NASAHA
Na. 050 Jumatano Mei 31 - Juni 5, 2000
Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita
MAKALA

CCM na sera za maendeleo (6)

Uongozi wa nchi hupatikana kwa nguvu?

Anuani ya makala ya leo inawakilisha swali, ambalo wananchi wanajiuliza kuanzia siku Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipotamka kwamba "Atatumia nguvu zake zote kuhakikisha kuwa chama chake kinaendelea kushika hatamu ya kuongoza nchi." Mwandishi RAJAB KANYAMA anaendelea...

KIMANTIKI, nguvu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni vyombo vya serikali, pamoja na majeshi ya ulinzi,ambayo yeye ni Amiri Jeshi Mkuu. 

Wananchi wameingiwa na hofu kubwa, maana matamko hayo ni tangazo la vita dhidi ya vyama vya upinzani, au mtu yoyote ambaye ataonekana kuwa ni kikwazo kwa chama tawala kutimiza azma yao ya kushika hatamu za uongozi wa nchi. 

Matokeo ya siku za hivi karibuni, wakati wa uchaguzi mdogo wa marudio ili kumpata Mbunge wa Jimbo la Kigoma mjini, Polisi walipoendesha msako wa nyumba hadi nyumba na kushambulia wananchi, na mashambulizi ya wananchi, waliodhaniwa kuwa ni wanachama wa Chama Cha Wananchi (CUF) yaliyofanywa na Polisi huko Zanzibar, yanatilia mkazo hofu hiyo. 

Wachunguzi wa mambo ya kijamii wanaeleza kwamba, matamshi ya aina hiyo ni hatari, kwa sababu yanafanya wananchi waanze kuamini kwamba, vyombo vya serikali vipo kwa ajili ya kulinda maslahi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali yake, badala ya wananchi na mipaka ya nchi yao. 

Jambo hili, wachunguzi wanasema linapanda mbegu mbaya, ya chuki, kati ya wananchi na watendaji katika vyombo hivyo. 

Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi, wamepamba moto kuendesha kampeni za kashfa, kejeli na matusi dhidi ya wananchi, wanaojaribu kuwazindua wananchi wenzao, juu ya umuhimu wa kuchagua viongozi bora, pamoja na baadhi ya vyama vya upinzani, hasa vile vinavyoonekana kuwa sasa, vinakubalika na wananchi wengi. 

Vitisho na kejeli, ni sera ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi, nina kumbuka tukio la mwezi wa Agosti mwaka 1999 wakati wabunge halipokuwa wanajadili makadirio ya fedha ya matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais, kwa mwaka huo, ambapo niliachwa hoi. 

Mbunge wa Mtera, kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Mhe. John Malecela,alisimama na kuwataka Wapemba, waache kujishughulisha na mambo ya siasa, na warudi Chake Chake, kuuza mchele na kanga." 

Japo kuwa maneno hayo, yalikuwa ni ya kibaguzi,yaliyojaa chuki na uchochezi, wabunge wa Chama Cha Mapinduzi, kama ilivyokawaida yao walishangilia kwa makofi na vicheko. 

Cha kushangaza ni kwamba, Mzee Malecela alipandisha jazba, baada ya Mbunge wa Vitongoji Mhe. Nassoro Juma, kueleza kwamba, njia pekee ya kupata aina ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, unaofaa ni kwa wananchi kupiga kura ya maoni. 

Kwa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali yake, tofauti za maoni na upinzani wa kisiasa ni uadui kati ya mtu na mtu, au chama na chama kingine, inatisha. 

Inapofika wakati wa maandalizi ya kupata kula, mipaka hutoweka, wapiga debe, hupasha mikwasa moto. 

Matamshi ya Mhe. Nchimbi, Mwenyekiti wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi, kwamba "atakae chukua fomu ya kugombea nafasi ya urais kwa tiketi ya CCM, baada ya Mwenyekiti wake kuchukua, atazomewa mpaka akihame chama", ni ushahidi tosha wa nukta iliyotangulia. 

Demokrasia ndani ya chama, ni jambo lisilokubalika ndani ya Chama Cha Mapinduzi. 

Ni hii ndio sababu, hata chaguzi zinazofanywa ndani ya Chama Cha Mapinduzi, mara nyingi ni za mizengwe mizenwe, na ghilba tupu. 

Mara zote, nia ya wagombea huwa ni kupata madaraka na sio kuongoza kwa sera za kuinua wananchi. 

Ndio sababu hata sera iliyokiweka Chama Cha Mapinduzi madarakani mwaka 1995, imeachwa, kwa maelezo kwamba haitekelezeki. 

Yote haya yanafanyika katika mazingira ya kudumaa kwa maendeleo ya nchi, kielimu na kiuchumi. 

Katika taarifa ya Benki ya Dunia na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Watoto(UNICEF) ya mwaka 1999, umeelezwa kwamba, asilimia 50 ya familia hapa nchini, ni maskini, na asilimia 36 kati ya familia hizo, haziwezi kumudu mahitaji muhimu yanayotambuliwa na jamii. 

Taarifa hiyo iliongeza kwamba, watoto wanaoingia shule wamepungua sana, zaidi ya watoto milioni 2,000,000 wanaopaswa kwenda shule, hawapelekwi. 

Kwa takwimu hizo, Tanzania iko nyuma mno kielimu, ikilinganishwa na Uganda, Kenya na Ethiopia. 

Kwa viongozi wa Chama Cha Mainduzi, hili si jambo la kutisha linalostahili kutengenezewa mikakati maana wao wanaouwezo wa kupeleka watoto wao nje kwa masomo ili kesho na kesho kutwa waje kurithi madaraka ya baba zao. 

Wananchi, tunatakiwa kuzingatia mambo yote haya, wakati wa kupiga kura mwezi Oktoba mwaka huu, ili kwa nguvu zetu, ambazo ni utashi na kura zetu, tukiondoe Chama Cha Mainduzi madarakani, na kukipa chama kingine hatamu ya uongozi wa nchi yetu, kwa matumaini kwamba tutapata maendeleo tunayoyataka. 

Kukirudisha Chama Cha Mapinduzi madarakani, ni kukubali kuwa thamani ya maisha yetu ni, pilau, vikoi na kanga, kama Mheshimiwa Mangula,Katibu Mkuu wa CCM, alivyowahi kusema. 

Je,tuko tayari kuendelea kunyanyaswa kwa karamu za pilau na vikoi? 
 

Juu
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI
Tahadhari ya Warioba juu ya rushwa isipuuzwe

Mkapa afanya ziara Pwani

CCM ‘inaweweseka’ - Sheikh

Zanzibar wadai kuyumbishwa na Bara

Serikali yatoa muelekeo wa Bajeti na kutangaza njaa

Habari za ndani
Wapinzani kusimamisha mgombea Urais mmoja 

SMZ haishughulikii mikarafuu -Maalim Seif

Mwalimu Mkuu Msimbazi Mseto atishia kujiuzulu 

Hizi ni 'arobaini' za mapandikizi

Waislamu Mbeya wamsusa Sheikh Mkuu wa BAKWATA 

Masheikh wa BAKWATA waongoza sherehe za kuwasimika makamanda wa vijana wa CCM 

Wakristo waishitukia CCM

MAKALA
Dini na siasa haviwezi kutenganishwa

Makala 
Mikutano ya Prof. Lipumba 'yaendelea' baada ya kuondoka 

MPASHO NASAHA
MATATA! MATATA!

Kalamu ya Mwandishi 
Wapinzani epukeni patupu 

MAKALA
CCM na sera za maendeleo (6)

Habari za Kimataifaza Kimataifa

Lishe 
Supu na umuhimu wake mwilini

BARUA

MASHAIRI

RIWAYA
Mapinduzi ya fikra - 4 

MICHEZO

  • Uchaguzi Yanga Julai
  • BATA yahimiza usajili michezo
  • 'Simba SC, Singida United baba mmoja mama mbali mbali' 
  • Tarimba akalia Kuti Kavu Yanga

  • Ambari, Mwakipesile wajitosa kugombea DRFA
     
     


       Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
    Au
    Andika barua  kwa: nasaha1420@yahoo.com

    Ukurasa wa mwanzo
    Islam Tanzania
    Matoleo yaliyopita