|
Na. 050 Jumatano Mei 31 - Juni 5, 2000 |
|
|
|
|
|
S.L.P. 72045, Simu: 0811 - 600145, Dar es Salaam Tahadhari ya Warioba juu ya rushwa isipuuzwe Jaji Joseph Sinde Warioba akiongea katika Chuo Kikuu cha Dar es Saaam hivi karibuni aliItuhumu serikali kwa kuzembea katika suala zima la kupambana na rushwa iliyokithiri hapa nchini. Alisema kuwa hatua zinazochukuliwa na serikali katika vita vyake dhidi ya rushwa ni za shabaha ya mbali na matokeo yake ni rushwa kupamba moto katika jamii ya Watanzania na akaonya kuwa nguvu za kupambana na rushwa zisipoelekezwa kwenye kuwasafisha viongozi wa juu nchi itabakia katika nadharia na propaganda zisizokwisha juu ya kupambana na rushwa. Kauli hiyo ya Jaji Warioba imekuja wakati ambapo jamii ya Watanzania imeathiriwa vibaya na rushwa kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya Taifa hili. Tanzania hivi sasa inaongoza kwa kuwa ya tatu kwa rushwa miongoni mwa nchi za Kiafrika na ya saba katika dunia. Athari ya kukithiri huko kwa rushwa inaonekana waziwazi katika nyanja mbali mbali za maisha ya Watanzania ambapo huduma mbali mbali kama vile za afya, elimu, ajira na sekta nyinginezo hutolewa kwa rushwa. Kauli ya Jaji Warioba kuwa wengi wa viongozi huingia madarakani kwa kutoa rushwa katika chaguzi mbalimbali kuanzie zile za udiwani, uwakilishi na hata ubunge, inaibua hisia zaidi za wananchi hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2000, ya kupatikana viongozi bomu na wasio waadilifu na wenye kula rushwa ambao hawataweza kupambana na rushwa kwa vitendo zaidi ya maneno. Ni jukumu na wajibu wa wananchi kuitilia maanani
tahadhari ya Jaji Warioba juu ya kuwa macho na wale wenye kuingia madarakani
kwa kutoa rushwa.
|
YALIYOMO
TAHARIRI
Zanzibar wadai kuyumbishwa na Bara Serikali yatoa muelekeo wa Bajeti na kutangaza njaa Habari za ndani
SMZ haishughulikii mikarafuu -Maalim Seif Mwalimu Mkuu Msimbazi Mseto atishia kujiuzulu Hizi ni 'arobaini' za mapandikizi Waislamu Mbeya wamsusa Sheikh Mkuu wa BAKWATA Masheikh wa BAKWATA waongoza sherehe za kuwasimika makamanda wa vijana wa CCM MAKALA
Makala
MPASHO NASAHA
Kalamu ya Mwandishi
MAKALA
Habari za Kimataifaza Kimataifa Lishe
RIWAYA
|
|
|
|
|