NASAHA
Na. 057 Jumatano  Julai 19 - 25, 2000
Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita
'Wanafunzi Lindi wamshughulikia Mkuu wa Shule aliyewazuia kuswali' 

Na Mwandishi Wetu, Lindi 

WANAFUNZI wa Kiislamu wa shule ya sekondari ya Lindi wamemchukulia hatua mwalimu wao mkuu anayewazuia kuswali Ijumaa kwa kumwandikia barua ya malalamiko Mkuu wa Mkoa wa Lindi.

Hatua hiyo imechukuliwa na wanafunzi hao baada ya kugundua kile walichodai kuwa mwalimu mkuu wa shule anaendesha mbinu za kuwanyima haki ya kuhudhuria swala ya Ijumaa wanafunzi wa Kiislamu. 

"Imekuwa ni kawaida katika shule yetu hii kufanya sherehe za mahafali na vikao vya shule (school Baraza) siku ya Ijumaa wakati wa ibada, bila kujali au kuthamini umuhimu wa siku hiyo kwa wanafunzi wa Kiislamu", imeeleza sehemu ya barua hiyo. 

Barua hiyo iliyoandikwa Juni 26, imemueleza Mkuu wa mkoa kuwa matukio hayo ni uvunjaji wa sheria ya nchi juu ya uhuru wa kuabudu iliyo katika kifungu cha 19 sehemu (1) na (2). 

Na pia ni uvunjaji wa waraka wa serkali wa wizara ya Elimu na Utamaduni wenye Kumbukumbu nambari ED/OK/C.2/4/77 wa 18/08/1999 unaowataka wakuu wa shule kusimamisha shughuli za masomo siku ya Ijumaa kati ya saa 6 - 8 mchana. 

Barua hiyo ambayo NASAHA ina nakala yake na ambayo inamtaja Mkuu wa shule kwa jina la Justine Mwingira imesambazwa kwa Afisa Elimu mkoa wa Lindi, Makatibu wa BAKWATA mkoa na wilaya, TAMSA, BARAZA KUU, wajumbe wa bodi ya shule na kamati ya Kutetea haki za Waislamu Tanzania. 
Juu


Milioni moja zachangwa kujenga madrasa 

Na Mwandisi wetu 

JUMLA ya zaidi ya shilingi moja zimechangwa kupitia harambee iliyoendeshwa katika Ijitimai ya kufana iliyofanyika wilayani Geita mapema mwezi huu.

Waislamu walichanga fedha hizo katika harambee iliyoongozwa na Sheikh Mohammed Issah huku Rais Mstaafu wa Zanzibar Alhaj Aboud Jumbe Mwinyi akiwa mgeni rasmi. 

Kwa mujibu wa Sheikh Issa, fedha hizo zitatumika katika kukamilisha jengo la shule lenye vyumba vitatu vya madrasa. 

Licha ya fedha waumini hao pia waliahidi kwa ridhaa yao kutoa vifaa vya ujenzi kama vile sement, mabati, mchanga, mawe na matofali. 
Juu


Hata na mimi sijala 

Na KhadijaM. Idd 

Ndio, 'hata na mimi sijala, mwananchi' ni maneno yanayotamkwa na Permanent Secretary katika shairi la 'Building the Nation" lililoandikwa na Henry Barlow wa Uganda. Kwa ujumla shairi hili linatupa hadithi ya dereva wa Permanent Secretary (PS) ambaye anatueleza yeye mwenyewe kwamba leo alitekeleza wajibu wake katika kujenga taifa nao ni kumpeleka P.S. kwenye "hafla muhimu."

Dereva huyu anatueleza juu ya hili kwamba hafla hii kwa kweli ilikuwa ni chakula cha mchana ambacho kilikuwa na kila kitu:-bia ,kuku wa kuchoma, mvinyo, ice-cream,kahawa kiasi cha haja. Baada ya mlo huu dereva anamrudisha P.S. ambaye anapiga miayo mingi sana. Sasa ili kujizuia asilale anamuulize dereva wake. Je,umekula rafiki yangu? 

Dereva anamjibu, huku akitabasamu kwa siri, kwamba hajala. Baada ya jibu hili P.S. naye anasema kwamba naye hajala na kwamba alikuwa 'busu' kushughulikia masuala nyeti ya taifa. Kutokana na hali hii ya "kushinda na njaa", P.S. anasema kuwa inamsababishia vidonda vya tumbo . Na kwamba haya ndiyo matatizo ayapatayo katika kujenga taifa. 

Dereva anashangaa na mshangao huu unamuingiza kwenye mawazo ,ambapo anaeleza kwamba vidonda vyake (dereva) vya tumbo vinauma pia lakini tofauti ni kwamba vimesabishwa na njaa na si vyakula visivyona idadi. Shairi linamalizia na kurejea nyumbani kwa wajenzi wawili wa taifa jioni ile wote wakiwa na maumivu makali ya tumbo. Matokeo ya kujenga taifa kila mtu kwa njia yake tofauti. 

Wako viongozi na watendaji wa serikali ambao wana tabia kama za P.S., kutumia mali ya umma kwa maslahi yao binafsi huku wakijitangazia kuwa wanajenga taifa. Wale ambao wanatekeleza wajibu wao hawaonekani na wengine hunyanyaswa kama huyu dereva, hawapewi chakula bali hukejeliwa kwa masuali kama hili lililoulizwa na P.S. 

Unafiki kama huu wa P.S. unaonekana wazi ambapo viongozi wa vyama na serikali hususan wakati huu wa kampeni, ambapo huja na sura ya kuonyesha kwamba wana matatizo kama yetu wananchi wataonekana kama wanajali shida za wananchi na kwamba na wao wanateseka na wengine tunawasikia eti wanamwaga mapesa na misaada katika shida "kujali" shida za wananchi. Lakini watu wanaweza kujiuliza kwamba hivi hali hii haifanani na ile ya P.S. ya kumuuliza dereva wake iwapo amekula,sikwka vile anamjali bali akinyamaza atasinzia. Labda pia hawa wanaotoa misaadasasawanaogopa 'kusinzia'wasije wakakosa kura. Kama ilivyo kwa PS,watu hawa watakapokuwa wanafaidi matunda ya "jasho lao" hawataongea wala kusikika wakitoa misaada. Kama P.S. wataongea watakapomaliza. 

Wakati tunahudhuria mikutano ya kampeni tuwe macho kuna watu watakaotuambia "hata na mimi sijala" ili tuwaone kwamba ni wenzetu kumbe meza wanayotoka imechafuka. Watu hawa wana maradhi mabaya yanayotokana kula mlo, maradhi yetu yanatokana na kukosa chakula. Tuwajue watu hawa na unafiki wao kama dereva alivyomjua P.S. na uongo wake. 

Juu
 
 

YALIYOMO
 

Tahariri
Tume, PCB na vyama vya siasa mmekiona mliochoandaliwa Oktoba?

Cheyo kuendeleza  ‘mfumo Kristo’

Rushwa katika kura za maoni: 'CCM isitafute mchawi'

CUF yakanusha propaganda za waraka

Wanachama wa  CUF kortini  Kilwa

Waumini waapa kulinda Msikiti

KINYANG’ANYIRO CHA UBUNGE: CCM Temeke wamtaka Bazaar

'Wanafunzi Lindi wamshughulikia Mkuu wa Shule aliyewazuia kuswali'

Milioni moja zachangwa kujenga madrasa

Hata na mimi sijala

USHAURI NASAHA
Jinamizi la ukewenza

MAKALA
Kushindwa kujitegemea ni laana

MAKALA
UDP, TLP wathibitisha hisia za Waislamu kuwa Uislamu ni kero Tanzania

MIPASHO NASAHA
Mwanasiasa wa kisasa

Kalamu ya Mwandishi
Mamluki wa mageuzi

MAKALA
Mrema na Cheyo wajihadhari wasije wakatumiwa kuwavuruga wananchi

MAKALA
Viongozi wa vyama vya siasa na udini nchini Tanzania

Mandela ni mfano wa kuigwa

Burudani/Muziki
Cat Stevens: Historia kwa Ufupi

Habari za Kimataifa

LISHE
Yanayoweza kumdhuru mtoto tumboni

MASHAIRI

MICHEZO

  • Jenerali Ulimwengu amgonga nyundo Mkapa
  • Hassan Affif aitabiria Simba Ubingwa

  •  


       Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
    Au
    Andika barua  kwa: nasaha1420@yahoo.com

    Ukurasa wa mwanzo
    Islam Tanzania
    Matoleo yaliyopita