NASAHA
Na. 050 Jumatano Mei 31 - Juni 5, 2000
Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita
Habari za Kimataifaza Kimataifa

Sokoto yaanzisha sheria ya Kiislamu

Lagos, NIGERIA

JIMBO la Sokoto lililopo Kaskazini mwa Nigeria limeanza rasmi Jumatatu wiki hii kutekeleza sharia za Kiislamu, mwaka mmoja tu baada ya Nigeria kurejea katika mfumo wa demokrasia.

Zamfara lilikuwa ni jimbo la kwanza nchini humo mnamo Januari 27, mwaka huu kuanza kutekeleza sharia za Kiislamu licha ya upinzani kutoka kwa Wakristu na serikali ya Shirikisho. 

Mnamo mwezi Februari, jimbo la Kaduna lilifuata nyayo hizo, ambapo ilitokea mapigano yaliyoacha wahanga zaidi ya 1000 kugharimu uhai. 

Upinzani kutoka kwa Wakristu wa Nigeria unatarajiwa kuendelea, huku wakidai kuwa sharia ya Kiislamu kutumika kutoka kiwango cha familia hadi ngazi ya Taifa ni ukiukwaji wa katiba. 

Gavana wa jimbo hilo, Bwana Attahiru Bafawara amewateua mahakimu 43 kuanza kazi katika mahaka zaidi ya 35 jimboni humo. 

Imeelezwa zaidi kuwa baadhi ya makundi ya jumuiya za Wakristu wanaopenda sharia ya Kiislamu itumike wamekwisha arifiwa juu ya mpango huu wa serikali. 


Chechnya yaua askari 66 wa Russia




Moscow, RUSSIA

WAPIGANAJI wa Kiislamu wa Chechnya wiki hii wamewaua askari wapatao 66 wa Russia katika mapigano yaliyotokea mara mbili kusini mashariki mwa Chechnya.

Msemaji wa wapiganaji wa Chechnya, Bw. Movladi Udugov amesema kuwa mapema siku ya Alhamisi walishambulia ngome ya Russia kijijini Betti-Mokhk ambapo katika mapigano hayo waliwaua askari 46 wa Russia na kuwaacha mashahidi wawili wa Chechnya. 

Katika shambulio jingine Alhamisi alasiri, lililofanywa na Russia, Wachechen saba waliuawa na askari wa 20 wa Russia kupoteza maisha. Hiyo ilikuwa huko Zhaini-Vedeno. 

Russia imepinga vikali habari hizo, msemaji wa Rais Vladimir Putin Bwana Sergei Yastrzhemsky alisema huu ni uzushi mtupu. 

Aliongeza kuwa katika kipindi cha saa 24 ziilzopita askari mmoja tu wa Russia amefariki kutokana na kujeruhiwa vibaya. 

Amedai zaidi kuwa helikopta za mabomu zilishambulia na kuua askari 12 wa Chechnya siku ya Alhamisi huko wilaya ya shatoi kusini mwa Chechnya. 

Umoja wa Ulaya unaotarajiwa kuzungumzia suala la Chechnya siku ya Jumatatu katika mkutano kati yake na Russia, Bwana Javier Solona, Mkuu wa Usalama na masuala ya nje ya Umoja wa Mataifa alisema. 

Russia iliivamia Chechnya mnamo Oktoba Mosi mwaka jana kwa lengo la kutaka kutawala. 


Ethiopia, Eritrea zaanza mazungumzo 




Algiers, ALGERIA

MAJIRANI wa pembe ya Afrika, Ethiopia na Eritrea zimeanza hapo jana mazungomzo katika kutatua mgogoro wa mpaka katika vita vilivyodumu miaka miwili sasa.

"Waziri wa sheria wa Algeria Bwana Ahmed Ovyalia alianzisha mazungumzo katika mkutano kati yake na ujumbe wa Ethiopia ulioongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia Bwana Seyeum Mesfin", alisema ofisa mwandamizi wa Algeria.

Ujumbe wa Eritrea unaoongozwa na Waziri wa mambo ya nje Bwana Haile Woldensal. 

Mazungumzo hayo yanasimamiwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Nchi Huru barani Afrika (OAU) Bwana Abdelaziz Boutelfika wa Algeria. 

Bila kutaja ajenda za mkutano afisa mmoja wa Algeria amesema kuwa kati ya siku tatu hadi nne mazungumzo yatamalizika. 

Ethiopia imesema kuwa imeyaondoa majeshi yake kutoka magharibi mwa Eritrea hapo jana ambapo imedai kuwa imewaua, kuwazingira na kuwakamata mateka askari wa Eritrea katika kampeni yake hiyo iliyodai kuwa ilikuwa na lengo la kudhoofisha nguvu za adui za kivita na kuikomboa ardhi. 

Msemaji wa Eritrea Bwana Ymane Gebremeskei amesema, bado anatafuta uhakika wa kujitoa kwa Ethiopia. 

Katikati ya uwanja wa vita inasadikiwa Ethiopia imerudishwa nyuma zaidi ya maili 60 na askari wa Eritrea. 


Clinton ziarani Ulaya 




Lisbon, URENO

RAIS Bill Clinton wa Marekani hapo jana ameanza ziara itakayomchukua katika nchi kadhaa za bara za Ulaya.

Baada ya kuwasili mjini Lisbon, Rais huyo alikuwa na mazungumzo na viongozi wa Ureno katika masuala yanayohusu silaha na hali ya utulivu barani Ulaya pamoja na utafiti wa dawa ya ukimwi. 

Katika ziara, Rais huyo anatarajiwa kuvishwa nishani na umoja wa Ulaya ya Amani, kutokana na mchango wake wa kuleta amani katika migogoro ya Bosnia, Kosovo na Balkan. 

Nchi nyingine anazotarajiwa kuzuru ni Ujerumani, Russia, Ukraine na Ireland ya kaskazini. 

Clinton anatarajiwa kuwasili kesho nchini Ujerumani ambapo licha ya kuvishwa nishani atakuwa na mazungumzo na mwenyeji wake Kansela Gehard Schroeder. 

Hii ni ziara ya 70 tangu ashike madaraka ya Urais takriban miaka saba na nusu hivi sasa, ambapo anatarajia kumaliza wadhifa huo mnamo mwezi Januari mwaka ujao, baada ya kutumika vipindi viwili vya miaka minne minne. 

Akiwa Ujerumani atakutana na waziri mkuu wa Israel Bwana Ehud Barak kuzungumzia suala la amani ya mashariki ya kati, mazungumzo ambayo yalisitishwa wiki moja kabla baada ya kutokea mapigano ukanda wa Gaza. 

Maudhui ya safari ya Bwana Clinton ni kuimarisha masuala ya biashara na usalama. 

Nchini Russia atakutana na Rais Vladimir Putin na kumalizia ziara yake hiyo ya wiki moja kwa kusimama muda mfupi nchini Ukraine. 
 

Juu
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI
Tahadhari ya Warioba juu ya rushwa isipuuzwe

Mkapa afanya ziara Pwani

CCM ‘inaweweseka’ - Sheikh

Zanzibar wadai kuyumbishwa na Bara

Serikali yatoa muelekeo wa Bajeti na kutangaza njaa

Habari za ndani
Wapinzani kusimamisha mgombea Urais mmoja 

SMZ haishughulikii mikarafuu -Maalim Seif

Mwalimu Mkuu Msimbazi Mseto atishia kujiuzulu 

Hizi ni 'arobaini' za mapandikizi

Waislamu Mbeya wamsusa Sheikh Mkuu wa BAKWATA 

Masheikh wa BAKWATA waongoza sherehe za kuwasimika makamanda wa vijana wa CCM 

Wakristo waishitukia CCM

MAKALA
Dini na siasa haviwezi kutenganishwa

Makala 
Mikutano ya Prof. Lipumba 'yaendelea' baada ya kuondoka 

MPASHO NASAHA
MATATA! MATATA!

Kalamu ya Mwandishi 
Wapinzani epukeni patupu 

MAKALA
CCM na sera za maendeleo (6)

Habari za Kimataifaza Kimataifa

Lishe 
Supu na umuhimu wake mwilini

BARUA

MASHAIRI

RIWAYA
Mapinduzi ya fikra - 4 

MICHEZO

  • Uchaguzi Yanga Julai
  • BATA yahimiza usajili michezo
  • 'Simba SC, Singida United baba mmoja mama mbali mbali' 
  • Tarimba akalia Kuti Kavu Yanga

  • Ambari, Mwakipesile wajitosa kugombea DRFA



       Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
    Au
    Andika barua  kwa: nasaha1420@yahoo.com

    Ukurasa wa mwanzo
    Islam Tanzania
    Matoleo yaliyopita