NASAHA
Na. 049 Jumatano Mei 24 - 30, 2000
Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita
Tahariri
S.L.P. 72045, Simu: 0811 - 600145, Dar es Salaam

KERO katika Elimu ziondolewe haraka


KERO mbali mbali zinazoikabili sekta ya elimu nchini zinahitaji juhudi za makusudi za Serikali na wananchi ili kuziondoa vinginevyo taifa litaangamia.
Taarifa za hivi karibuni kutoka hapa Jijini na mkoa wa Pwani zinaashiria kuongezeka kwa kero katika sekta hiyo muhimu katika jamii, licha ya hatua zinazodaiwa kuchukuliwa na serikali na wananchi katika ujumla wao.

Imeripotiwa wiki hii kwamba elimu katika mkoa wa Pwani ni duni ambapo shule kadhaa za msingi hazijawahi kutoa wanafunzi wanaofaulu kwenda sekondari za serikali kwa karibu miaka 20 tangu zilipoanzishwa. 

Aidha, imeelezwa kuwa matokeo hayo yanachangiwa na mazingira duni watoto wanaposomea, walimu kukosa mishahara yao kwa zaidi ya miezi sita, na walimu hao kuishi katika nyumba ambazo hazina mwanga.

Kama kwamba hayo hayatoshi, tunaambiwa kwamba hivi sasa kuna walimu zaidi ya 1500 ambao hawajalipwa mishahara yao tangu waajiriwe mwaka jana.

Sambamba na hali hiyo kero sasa zinapanda kutoka shule za msingi na sekondari na kufika katika vyuo vikuu.

Wiki hii baadhi ya wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, sehemu ya Mlimani, wamekuwa wakifanyia mitihani yao ya kumaliza mwaka na wengine kuhitimu shahada za katika bwalo la chakula. Hali hii inatokana na hatua ya Serikali kuongoza idadi ya wanafunzi chuoni hapo kila mwaka, wakati miundo mbinu haiongezeki kwa idadi sawa na ongezeko la wanafunzi.

Mpaka sasa baadhi ya wanafunzi wa Kitivo cha Uhandisi wamesimamishwa masomo baada ya ugomvi kati yao na wanafunzi wenzao wa Kitivo cha Sheria. Inadaiwa kuwa sakata hilo linatokana na hatua ya wanafunzi wa Kitivo cha Sheria kutumia madarasa ya Kitivo cha Uhandisi.

Tukiutazama mwendo huu kwa makini na bila ya mapenzi ya vyama vya siasa, tutaona kwamba taifa letu linaelekea pabaya, ambapo kero katika sekta ya elimu zinaongezeka kila kukicha.

Kwa hiyo, tunaiomba serikali na wananchi kwa ujumla kuziondoa kero mbali mbali katika elimu.


Juu
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI
KERO katika Elimu ziondolewe haraka

Chuo Kikuu Dar wafanya mitihani katika Bwalo la chakula

Udini wa CCM utaisambaratisha nchi -Tambwe

‘Kutoweka’ kanda ya Kakobe: CCM yatuhumiwa

Maalim Seif awaambia Wazanzibari: Wenye mamlaka ya kumuweka mtu Ikulu ni wananchi

Mkapa afurahia maendeleo Pwani

Wapinzani wajiimarisha Moro

‘Zawadi’ ya Uchaguzi yatishia kusambaratisha taasisi ya Kiislam Tanga

Serikali yakemea mwanamke kudhalilishwa

Ushauri Nasaha
Umuhimu wa kushirikiana na majirani katika malezi ya watoto

MAKALA
Afande Mahita, wananchi hatutaki Dola ya kipolisi

Makala
CCM hawawezi kuondoa umasikini, ndio tegemeo lao

Kalamu ya Mwandishi
Makubaliano kwa vitendo Z'bar

MAKALA
CCM na sera za maendeleo (5)

Makala
Wanawake na maendeleo: Je ni wimbo wa kuchaguliwa?

Makala
CCM inatawala badala ya kuongoza

Habari za Kimataifa

RIWAYA
Mapinduzi ya fikra -4

Lishe
Unachotakiwa kufanya kabla ya kuweka chakula kwenye jokofu

BARUA

MASHAIRI

MICHEZO

  • Raza kufungua mashindano ya Wavu Zanzibar
  • Real Madrid yaota Ubingwa  leo
  • Kajumulo asema Yanga timu ya Wananchi

  •    Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
    Au
    Andika barua  kwa: nasaha1420@yahoo.com

    Ukurasa wa mwanzo
    Islam Tanzania
    Matoleo yaliyopita