|
Na. 049 Jumatano Mei 24 - 30, 2000 |
|
|
|
|
|
Unachotakiwa kufanya kabla ya kuweka chakula kwenye jokofu
CHAMOS, H.J Kila kitu kina mipangilio yake. Na kwa kila chenye mipangilio ni muhali kukosa matayarisho. Ili uwezo kupata mafanikio unayotarajia, huna budi kujiandaa vyema. Iwapo unahitaji kuhifadhi vyakula vyako kwenye jokofu, ufuatao ni muhtasari wa matayarisho. Unapokuwa tayari na vyakula mezani, ndio kwanza unataka kupanga kwenye jokofu ni vyema ukazingatia yafuatayo. Kwanza gawanya vyakula katika makundi tofauti. Bila shaka vyakula vyako vitakuwa si vya aina moja bali ni aina mbalimbali. Kila chakula kina ladha na harufu totauti. Kuna vyenye mafuta na visivyokuwa navyo. Hivyo basi ni lazima vyakula vyako uvitenganishe sawasawa. Mathalani, nyama, samaki, dagaa kuwa kundi moja. Mboga za majani na matunda, maziwa, maji ya matunda na vyakula vya makopo. Kundi la mwisho ni viungo vibichi kama vile vitunguu saumu, tangawizi n.k. Kuna vyakula vinaweza kufyonza harufu ya vyakula vingine mfano maziwa iwapo vitachanganywa. Ndio maana tunasisitiza kutenganisha. Ama baada ya kutenganisha, vyakula visafishwe kulingana na makundi yake. Jaribu kutotumia maji mara mbili. Mfano maji yaliyooshea matunda kuoshea mboga za majani, si katika mpangilio unaofaa. Kila kundi lijitegemee. Vyakula visafishwe kwa uangalifu mkubwa kwa kuzingatia kuwa, baada ya kuhifadhiwa hakitaoshwa tena, bali kupikwa au kuliwa moja kwa moja. Baada ya kusafisha vyakula viweke katika kiasi kinachowekeka. Mfano huwezi kuweka mguu mzima wa ng’ombe bila kukatakata. Zoezi hili lifanyike bila kuchanganya makundi yaliyokwisha tengwa. Utakapo katakata vizuri, itasaidia kuhifadhi vyakula vingi zaidi kuliko kuweka shagalabagala katika ukubwa au udogo usio na uwiano. Kwa vyakula ambavyo vitapikwa tena, vikatwekatwe kwa saizi itakayotumika wakati wa mapishi. Kama nilivyowahi kueleza huko nyuma, vyakula vilivyotolewa kwenye jokofu huharibika haraka. Hivyo basi ni vizuri kuandaa kabisa ili chakula kisibaki nje muda mrefu kabla ya kupikwa. Kwa mboga za majani itategemea na aina. Mathalani mchicha ni bora ‘uchambuliwe’ kwanza na kuwekwa kwa kiasi unachotaka (kumbuka kukatakata mchicha au mboga za majani baada ya kuosha). Ama mboga mboga zingine kama bamia, karoti, njegere, biringanya n.k. vinaweza kuwekwa bila ya kukatakata. Kumbuka kuwa kukatakata kuna kifanya chakula kiweze kupoteza virutubisho haraka zaidi kuliko vile ambavyo havijakatwa. Na kuzuia kwake kunahitaji uangalifu mkubwa. Kwa sababu hiyo ni vyema kukatakata vyakula vile tu ambavyo vinaulazima huo na si kila chakula. Hatua inayofuata ni kufungasha (packing). Vyakula ambavyo tayari vimekatwa katwa na vipo katika makundi vipakiwe kwenye vyombo, mifuko au vifaa vyovyote vilivyotayarishwa kayari kwa kazi hiyo. Iwapo unahitaji chakula chako kidumu muda mrefu zaidi, ndivyo itakavyokuhitaji ufungashe vizuri zaidi. Vyakula vinaweza kudumu hata miezi 6-12 kulingana na uhifadhi wako. Fungasha kulingana na makundi ambayo tayari umeyapanga. Vifurushi viwe katika ujazo ambao utatumika kwa chakula hicho kitakapohitajika. Kuna aina nyingi za vifaa vitumikavyo kufungashia vyakula. Cha msingi ni kuwa kifaa hicho kisiweze kutoboka na kioneshe chakula kilichopo ndani yake. Hii itakurahisishia kuona unachohitaji badala ya kupekuapekua. Harufu za vyakula zinaweza kusafiri kutoka chakula kimoja hadi kingine. Ili kuzuia hili, fungasha kwa uangalifu ili kuzuia harufu kusambaa. Vifuko vya kuwekea vyakula ni vizuri iwapo vitakuwa vya rangi tofauti tofauti. Hii husaidia kutofautisha vyakula kwa urahisi. Mara baada ya kufungasha, panga
vyakula vyako vizuri kulingana na muda wa kuhifadhi. Vitakavyo tumiwa muda
mfupi vikae chini kwenye baridi ya kati. Iwapo jokofu lako lina milango
miwili pamoja na vichumba viwili, tumia chumba kimoja kwa ajili ya vyakula
vitavyotumika karibuni na kingine kwa ajili ya vyakula vitavyotumika baadaye
sana. Mlango wa chumba chenye vyakula vya muda mrefu, usifunguliwe mara
kwa mara. Kumbuka kupanga kulingana na makundi uliyotenganisha.
|
YALIYOMO
TAHARIRI
Chuo Kikuu Dar wafanya mitihani katika Bwalo la chakula Udini wa CCM utaisambaratisha nchi -Tambwe ‘Kutoweka’ kanda ya Kakobe: CCM yatuhumiwa Maalim Seif awaambia Wazanzibari: Wenye mamlaka ya kumuweka mtu Ikulu ni wananchi Mkapa afurahia maendeleo Pwani ‘Zawadi’ ya Uchaguzi yatishia kusambaratisha taasisi ya Kiislam Tanga Serikali yakemea mwanamke kudhalilishwa Ushauri Nasaha
MAKALA
Makala
Kalamu ya Mwandishi
MAKALA
Makala
Makala
RIWAYA
Lishe
|
|
|
|
|