NASAHA
Na. 050 Jumatano Mei 31 - Juni 5, 2000
Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita
Habari za Ndani 

Waislamu Mbeya wamsusa Sheikh Mkuu wa BAKWATA 

Na Mwandishi Wetu 

HABARI kutoka Mbeya zimedai kuwa Waislamu wa mkoa huo wameisusa ziara ya Sheikh Mkuu wa BAKWATA naujumbe wake.

Habari hizo zimemnukuu Sheikh Duru Mahamed wakati akitoa khutuba ya Ijumaa katika msikiti wa Ijumaa uliopo barabara ya 8,mjini Mbeya. 

Katikakhutuba hiyo Sheikh Mohammed aliwalaumu Waislamu wa mkoa huo kwa kitendo chao cha kukataa kuupokea na kuhudhuria katika mikutano ya Sheikh huyo mkuu wa BAKWATA. 

Sheikh Duru Mohammed alilaumu kwamba hata wale waliopewa kadiza mwaliko nao pia hawakuhudhuria. 

Kwa mujibu wa maoni ya Waislam mjini Mbeya walidai kuwa hawakuhudhuria katika mapokezi na mikutano ya ujumbe wa BAKWATA kwa sababu ilielezwa kuwa ujumbehuo ni ugeni wa Mkuu wa Mkoa. 

Waislamu hao walidai kwamba hawawezi kujikurubisha na Sheikh aliekaribu na serikali iliyopuuza mauaji ya Mwembe Chai. 

Waislam wengine mkoani humo walidai kuwa ziara hiyo ya Sheikh Mkuu wa BAKWATA na ujumbe wake walisusa kwa kuwa ilisemekana kuwa lengo lake ni kuipigia debe CCM. 


Masheikh wa BAKWATA waongoza sherehe za kuwasimika makamanda wa vijana wa CCM

Na Mwandishi Wetu 

Habari zilizotufika kutoka Mwanza zimedai kwamba Masheikh wa BAKWATA wa Mkoani humo wako mstari wa mbelekatika sherehe za kuwasimika makamanda wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani humo.

Kwa mujibu wa habari hizo CCMimesimika makamanda wa vijanakatika matawi mbali mbali katika Manispaa hiyo. Mwishoni mwa wiki iliyopita. 

Habari hizo zinazidi kudai kuwa katika sherehe zilizofanyika katika tawi la Pamba, kiongozi wa BAKWATA Sheikh Ramia alipewa fursa ya kutoa salam za chama chake. 

Katika ufunguzi wa tawi la Kirumba, viongozi wa BAKWATA walioshiriki katika sherehe hizo ni pamoja na Sheikh wa Mkoa, Sheikh wa wilaya na Katibu Mkuu. 

Kitendo cha Masheikh hao wa BAKWATA kushiriki kikamilifu katika sherehe za CCM hazikuwawashangaza Waislam mkoani humo kwa maelezo kuwa ni sawa na siasa ya Sheikh Mkuu, Hemed bin Juma anayoifanya nchi nzima, ambapo inadaiwa anapokewa na baadhi ya viongozi wa serikali. 

Hata hivyo,Waislamu wengi wa mji wa Mwanza wamesikitishwa na tabia ya masheikh hao wa BAKWATA kushiriki katika baadhi ya mambo ya kimila ambayo yanapingana na imani ya dini ya Kiislam. 

Mwaka 1983 vijana wa CCM pamoja na sungusungu walimwadhibu Imam wa Msikiti wa Buzuluga, Mwanza kwa kukataa kushiriki katika mila ya kuabudu jua. 

Sheikh huyo alipigwa na kuchaniwa vitabu vyake vya Qur'an. Wakati Waislam wote nchini walilaani kitendo hicho, Sheikh Mkuu wa BAKWATA alipinga na kusema Qur'an haikuchanwa isipokuwa "kiji-yasin." 


Wakristo waishitukia CCM

Na Mwandishi Wetu
 

KUTOWEKA kwa kanda iliyorekodi mahojiano ya Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zakaria Kakobe, katika kipindi cha Televisheni cha Kiti Moto kumezua tuhuma nzito dhidi ya serikali na chama tawala ambapo Wakristo waliojitambulisha kuwa ni wa madhehebu yasiyo ya kikatoliki nchini wanadai kuwa CCM ina agenda maalum na Kanisa Katoliki nchini ya kuwatenga waumini wote wasiokuwa Wakatoliki wasishiriki katika uongozi wa nchi.

Madai hayo yametolewa na baadhi ya Wakristo wa madhehebu ya Kiprotestanti kufuatia taarifa za madai kwamba Chama cha Mapinduzi kimehusika kuzuia kuoneshwa katika televisheni kwa kanda hiyo kama ilivyo kawaida ya utangazaji wa kipndi hicho maarufu. 

Kipindi cha Kiti Moto hutayarishwa na Maasai Studio na kutangazwa na kituo cha television cha binafsi cha DTV cha jijini Dar es Salaam kila siku yaAlhamisi usiku. Mahojiano hayo ya Askofu Mkuu Kakobe yalirekodiwa Jumanne, Mei 16, mwaka huu na yalitarajiwa ktangazwa hewani na kituo hicho cha televisheni alhamisi, Mei 18. Mpaka sasa si Maasai Studio wala DTV waliothubutu kueleza sababu za kukwama kwa kipindi hicho. 

Waprotestanti hao wamedai kuwa wakatoliki wamediriki kutunga kitabu kueleza udhaifu wa wanasiasa walio madarakani na serikali yao lakini hakuna kiongozi wa serikali wala wa CCM se aliyethubutu kuwakemea. Lakini, wameendelea kudai waporestata hao, "(Askofu) Kakobe kusema imekuwa nongwa... mara kaongea (Emmanuel) Nchimbi, mara kaongea (Philip) Mangula". 

Bw. Emmanuel Nchimbi ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM na Bw. Philip Mangula ni Katibu Mkuu wa CCM. 

Aidha, Wakristo hao wamedai kwamba madai ambayo yamekuwa yakitolewa na Waislamu kwamba wanadhulumiwa na Wakristo hayawahusishi Wakristo wote. 

"Tena ndugu zetu Waislamu wanaposema wanadhulumiwa na Wakristo wasituchanganye sisi wote... wanaowadhulumu ni hawa hawa Wakatoliki", amedai mzee mmoja aliyejitambulisha kuwa ni muumini wa Kianglikana.

Mzee huyo, Bw.Mdoe, aliendelea kueleza kwamba wao Waanglikana ni watu wenye kupenda elimu na kuongeza kwamba wakati wa mkoloni wa Kiingereza wao walikuwa wameshika nafasi nyingi serikalini lakini sasa "tumeenguliwa kwa mpango maalum wa siri". 

Wamedai kwamba kwa mpango huo wa siri hata wanasiasa mashuhuri hapa nchini wamewahi kunyimwa uongozi wa nchi kwa sababu tu wao si wakatoliki. 

Wamemtaja Bw. John Malecela ambaye ni muanglikana kuwa amewahi kunyimwa kugombea urais kwa sababu yeye si mkatoliki. 

"Mzee Malecela ni mzoefu sana wamenyima urais wakati amekwishawahi kuwa Waziri Mkuu na (pia) waziri wa kawaida..., amekuwa Makamu wa Rais na Makamu wa Mwenyekiti wa hiyo hiyo CCM. 

"Tena ni mtu mashuhuri duniani, alikuwa balozi wetu Uingereza na alichaguliwa miongoni mwa watu wenye busara kutoka Commonwealth kutafuta ukombozi wa Afrika ya Kusini", alisema Bw. Mathias Mbegu na kusisitiza kuwa katika watu hao ambao idadi yao ilikuwa ni saba, waliotoka Afrika walikuwa ni wawili tu ambao ni Malecela mwenyewe na Rais wa sasa wa Nigeria Generali Mstaafu Olusegen Obasanjo. 

Wakristo hao wamedai pia kuwa mtu mwingine ambaye amekuwa akibughudhiwa na serikali kwa sababu tu yeye si mkatoliki ni Mchungaji Christopher Mtikila. 

"Tangu Mtikila ajitokeze na kuikosoa serikali hadharani amekuwa akibughudhiwa sana na serikali,... lakini cha ajabu ni kuwa maaskofu wa Wakatoliki wameikosoa serikali na kuiacha karibu uchi lakini hakuna aliyewagusa" alisema mmoja wa Wakristo hao. 

Mchungaji Mtikila ni Kiongozi wa kikundi cha kidini cha Liberty Desk na pia ni kiongozi wa chama cha siasa kilichonyimwa usajili cha Democratic Party. Hivi sasa Mchungaji huyo anatumikia kifungio cha mwaka mmoja jela baada ya kupatikana na hatia ya kumkashifu aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Tanganyika na baadaye Tanzania Hayati Mwalimu Nyerere. 

Tuhuma hizi za Waprotestanti zinakuja wakati ambapo CCM na viongozi wamekuwa wakikemea udini katika vyama vya siasa ingawa mambo yanayodaiwa kufanywa na chama hicho tawala ni tofauti na makemeo ya viongozi wake. 

Wakristo hao wasio Wakatoliki wametahadharisha kwamba kwa mwenendo huo wa CCM na serikali yake nchi inapelekwa pabaya. 

"Tunawaomba ndugu zetu Waislamu watuelewe kwamba wanaoipeleka nchi pabaya ni Wakatoliki,... na kama wapo wenzetu (Waprotestanti) wanaoshiriki hayo basi ni wachache...", alieleza mmoja wao. 
 

Juu
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI
Tahadhari ya Warioba juu ya rushwa isipuuzwe

Mkapa afanya ziara Pwani

CCM ‘inaweweseka’ - Sheikh

Zanzibar wadai kuyumbishwa na Bara

Serikali yatoa muelekeo wa Bajeti na kutangaza njaa

Habari za ndani
Wapinzani kusimamisha mgombea Urais mmoja 

SMZ haishughulikii mikarafuu -Maalim Seif

Mwalimu Mkuu Msimbazi Mseto atishia kujiuzulu 

Hizi ni 'arobaini' za mapandikizi

Waislamu Mbeya wamsusa Sheikh Mkuu wa BAKWATA 

Masheikh wa BAKWATA waongoza sherehe za kuwasimika makamanda wa vijana wa CCM 

Wakristo waishitukia CCM

MAKALA
Dini na siasa haviwezi kutenganishwa

Makala 
Mikutano ya Prof. Lipumba 'yaendelea' baada ya kuondoka 

MPASHO NASAHA
MATATA! MATATA!

Kalamu ya Mwandishi 
Wapinzani epukeni patupu 

MAKALA
CCM na sera za maendeleo (6)

Habari za Kimataifaza Kimataifa

Lishe 
Supu na umuhimu wake mwilini

BARUA

MASHAIRI

RIWAYA
Mapinduzi ya fikra - 4 

MICHEZO

  • Uchaguzi Yanga Julai
  • BATA yahimiza usajili michezo
  • 'Simba SC, Singida United baba mmoja mama mbali mbali' 
  • Tarimba akalia Kuti Kavu Yanga

  • Ambari, Mwakipesile wajitosa kugombea DRFA



       Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
    Au
    Andika barua  kwa: nasaha1420@yahoo.com

    Ukurasa wa mwanzo
    Islam Tanzania
    Matoleo yaliyopita