NASAHA
Na. 057 Jumatano  Julai 19 - 25, 2000
Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita
MAKALA 

Viongozi wa vyama vya siasa na udini nchini Tanzania 

Na: Rajab Kanyama 

KATIKA mfululizo wa makala hizi, wiki iliyopita, tulikuwa tumekusudia kuendelea kuangalia mantiki ndani ya matamshi ya viongozi wa vyama vya siasa na malengo ya kisiasa yaliyojificha nyuma ya matamshi hayo.

Tulishindwa kufanya hivyo, na badala yake, tutakazungumzia rushwa zilizozuka za wagombea uongozi wa Chama Cha Mapinduzi na hatma ya taifa. 

Sakata la rushwa la wagombea uongozi wa Chama Cha Mapinduzi ni fumbua macho itakayo wasaidia sana wananchi katika uchaguzi mkuu ujao, maana sasa watakuwa na uwezo wa kufahamu watu wenye sifa ya kupewa uongozi na wale wasiostahili. 

Utafiti juu ya jambo hili, umeonyesha kwamba, wananchi wamekwisha amua kwamba katika uchaguzi mkuu ujao, watoa rushwa za mapesa, ubwabwa na vikoi, safari hii hawapati kitu. 

Si hivyo tu, hata viongozi matapeli, wanaopumbaza wananchi kwamba wao hawataki udini, na wao pia dawa yao sasa inakorogwa. 

Wananchi wamekwisha baini kwamba, kumbe wale wanaodai kuwa wanaupiga vita udini, ndio hasa wanaouendeleza nchini. 

Wananchi wanahoji, iweje? Wazandiki hao wadai kwamba Chama cha Wananchi (CUF) na CHADEMA ni vyma vya kidini, kwa sababu tu ya kuongozwa na Waislamu, wakati hata vyama wanavyoviongoza wao wenyewe, vimejaa viongozi Wakristo watupu? Au ndio tuseme sasa ndio wananchi wanatakiwa kujua kwamba ndani ya vyama vyao hamna Waislamu? Na kwa maana hiyo ni vyama vya wakristo wakatoliki? Matamshi ya baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa yanatia kichefuchefu. Kama ni ushahidi, sasa umepatikana kumbe yaliyokuwa yakisemwa ni kweli, udini upo tu pale ambapo Mwisilamu ni kiongozi au anaposhika madaraka katika taasisi za umma. 

Kwa vitendo na matamshi ya viongozi wa juu wa vyama vya UDP, TLP na NCCR-Mageuzi, ni ishara ya wazi kwamba vyama hivyo ni matawi ya Catholic Church Movement (CCM) chama hatari kabisa kwa usalama wa nchi. 

Niwazi sasa kuwa ChamachaMapinduzi na serikali yake, havina uwezo tena wa kubuni utaratibu ulio bora wa kumletea mwananchi wa kawaida maendeleo. 

Siku zote,viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na serikali yake wanaendelea kuwanyonya wananchi kwa kujilundikia marupurupu na kujipatia mikopo kutoka katika taasisi za umma na kukandamiza wananchi kwa visingizio mbali mbali, hila na ulaghai kupitia mtandao wao katika vyombo vya habari. 

Kwa vile Serikali ni taasisi, wakati ni huu sasa kwa wananchi kuchukua jukumu la kuruka mipaka ya kinyama, kwa lengo la kuleta mabadiliko. 

Wananchi wamekwisha kujua kwamba, vyama vingi vya siasa hapa nchini ni matawi ya Chama Cha Mapinduzi, vilivyobuniwa makusudi, ili kuwagawa wananchi wasiwe na nguvu za kuleta mabadiliko ya uongozi wa chama cha siasa nchini. 

Mayowe yote tunayosikia ya udini na mara nyingine ooh ukabila, yanayopigwa na walaghai, ni katika kuendeleza hila za kuwalaghai wananchi, ambao bado wanadhaniwa kuwa ni punguwani,hasa wale wanaoambiwa kwamba hawakusoma. 

Lengo la kundi hili la viongozi,ni kuendeleza dhulma dhidi ya baadhi ya wananchi, kwa sababu ya dini zao, na kwa upande mwingine kupata fursa ya kuendelea kufuja mapato ya taifa kwa kujinunulia magari ya fahari, tafrija zisizokwisha, semina na makongamano, ambayo hayana tija yoyote. 

Stahamala ya kisiasa ndio umekuwa mtihani ulio washinda viongozi wa Chama cha Mapinduzi na serikali yake. 

Kila viongozi hao wanapopata fursa ya kuhutubia wananchi, wanachokifanya ni kushambulia vyama vya siasa vya upinzani, badala ya kutangaza sera za chama chao. 

Wimbo wao ni ule ule uliokwisha kupitwa na wakati.Kila uchao ni amani na utulivu, huku matendo yao yanapingana kabisa na dhana nzima ya maneno wanayotamka. 

Kufutiwa madeni ndio wimbo mpya, pamoja na ahadi za kuboresha maisha ya wananchi katika kipindi kijacho baada ya uchaguzi wa Oktoba 2000, mambo ambayo si kweli, kwa sababu ya kutokuwepo kwa miundo mbinu ya kufanikisha azma hiyo kama ipo. 

Oktoba mwaka huu, ndio utakuwa mwezi wa kutofautisha mchele, na chuya. 


Mandela ni mfano wa kuigwa



KIONGOZI bora ni yule atakayetekeleza majukumu yake kwa ajili ya maslahi ya wananchi wake, ambao ndio walio mwajiri. Kiongozi wa namna hiyo hataweza kuwadunisha baadhi ya raia zake wala hatawakumbuka wakati wa kutafuta kura tu, bali atatumia muda wake kushughulikia matatizo ya wananchi pia.
 

MWANADAMU ana silika ya utiifu, sasa itategemea huyo anayeongoza. Iwapo ataongoza kwa kufuata haki na usawa basi jamii hiyo huwa na mwelekeo mzuri. Lakini iwapo atawagawa katika matapo kwa kuwadunisha baadhi ya raia zake kwa makusudi, basi jamii hiyo itakuwa na chuki na matokeo yake hayatakuwa mazuri. Hapo ndipo itakapokuja dhana ya kutafuta mchawi nje hali ya kuwa wachawi wamo humo humo. 

Afrika ya Kusini ni nchi ambayo imekaa na utawala wa Kibaguzi mpaka kufikia miaka ya 1990, hali ilikuwa mbaya kupita kiasi. Makaburu walidhania kuwa wataendelea kuua, kudhulumu, kunyanyasa, kunyonya na kufanya maovu ya kila aina. Lakini ilifikia hatua wananchi wakasimama imara na kuiondio kadhia kwa kumtaka kiongozi ambaye angewajali na kuwathamini, makaburu waliua raia mpaka wakachoka lakini hali haikuwa shwari. Raia walipambana na utawala wa huo dhalimu mpaka wakaung'oa. 

NELSON MANDELA alikuwa ni kiongozi wa chama cha Upinzani cha ANC.Mandela alipata taabu nyingi mbalimbali na kutothaminiwa utu wake. Aliwekwa gerezani kwa kipindi kirefu. Karibu ujana wake wote aliutumia gerezani akitetea haki za wanyonge. Mandela hakukata tamaa pamoja na vitisho vyote alivyopata. Makaburu walidai kuwa Mandela akiachiwa nchi ataleta vita na hakutakuwa na amani Afrika ya Kusini. Mbinu hiyo haikuwafanya wananchi waache kudai haki zao ambazo ziliporwa na Makaburu. Ili kujua kwamba Mandela ni kiigizo na fundishoitabidi tuangalie dondoo zifuatazo: 

Kwanza Mandela ni shupavu, mvumilivu na asiyetaka matunda ya haraka.Mandela alikaa gerezani kwa muda mrefu na kuvumilia mateso yote yapatikanayo ndani ya gereza. 

Pili Mandela alikuwa na sera za kuondoa ubaguzi wa rangi na kufanya wananchi wajione kuwa ni sawa na wanastahili kuheshimiana na kuendelezwa.Katika utekelezaji wa hilo aliwasamehe wale wote walioendesha sera za ubaguzi, waliomtesa na pengine kutaka kumuua kabisa. Hali hiyo siyo ya kawaida kwa viongozi katika jamii, wengi hutaka kulipiza kisasi au kuwakomoa. Akitokea mtu kutetea haki za wanyonge basi aswekwa rumande na pengine kuuawa. Je watu wangapi wameuawa kwa kudia haki zao? Je hakuna watu wanaozushiwa kesi kwa kutetea wanyonge? Viongozi hawajifunzi kutoka Afrika ya Kusini!. 

Tatu Mandela hakuwa na uchu wa madaraka kama viongozi wengine, aliacha madaraka ya urais baada ya kuongoza muda mchache. Hii ni nadra sana kutokea, kwani viongozi wengi wana uchu wa madarakana kung'ang'ania. Kibaya zaidi wale ambao ni wapinzani huandaliwa mazingira magumu sana kama walivyofanya Makaburu wa Afrika ya Kusini. Vile vile Mandela, alithubutu kumwachia madaraka kwa muda kiongozi wa Upinzani Chief Buthelezi. Ni kiongozi gani anaweza kufanya hivyo? Hata kama kiongozi wa upinzani atakuwa na utaalam kiasi gani, hawezi kushirikishwa katika kuleta maendeleo katika Taifa lake. Leo nchi haina maendeleo kwa sababu ya dhama hiyo, na wananchi wanadanganywa kwa visenti kidogo ambavyo haviwezi kusaidia hata kwa mwezi mmoja, wakati huo mwananchi anauziwa matatizo ya miaka mitano. 

Nne Mandela hakukubali kuchaguliwa rafiki atakayemfaa. Marekani walimkataza Mandela kutembelea Libya kwa sababu iliwekewa vikwazo vya kiuchumi. Lakini alienda na ziara yake nchini Libya ikawa na mafanikio. Alishamwuliza Rais wa Marekani kuwa upolisi wa dunia nani aliyempa. Viongozi wengine wanafanya tofauti, adui wa Marekani atakuwa adui wa viongozi wote bila kufanya utafiti, hata kama adui wa Marekani atakuwa na haki. Mandela hakukubali kuendeshwa kama bendera. 

Tano namna anavyosimamia usuluhishi wa Rwanda,Burundin.k. Tokea achukue wadhifa huo migogoro imechukua sura mpya. Kwa mara ya kwanza wapinzani wa kikabila nchini Rwanda wamekubali kuunda serikali ya pamoja. Jambo hilo sio la kawaida na linafaa kuigwa. 

Hivi sasa takribani nchi nyingi zimeshapata uhuru wao. Lakini namna viongozi wanavyoongoza nchi hizo hakuna tofauti na Makaburu wa Afrika ya Kusini kwani makaburu walianza hivyo mpaka wakafikia kilele. Iwapo wananchi wanakufa na njaa halafu watawala wanakana kuwepo kuwepo kwa hali hiyo.Je viongozi hao wanafaa kuongoza?Serikali inaua wananchi halafu vigogo wanakaa na kupongezana!!Hawa hawatufai. 

Lazima ifahamike kwamba propaganda za nguvu za dola,vitisho vinavyotumiwa na viongozi havitaendelea kuwa hivyo muda wote. Sera za kuwadanganya wananchi kuwa wasiwape wapinzani kura wataleta vita na kuvuruga amani zina mwisho wake. Huwezi kusema kuna amani. Huwezi kusema kuna wakayi raia wanauwawa na viongozi kupongezana, wavuja jasho wakufa na njaa, wananchi wanaishi kwa wasiwasi wa kukamatwa na polisi majumbani mwao na kuambiwa wazururaji, wananchi hawana uhuru wa kujiamlia mambo yao kwa mujibu wa Katiba. Na kero nyingine lukuki. 

Afrika ya Kusini ni fundisho kwa wananchi na viongozi. Hakuna nguvu ya dola inayoweza kushindana na wananchi. Cha msingi wananchi wasifikishwe mahali wakatamani kufa kuliko kuishi. 

Juu
 

YALIYOMO
 

Tahariri
Tume, PCB na vyama vya siasa mmekiona mliochoandaliwa Oktoba?

Cheyo kuendeleza  ‘mfumo Kristo’

Rushwa katika kura za maoni: 'CCM isitafute mchawi'

CUF yakanusha propaganda za waraka

Wanachama wa  CUF kortini  Kilwa

Waumini waapa kulinda Msikiti

KINYANG’ANYIRO CHA UBUNGE: CCM Temeke wamtaka Bazaar

'Wanafunzi Lindi wamshughulikia Mkuu wa Shule aliyewazuia kuswali'

Milioni moja zachangwa kujenga madrasa

Hata na mimi sijala

USHAURI NASAHA
Jinamizi la ukewenza

MAKALA
Kushindwa kujitegemea ni laana

MAKALA
UDP, TLP wathibitisha hisia za Waislamu kuwa Uislamu ni kero Tanzania

MIPASHO NASAHA
Mwanasiasa wa kisasa

Kalamu ya Mwandishi
Mamluki wa mageuzi

MAKALA
Mrema na Cheyo wajihadhari wasije wakatumiwa kuwavuruga wananchi

MAKALA
Viongozi wa vyama vya siasa na udini nchini Tanzania

Mandela ni mfano wa kuigwa

Burudani/Muziki
Cat Stevens: Historia kwa Ufupi

Habari za Kimataifa

LISHE
Yanayoweza kumdhuru mtoto tumboni

MASHAIRI

MICHEZO

  • Jenerali Ulimwengu amgonga nyundo Mkapa
  • Hassan Affif aitabiria Simba Ubingwa

  •  


    Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
    Au
    Andika barua  kwa: nasaha1420@yahoo.com


    Ukurasa wa mwanzo
    Islam Tanzania
    Matoleo yaliyopita