|
Na. 049 Jumatano Mei 24 - 30, 2000 |
|
|
|
|
|
Mapinduzi ya fikra - 4 MTUNZI: ABU FIRDAUS Wakiwa wamefika Jangwani wakielekea hospitali Muhimbili, Mama Luqman alipepesa macho kulia na kushoto kisha alitoa shahada "Ash-hadu an Ilah ilaha illah ila wa ash-hadu anna Muhammad Rasurullah". Kisha alishusha pumzi kwa nguvu na kukata roho.Rahma alishtushwa na kutulia kwa mama yake, alijaribu kusikiliza mapigo ya moyo yaliyokuwa yakienda kasi, moyo ulikuwa umetulia huku joto lamwili likitoweka taratibu. Alimkumbatia marehemu mama yake katutangulia, alilalama kwa uchungu. Sikuiliyofuata, Luqman alimuandikia barua mjomba wake kumueleza yale waliyokusudia. Mjomba wake alipojibu, alikuwa yuko tayari kuendelea kumsomesha Omar pamoja na hali ngumualiyokuwa nayo. Luqman kwa upande wake, alianza kufanya pilika huku na kule ili kutafuta fedha za ada ili amlipie Rahma na Lulu. Pindi muda wa kuanza masomo utakapoanza. Alikuwa tayari kufanya kazi ya aina yeyote ilimradiapate fedha za kuwasomesha waodogo zake. Haikuchukuwa muda mrefu akawa amepata kibaruacha kubeba zege katika kmapuni moja ya ujenziiliyokuwa inajenga majengo mawili makubwa katikati ya mji. Luqman alifurahi fedha alizokuwa analipwa takriban elfu kumi na tano kwa wiki. Aliendelea na kazi hii kwa muda wa wiki tatu na siku nne.Siku hiyo alikuja muhandisi wa jengo ambaye alikuwa anapenda sana kwa karibu na wafanyakazi na hata kufanya nao mas-hara hasa wakati wa chakula. Muhandisi alianza baada ya muda aliinuka na kumfuata Luqman ambaye alikuwa amekaa kwa kujitenga. Alinawa mikono na kuanza kula naye chakula huku akimuagiza muuzaji (mama ntilie)awaongezee chakula kingine. "Umejitenga kusudi msile chakula chako." Alitania mhandisi. "Si hivyo basi, nina matatizo mengi ambayo yananifanya nikae pembeni."Unataka kuumba mtu? Aliendelea kudhihaki mhandisi. Luqman alikuwa kimya kwa dakika kadhaa. Luqman unamawazogani mbona mnyonge? Aliuliza muhandisi, naomba unieleze shida yako na kama ntaweza kukusaidia niko tayari kufanya hivyo, alimbembeleza Luqman. Ni habari ndefu inahitaji muda wa kutosha kukueleza, alijibu Luqman basinaomba tuonane ofisini saa tisa baada ya kumaliza kazi. Sawa bosi, alijibu kwa kifupi Luqman.Na bosi alinawa na kuondika. Wafanyakazi walirejea kazini mpaka saa nane na nusu kisha walianza kunawa na wengine kuoga kisha kuondoka. Luqman alibisha hodi ofisini kwa bosi yapata saa tisa na dakika mbili. Bosi (Yusuph) alimkaribisha kwenye kiti. Bosio Yusuph aliacha kazi zote na kuanza kumsikiliza Luqman. Luqman alimueleza juu ya misiba ya wazazi wake, matatizo waliyokumbana nayo, majukumu yanayomkabiri na kumwambia kuwa ni kutokana na majukumu hayo hakujali kuwa ana elimu ya FTC hivyo asibebe zege. Umemaliza FTC? Aliuliza bosi Yusuph, ndio alijibu Luqman. Unachetiapana vyeti havijatoka, ila nina "slip result’. KweliLuqman ana majukumu mazito. Sasa mimintakusaidia vitu viwili, kwanza ntakusaidia kumsomesha mdogo wako mmoja na wewe utamsomesha aliyesalia. Iliuweze kumudu kumsomesha huyo mmoja aliyesalia, ntakubadilishia kitengo. Kesho asubuhi ukifika njoo moja kwa moja uofisini saa mbili na karatasi yako ya matokeo ya mitihani yako ya FTC. Ntashukurusana bosi. Usiowe na wasiwasi Luqman, wewe ni ndugu yangu. Waliagana na Luqman akaondoka huku akiwa na furaha tele. Alifika nyumbani na jioni ileile aliwaita wadogo zake na kuwaeleza yale aliyoongea na bosi. Wote walifurahi na kuombadua. Sikuiliyofuata, Luqman alifika ofisini kwa bosi Yusuph yapata saa moja na nusu, muda ambao huwasilivibaru. Aliendelea kumsubiri bosi mpaka yapata saa mbili narobo, ambapo bosi aliwasili. Walisalimiana na bosi alifungua mlango na kumkaribisha ndani Luqman. Baada ya kufanya mazungumzo na kukabidhiwa kivuli cha matokeo, alimwambia angempeleka katika maabara yaudongo, na kwamba mshahara wake utakuwa shilingi efu tisini na nauli shilingi elfu kumi. Hivyo atapata shgilingi laki moja kila mwezi. Luqman alimshukuru sana bosi. BosiYusuph alisimama na kuongozana naye mpakja maabara na kumtambulisha kwa wezake. Luqman alianza kuchapa kazi kwa moyo wote hata wenzake walimsifia kwa juhudi yake. Kadri ya miezi ilivyokwenda Luqman alizidi kujiwekea akiba, alutumiashilingi elfu moja tu kila siku. Hivyo alikuwa na akiba ya shilingi elfusabini kila mwezi. Muda wa miezi mitatu tangu Luqman aanze kazi, muda wa Rahman kuanza masomo ya kidato cha tano uliwadia. Luqman alimpeleka dada yake shuleni na kumlipiaada ya miezio sita, shilingi laki moja na elfu ishirini. Luqman aliendelea kumsomesha dadayake huku Luluakilipiwa ada na matumizi mbalimbali ya shule na bosi Yusuph. Omar aliendelea kupokea ada yashule kutoka kwa mjomba wao. Mbali na kumlipiaada Rahma, Luqman alikuwa na jukumu la kuuhudumiafamilia kwa chakula na mahitaji mengine. Alimthamini sana mama Suleiman kwa mchango alioutoa mpaka kufikia wakati ule. Matokeo ya mtihani yalipotoka, Omar alipata daraja la pili katikamtihani wake wa Kidato cha Nne, alichaguliwa kujiunga kidato cha tano katika shule ya sekondari Tambaza. Rahama kwa upande wake alisoma kwa bidii, japo alikumbana navishawishivingi ambavyovilitosha kuwa chachu ya kumfanya apoteze muelekeo, lakini Rahma aliendelea kuzingatia masomo. Hakutamanikupata kitukilicho nje ya uwezo wake. Muda uliwadia wa Rahma kufanya mtihaniwa Kidato cha sita. Alimaliza masomo yake na kumuacha Omari akiingia kidatocha sita. Kwa upande wa Lulu ambaye alikuwa kidato cha tatu, alikuwa Lulu kwelikweli. Alikuw anyota wa kutumainiwa shuleni kwao. Baada ya matokeo kutangazwa,Rahma ambaye alijuwa anasoma uchumi, jiografiana hesabu. Alipata daraja la kwanza pointi nane, na kujiunga na Chuo Kikuu kusomea shahada ya kwanza ya uchumi. Kutokana na posho walizokuwa wanalipwa ple chuoni, Rahma sasa aliweza kujikimu bila kuhitaji fedha kutoka kwa kaka yake. Mwaka mmoja baadae, Omar naye alifanya mtihani wa kidatocha sita. Omar yeye alisomafizikia, kemia na hesabu. Matokeo yalivyotoka, Omar alipata daraja la kwanza pointi nne. Akiwa ameomba kujinga naChuo Kikuu cha Dar es Saaam, Omar alipata nafasi ya kwenda nchini Marekani kusomea kompyuta. Hivyo Omari alishauriana na nduguzek na kufikia uamuzi wa kutokwenda Marekani. Kwakuwa moja, anahitajika kumsaidia Lulu kitaaluma pamoja na vijana wengine, pili waliona si vizuri yeye kwenda huko kwa kuwa vijana walio wengi waendapo huko hupoteza maadili mema ya dini zaowaliyolelewa. Hivyo Omar alijiunga na ChuoKikuu cha Dar es Salaamkusomea kompyuta. Baada ya kuona mzigo aliokuwa nao umepungua, Luqman nayealijiandikisha kusomea shahada ya kwanza ya sayansinaelimu, katika Chuo Kikuu huria. Hivyo kila atokapo kazini aliwahi nyumbani kujisomea. Rahma alimaliza shahada ya kwanza na ya pili katika chuo kikuu cha Dar es Salaam, naOmar alisomashahada ya kwanza tu, ya kompyuta. Baada ya kumaliza masomo yao, Rahma aliajiriwa na kampuni yauuzaji vyombo vya nyumbani kutokaSaudia Arabiakama meneja maozu. Na Omari alijiriwa katika kampuni moja iitwayo "Yasir Computer system management’ ya hapa jijini. Lulu kwa upande mwinginealiamua kusomea udaktari baada ya kupata daraja la pili pointi kumi na mbili katika mtihani wake wa kidato cha sita. Akiwa kidatocha tanona sita, Lulualiendewlea kuwa nyota katika masomo ya kemia na Bilojia. Baada ya kuwa wote wamehitimu isipokuwa Lulu tuambaye
alikuwa mwaka wa nne pale Chuo Kikuu cha Muhimbili, Luqman aliandaa chai
ya jioni nyumbani kwakeSinza. Walikutana baada yasala ya Magharibi. Walizungumza
mengi ya kufurahisha, lakini kubwa katika mazungumzo yao, walikumbushana
safari yao kuanzaia kufiwa na wazazi, Rahma kumwagiwa chakula chake, Luqman
kuvunjiwa kibanda pale Magomenina kuporwa biashara pale Kariakoo na kikao
chao kilichotoa maamuzi waliyoyaita "maamuzi ya busara" ya kuamua kusoma
katika mazingira magumu na kuwa na subira. Lakini leo wanazungumza kila
mtuakiwa naelimu ya kutosha, maisha mazuri naanamuabuduMolawake bila mawazo
ya kulala njaa. Baada ya historia hiyo iliyochangiwa na kila mmojakadri
alivyokumbuka, "kweli usia aliotupa Mama kuwa tuishikimapinduziulikuw anao
ni usia wa kimapinduzi. Alisema Lulu, na wote wakamuunga mkono. Walimaliza
kunywa chaia, wakaombaduakwa pamoja naksiaha wakatawanyika majumbani mwao.
|
YALIYOMO
TAHARIRI
Chuo Kikuu Dar wafanya mitihani katika Bwalo la chakula Udini wa CCM utaisambaratisha nchi -Tambwe ‘Kutoweka’ kanda ya Kakobe: CCM yatuhumiwa Maalim Seif awaambia Wazanzibari: Wenye mamlaka ya kumuweka mtu Ikulu ni wananchi Mkapa afurahia maendeleo Pwani ‘Zawadi’ ya Uchaguzi yatishia kusambaratisha taasisi ya Kiislam Tanga Serikali yakemea mwanamke kudhalilishwa Ushauri Nasaha
MAKALA
Makala
Kalamu ya Mwandishi
MAKALA
Makala
Makala
RIWAYA
Lishe
|
|
|
|
|