biblia atakuwa mtu wa dini, kama sio mchungaji basi mhubiri tu. Akibeba hili boksi la nanihii atakuwa mtu wa wanawake, au muasherati hapo itabidi tumshughulikie mapema. Hii chupa ya pombe itatujulisha kwamba atakuwa bambata, yaani mlevi. 

MAMA TOTI: Weka basi na huu mkufu wangu. 

BABA TOTI: Hiyo ndiyo itatuonyesha nini? 

MAMA TOTI: Atakuwa kibaka, kwa hiyo tutamshughulikia kabla. 

BABA TOTI: Aisee mama Toti leo una akili!! Hebu weka hapo huo mkufu. Halafu nitaongeza na ile silaha yangu, pengine atakuwa mtu wa masilaha, labda polisi au askari. 

MAMA TOTI: Khe ! Je akiwa jambazi? 

BABA TOTI: Wewe mbona unamfikiria mabaya tu. Mara kibaka, mara jambazi! 

MAMA TOTI: Basi tuseme mwanamgambo. 

BABA TOTI: mfyuu! Hebu tuondoke asije akatukuta hapa. Tukakae kwenye kale kadirisha kakutolea chakula tumuone akija atachagua nini. 

Baada ya muda, Toti anaingia, anapiga winja. Anafika mezani, anashangaa kidogo. 

TOTI: Siku zote wananiwekea chakula hapa, leo wameniwekea hivi vitu vyote. Nashukuru sana. (Anapitisha macho kuviangalia) Kufu la nguvu, mvinyo, boksi la soksiDuh, ama kweli hawa wazee sasa wamekuwa. Nanga, neno la Bwana GodIla pesa wamepunja kidogo. Hata hivyo, si haba. Nakomba tu kiulaiiini. (Anaanza kuchukua vitu kuingiza chumbani kwake

MAMA TOTI: (Ananong'ona) He! Sasa mbona anabeba vutu vingi, tutajuaje? 

BABA TOTI: (ananong'ona) Ngoja tuonekachukua pesa, pombe..eeeh.. na boksi la konnanihii, na silaha. Mama yangu eeeh! Atakuwa mwanajeshi. Wanajeshi ndio wenye WWWsio world wide web ya internet ni wine, women na war

MAMA TOTI: Tutafaidi! Ndio vitu gani hivyo? 

BABA TOTI: Utafaidi? Nilikuona umeanza kupata akili, kumbe ni za sekunde tu. Wine ni pombe, women ni wanawake, na war ni vita. Hiyo ndiyo www ya jeshini. 

MAMA TOTI: Yobwa! Tuufwile nyaambala! Mbona kachukua na tule tupesa, hatakuwa benki? 

BABA TOTI: Sasa vitani ataenda bila kulipwa? Na wanawake na mvinyo atapata bila pesa? 

Mara Toti anatokea tena. Anachukua vingine vyote vilivyobaki mezani. Baba Toti anashika kichwa. Mama Toti amebaki kushangaa. 

MAMA TOTI: Jamani, sasa Toti wangu ndio atakuwa nani? Au atakuwa vyote? 

BABA TOTI: Lahaulaaaa!! Mke wangu, mwanao atakuwa mwanasiasa wa kisasa. Hao ndio wamechanganya vyoote alivyochukua Toti. 

SA CHANGWA: Ndugu watazamaji wa Televisheni yetu ya Mpasho, kutoka Nasaha, natumaini mmeburudika vya kutosha na tamthilia yetu. Tamthilia hii inaakisi moja kwa moja hali tuliyonayo katika jamii yetu. Wakati wananchi wamo katika msoto wa hali ya juu, wanasiasa wetu ni pombe tu, Mikutano nyeti ya kupanga mikakati ya Taifa hainogi bila ya mvinyo. Pombe zinazinduliwa kila siku, na wanasiasa wengine ni ma Al-hajj, lakini tunawaona wakionyesha kwenye televisheni jinsi pombe inavyonywewa. Dola wameifanya yao, ni ya kulinda maslahi yao, na sio kusimamia amani ya nchi. Silaha zinatumika kuwamwagia wananchi vyakula vyao wanavyouza, kuwavunjia vibanda vyao, kuwashambulia na hadi kuwaua hata kwenye nyumba za ibada. Pesa ndio usiseme. Hakuna kazi wanazozifanya kama wanavyofanya walalahoi, lakini ukapa ni kwa mlala hoi tu, sio kwao. Kwa upande wa viboksi vya nanihii ndio usiseme. Tunaona makasino yanavyokuwa mengi, karibu yatafikia idadi ya shule, Bei ya kwenda kasino sio ya kwenda kwenye mabaa ya mabambata ya kilalahoi. Mashindano ya wendauchi ndiyo hayo kila siku yanahudhuriwa na wanasiasa, kuangalia mabinti wa watu wakipita jukwaani na vichupi. Ukija kwenye dini, mafundi ni wao. Wao ni mashehe, wao ni mapadre, wao ndio maustadh, wao ndio maparoko. Na hawataki mwingine mwenye dini kuikosoa siasa, ila wenye dini wakisifu siasa zao utawaona wanatangwazwa kwenye redio na magazeti. "Shehe fulani kasema, Padiri fulani kanena" Kuna wale mashehe na mapadre wasiovuma, lakini kipindi hiki cha kampeni wanakuwemo. Hivi ndivyo mwanasiasa wa kisasa alivyo. Ana vyoote alivyokomba Toti (pesa, pombe, neno la Mungu, silaha na maboksi ya nanihii). Na kinachotishia zaidi ni kwamba akina Toti bado wanazaliwa. Leo tutaishia hapa. Mimi ni mtayarishaji wako, Abu Halima Sa Changwa, wa Televiheni ya Mpasho kutoka Nasaha. Tukutane tena katika kipindi kingine. Bye for now.(Tabasamu, meno nje). 

Juu
 

YALIYOMO
 

Tahariri
Tume, PCB na vyama vya siasa mmekiona mliochoandaliwa Oktoba?

Cheyo kuendeleza  ‘mfumo Kristo’

Rushwa katika kura za maoni: 'CCM isitafute mchawi'

CUF yakanusha propaganda za waraka

Wanachama wa  CUF kortini  Kilwa

Waumini waapa kulinda Msikiti

KINYANG’ANYIRO CHA UBUNGE: CCM Temeke wamtaka Bazaar

'Wanafunzi Lindi wamshughulikia Mkuu wa Shule aliyewazuia kuswali'

Milioni moja zachangwa kujenga madrasa

Hata na mimi sijala

USHAURI NASAHA
Jinamizi la ukewenza

MAKALA
Kushindwa kujitegemea ni laana

MAKALA
UDP, TLP wathibitisha hisia za Waislamu kuwa Uislamu ni kero Tanzania

MIPASHO NASAHA
Mwanasiasa wa kisasa

Kalamu ya Mwandishi
Mamluki wa mageuzi

MAKALA
Mrema na Cheyo wajihadhari wasije wakatumiwa kuwavuruga wananchi

MAKALA
Viongozi wa vyama vya siasa na udini nchini Tanzania

Mandela ni mfano wa kuigwa

Burudani/Muziki
Cat Stevens: Historia kwa Ufupi

Habari za Kimataifa

LISHE
Yanayoweza kumdhuru mtoto tumboni

MASHAIRI

MICHEZO

  • Jenerali Ulimwengu amgonga nyundo Mkapa
  • Hassan Affif aitabiria Simba Ubingwa

  •  


    Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
    Au
    Andika barua  kwa: nasaha1420@yahoo.com

    Ukurasa wa mwanzo
    Islam Tanzania
    Matoleo yaliyopita