NASAHA
Na. 049 Jumatano Mei 24 - 30, 2000
Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita
Maalim Seif awaambia Wazanzibari:
Wenye mamlaka ya kumuweka mtu Ikulu ni wananchi
  • Msikubali kuletewa mtu wa ‘hewala bwana’
Na Mwandishi Wetu

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Mhe. Seif Shariff Hamad amewataka viongozi wa CCM kufahamu kuwa wananchi ndio wenye uwezo na mamlaka ya kumuweka madarakani mtu na chama wanachokitaka wao na si vinginevyo.

Maalim Seif aliyasema hayo Mei 21, mwaka huu katika viwanja vya Malindi mjini Zanzibar alipokuwa akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara wa chama chake.

Kauli hiyo ya Katibu Mkuu wa CUF ambaye anatarajiwa kuwa mgombea pekee wa chama hicho wa kiti cha Urais wa Zanzibar imekuja kufuatia kauli ya Mwenyekiti wa CCM Mhe. Benjamin William Mkapa kuwa hawatakiachia chama kisicho na ridhaa ya ASP na TANU kuiongoza Tanzania.

Chama cha Mpinduzi kilizaliwa mwaka 1977 kwa kuunganisha vyama vya TANU na ASP.

Maalim Seif alisema kuwa sheria iliyoanzisha mfumo wa vyama vingi vya siasa inataka chama kisiwe na mafungamano na vyama vya zamani, lakini kwa mshangao Mwenyekiti wa CCM anatamka hadharani kauli inayokwenda kinyume na sheria hiyo wakati wao ndio walioipitisha.

"Ni nani huyo hasa ambaye wananchi wakishaamua kuiweka CUF madarakani atazuia", aliuliza Maalim Seif na kuongeza kuwa hakuna mamlaka inayozidi maamuzi ya wananchi, kwani wao ndio wenye maamuzi ya mwisho.

Aliwatanabanisha Wazanzibari kuwa macho na kukataa Rais wa kupendekezwa na Bara kwani mara nyingi huwa wanatekeleza kila jambo linaloamuliwa hata kama halina manufaa kwa Zanzibar.

"Analotaka Bw. Mkapa ni mumchague mtu ambaye lolote litakalofanywa Zanzibar asema ‘hewala bwana....’, ndio maana akasema nitawaleteeni kijana mzuri", alisema Maalim Seif.

Akizitaja sababu zilizopelekea yeye kutohudhuria sherehe za Muungano zilizofanyika Uwanja wa Taifa hapa Jijini Aprili 26, mwaka huu, Maalim Seif alisema kuwa yeye kama kiongozi wa wananchi wa Zanzibar isingekuwa vyema kwake kuhudhuria sherehe hizo wakati wanachi Zanzibar wanapigwa na kuteswa na polisi wa muungano. 

"Siwezi kukaa meza moja na mtesaji wakati wananchi wanateswa", alisema Katibu Mkuu huyo wa CUF.

Akizungumzia mwafaka visiwani humo, Maalim Seif alisema kuwa shutuma zote zinazotolewa na CCM juu ya CUF kuhusu suala la utekelezaji wake ni uzushi na kwamba hazina msingi wowote kwani CUF imetekeleza kikamilifu vipengele vyote vya mwafaka kama vile kumtambua Rais wa Zanzibar pamoja na serikali yake na pia wawakilishi wa CUF kuhudhuria katika Baraza la Wawakilishi. Isipokuwa wanaokwamisha utekelezaji wa mwafaka huo ni CCM.

Aidha, Maalim Seif aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi wakati wa uandikishaji na hatimaye kuzitumia vyema kura zao ili kuleta mabadiliko ya kisiasa Visiwani humo. Alisema Zanzibar inahitaji mabadiliko na uongozi utakaoondoa aina zote za mtengano katika jamii. 

Ili kufanikisha hilo, Maalim Seif alisema kuwa "Rais wa CUF" atakayeshika madaraka ataunda serikali ya Umoja wa Kitaifa ili kila mtu ajihisi ni serikali yake.

Mkutano huo pia ulihudhuriwa na viongozi wengine wa wa CUF wakiwemo Makamu Mwenyekiti Shaaban Mloo, Katibu wa Kuratibu Mwafaka kwa upande wa CUF,Bw. Abdulraham Muhammad Dedes.
 

Juu
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI
KERO katika Elimu ziondolewe haraka

Chuo Kikuu Dar wafanya mitihani katika Bwalo la chakula

Udini wa CCM utaisambaratisha nchi -Tambwe

‘Kutoweka’ kanda ya Kakobe: CCM yatuhumiwa

Maalim Seif awaambia Wazanzibari: Wenye mamlaka ya kumuweka mtu Ikulu ni wananchi

Mkapa afurahia maendeleo Pwani

Wapinzani wajiimarisha Moro

‘Zawadi’ ya Uchaguzi yatishia kusambaratisha taasisi ya Kiislam Tanga

Serikali yakemea mwanamke kudhalilishwa

Ushauri Nasaha
Umuhimu wa kushirikiana na majirani katika malezi ya watoto

MAKALA
Afande Mahita, wananchi hatutaki Dola ya kipolisi

Makala
CCM hawawezi kuondoa umasikini, ndio tegemeo lao

Kalamu ya Mwandishi
Makubaliano kwa vitendo Z'bar

MAKALA
CCM na sera za maendeleo (5)

Makala
Wanawake na maendeleo: Je ni wimbo wa kuchaguliwa?

Makala
CCM inatawala badala ya kuongoza

Habari za Kimataifa

RIWAYA
Mapinduzi ya fikra -4

Lishe
Unachotakiwa kufanya kabla ya kuweka chakula kwenye jokofu

BARUA

MASHAIRI

MICHEZO

  • Raza kufungua mashindano ya Wavu Zanzibar
  • Real Madrid yaota Ubingwa  leo
  • Kajumulo asema Yanga timu ya Wananchi

  •  


       Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
    Au
    Andika barua  kwa: nasaha1420@yahoo.com

    Ukurasa wa mwanzo
    Islam Tanzania
    Matoleo yaliyopita