|
Na. 049 Jumatano Mei 24 - 30, 2000 |
|
|
|
|
|
Tujihadhari na propaganda za CCM Ndugu Mhariri, Naomba unipatie nafasi katika gazeti lako tukufu ili nitoe yangu machache kuhusiana na hali halisi ya kisiasa na kijamii hapa nchini, hasa katika mwaka huu wa uchaguzi. Wakati tukikaribia mwezi Oktoba ambao ni wa uchaguzi inatupasa kuwa makini dhidi ya propaganda zinazoendelea za chama tawala (CCM) za kutaka kutuhamisha katika mada yetu yakuking’oa madarakani chama tawala baada ya kuona kuna kila dalili za wimbi la kisiasa linaloashiria mabadiliko. Waathirika wakubwa wa utawala mbaya wa CCM ni walala hoi pamoja na jamii ya Kiislamu nchini tuna paswa kuwa makini na ngangali hasa katika kipindi hiki ambacho kampeni zisizo rasmi zimekwishaanza. Kitu cha muhimu hivi sasa ni kujitahidi kupiga kampeni kila mahali ilituweze kuwa na kura ya pamoja na kwa kutumia wingi wetu ‘Inshaallah’ udhalimu utatokomea, ambao una kila mikakati ya kututawala na kutufanya wajinga milele. Mwaka huu ni muhimu kufanya kweli (kuitoa CCM), kwani endapo madhalimu hawa watarudi madarakani katika kipindi kingine (2000-2005) ambacho ndicho kitakuwa cha mwisho kwa Rais wa sasa (Mkapa),itakuwa ni hatari zaidi hasa kwetu sisi Waislamu na walalahoi wengine (Wamachinga) ambao tumekwisha onesha upinzani wa dhahiri kwa CCM, hapo itakuwa ni kama ‘Fungulia Mbwa’ hakuna kutojali maana hatorudi tena kutuomba kura. Tujiulize endapo sasa (1995-2000) tumenyanyasika kiasi hiki ambapo anajua bado anahitaji kura zetu kuwa Ikulu. Je hapo atakapokuwa anamalizia itakuwaje? Kwa hiyo bado hatujachelewa tujizatiti na kuwapa nguvu WANA MAGEUZI WA KWELI ili kuondokana na madhila haya yaliyotusibu kwa takriban miaka 40 sasa. Tuige mifano ya Senegal na Taiwan kuleta mabadiliko baada ya kuchoshwa na watawala hawa wanaopenda kutomilikiwa na wananchi zaidi ya wao kuwatumikia wananchi, hukuwakieka maslahi yao mbele zaidi ya waajiri wao (wananchi) na kutokuwa waadilifu katika kutoa haki baina ya raia kwa misingi yadini zao na jamii zao. Nduguzangu’wakati ni huu na inawezekana’. Hassan Amir Kunuga,
Sekondari ya Umbwe yaanguka Ndugu Mhariri, Maendeleo ya kitaaluma ya shule yetu ya Umbwe yamedidimia kiasi cha kutisha. Mambo yalianza kwenda kombo baada ya kumpata Mkuu wa Shule mpya mwaka 1996. Wakati ule shule ilikuwa ya 1. Kitaifa. Kilichofuatia ni kuanza kuhama ovyo kwa waalimu ambao ndiyo waliokuwa msingi wa mafanikio yetu. Hadi mwaka jana 1999 mtihani wa kidato cha nne ambao majibu yake yametoka Aprili 2000 shule yetu sasa imeporomoka hali hushika nafasi ya 151! Sambamba na uhamisho wa waalimu pia Mkuu huyu anatabia ya kuwafuatafuata wanafunzi wenye tabia za kuuliza maswali na hata kuwafukuza shule. TunaombaWizara ifuatilie hali hii. Wanafunzi
Hongera Lipumba, tuko nyuma yako Ndugu Mhariri, Wananchi tumefarijika kutokana na kitendo cha Profesa Lipumba cha kuchukua fomu ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tunaahidi kukuunga mkono kuyatekeleza yale unayotueleza wakati tukielekea kwenye uchaguzi mkuu na tunakuhakikishia kuwa tutakupigia kura ili uwe rais wa nchi hii. Tutajiandikisha kwa wingi, tutapiga kura na tutazilinda kura zetu. Hatutakubali kamwe kura zetu ziibwe na wale wenye uchu wa madaraka ambao wako tayari kuipiga kumbo demokrasia ilimuradi tu wabakie madarakani. Miaka 40 waliokaa madarakani ambapo taifa wamelididimiza kiuchumi bado haijawatosha, wanataka miaka mingine zaidi. Tunasema, tena kwa kinywa kipana, kuwa safari hii kama watatuletea yale mambo waliyoyafanya mwaka 95 basi wajue wazi kuwa hatutakubali na itakuwa ‘jino kwa jino’. Tumekuelewa vyema pale ulipotuambia kuwa haki haipatikani kwenye sahani bali hupiganiwa, nasi tunakuahidi kuwa tupo "ngangali". Vijana wa CUF,
Wafanyakazi msishangae Ndugu Mhariri, Wako baadhi ya wafanyakazi wako mstari wa mbele kudai etiutawalawa CCM siyo mbaya kwani CCMndiyo iliyawalea. Sasa butwaa ya nini kama mkuu wenu kasema haongezi mshahara hadi kuwepo ufanisi kazini? Kama hatuwezi kusimama na kuwakataa viongozi hawa Oktoba 2000 basi tujue hali yetu itabakia hivi hivi tu. TFTU lazima isimame imara bila woga kuwa kama kiongozi hafai aambiwe ukweli, bwana wewe hutufai. Chanzo cha umaskini, ujinga na dhuluma ni woga haya yameshabainishwa na Amir Mbukuzi, Kakobe na Pengo. Bw.Mpangala valia njuga ujinga ili ulazimike kuwatetea wafanyakazi. Lioche A. Lioche,
|
YALIYOMO
TAHARIRI
Chuo Kikuu Dar wafanya mitihani katika Bwalo la chakula Udini wa CCM utaisambaratisha nchi -Tambwe ‘Kutoweka’ kanda ya Kakobe: CCM yatuhumiwa Maalim Seif awaambia Wazanzibari: Wenye mamlaka ya kumuweka mtu Ikulu ni wananchi Mkapa afurahia maendeleo Pwani ‘Zawadi’ ya Uchaguzi yatishia kusambaratisha taasisi ya Kiislam Tanga Serikali yakemea mwanamke kudhalilishwa Ushauri Nasaha
MAKALA
Makala
Kalamu ya Mwandishi
MAKALA
Makala
Makala
RIWAYA
Lishe
|
|
|
|
|