|
|
|
Kama mkitoa sadaka kwa dhahiri ni vizuri; na kama mkitoa kwa siri na kuwapa mafakiri, basi huo ni ubora zaidi kwenu; na atakuondoleeni maovu yenu na Allah anazo habari za mnayoyatenda. Aya hii inazungumzia suala la utoaji ambao siyo ule wa lazima (yaani ni utoaji wa hiari au sunna - sadaka). Utoaji huu unaelezwa hapa kuwa unaweza kufanywa kwa kufuata mojawapo wa njia mbili zilizotajwa - ama kutoa kwa dhahiri au kutoa kwa siri. Hata hivyo kutoa kwa siri kumesifiwa kuwa ni bora zaidi kuliko kule kwa dhahiri. Tunachojifunza katika aya hii na ambacho kimethibitika katika mwenendo wa Mtume (s.a.w.) ni kuwa ni vyema zaidi kwa Waislamu kuzifanya ibada za sunna kwa njia ya siri na zile za fardhi zifanywe kwa dhahiri. Ziko tofauti ndogo ndogo za suala hili kwa kutegemea kama muhusika ni mwanamke au mwanamme na wakati mwengine baadhi ya ibada zenyewe. Mfano wa wazi ni ule wa sala ambapo kwa mwanamke kusali fardhi yake nyumbani kwa siri ni bora kuliko kwa dhahiri. Ama kwa sunna ya sala ya Idi inatakiwa ifanywe kwa dhahiri. Ukitoa hali hizo; ubora wa kufanya mambo yanayohusiana na ibada maalumu za sunna kwa siri ungali juu na unaosisitizwa na Uislamu. Hiyo ni kinyume cha ibada maalumu za fardhi ambazo maumbile yake yanahimizwa yale ya wazi pasipo na uficho. Faida ya jambo hili iko wazi kama ilivyo kwa maagizo mengine ya Allah kwa wanadamu. Ibada za hiari zimelengwa kusaidia kuziba dosari zinazojitokeza kwenye ibada za fardhi pamoja na kumjengea mja ukaribu wake na Mola wake. Kwa sababu hizo kila mja anapojificha na kutenda ndipo anapojisogeza karibu zaidi; tofauti na anapofanya dhahiri ambapo anaweza kupata hisia za kujionyesha kwa wengine (kuwa na riya). Jambo hili iwapo litatokea linamfanya mtu kuwa hana kitu. Ibada maalum za fardhi mbali na kulengwa kufikisha lengo moja moja au mengi kwa kila moja; vile vile zimelengwa kutoa picha ya utambuzi na utambulisho wa Allah katika kutawala maisha ya wanadamu kila siku. Ibada hizi zinapotekelezwa kwa jumla na hadharani zinatoa picha ya namna gani jamii hiyo inavyoukubali ufalme wa Allah. Chukua mfano mmoja wakati watu wanapoacha shughuli zao kwa wakati mmoja na kuelekea misikitini mara baada ya kusikia adhana. AYA YA 272 Si juu yako kuwaongoa; lakini Allah humuongoa amtakaye. Na mali yoyote mtakayotoa ni kwa (faida) ya nafsi zenu. Wala msitoe ila kwa kutafuta radhi za Allah. Na mali yoyote mtakayotoa mtawaishiwa kamili wala hamtadhulumiwa. Aya hii pamoja na mambo mengine imekuja kufuta wasiwasi waliokuwa hao Waislamu kuhusiana na kuwapa mali zao kwa njia ya msaada (au sadaka) watu ambao walikuwa hawajakubali kuamini licha ya kuwa walikuwa tayari wameshawafikishwa ujumbe wa Uislamu. Waislamu hao walikuwa na pupa na hamu kubwa ya kuona watu hao wanasilimu ndipo na wao wawape misaada yao. Hapa Allah anawaambia kuwa si jukumu la Mtume (s.a.w.) wala Waislamu kuwaongoa wale ambao walikuwa bado hawajawa tayari kuukubali Uislamu. Wajibu wao ambao wataulizwa ni kufikisha ujumbe kama unavyotaka. Pamekuwepo na masuala mengi kwenye aya kama hizi ambazo Allah husema kuwa "anamuongoa au anamuongoza amtakaye" na "humpoteza au kumwacha kupotea amtakaye" Baadhi ya watu hususan Waislamu - maamuma wamezifanya aya hizi kama hirizi zao za kuwazuilia kuulizwa masuala au kutakiwa wafanye mema na wakatazike na mkaovu. Mara nyingi hudai kuwa wao bado Allah hajawafikisha kutenda mema na kuwacha maovu na kuwa wakati ukifika basi mambo hayatakuja yenyewe bila ya kuhimizwa. Suala hili tumekuwa tukilitolea maelezo katika sehemu mbali mbali za makala hizi. Hata hivyo ilivyokuwa Allah Mwenyewe tayari amelifafanua suala hili ni vyema tukanukuu baadhi ya ufafanuzi huo kwa faida ya wasomaji wetu. Aya mbili zinazoelezea vipi Allah humuongoza amtakaye na vipi humuachia apotoke yule aliyeamua kupotoka ni: Na atakayemuasi Mtume baada ya kumdhihirikia uwongofu na akafuata njia isiyokuwa ya Waislamu, tutamgeuza alikogeukia mwenyewe na tutamwingiza katika Jahannam; hapo ni pahali pabaya kabisa pa mtu kurudia. (4:115). Aya nyingine inasema: Amekupeni sharia ya dini ile ile aliyomuusia Nuhu na tuliyokufunulia wewe na tuliyowausia Ibrahim na Musa na Isa kwamba simamisheni dini wala msifarikiane kwayo; ni ngumu kwa wenye kushirikisha (dini hii) unayowaitia; Allah humchagua kwake amtakaye na humuongoza kwake aelekeaye (kwake). (42:13). Kinachojitokeza katika aya hizi ni kuwa kwanza mtu mwenyewe hufanya uchaguzi wa ama wema au ubaya na ndipo Allah humuwafikisha katika uchaguzi wake huo. Katika aya ya kwanza mbali na Allah kutoa nafasi sawa kwa wanadamu wote ya kuongozwa kwa njia ya ilhamu kwa kueleweshwa mema na maovu, (Na naapa kwa nafsi (roho) na Aliyeitengeneza; kisha akaifahamisha ouvu wake na wema kwake), wanadamu wote wamepata fursa ya kuletewa Mitume ambao wamekuja na vitabu ili kuwafahamisha uongofu pamoja na kuwakumbusha yale ambayo tayari wameshafahamishwa kwa njia ya ilhamu. Iwapo binadamu ameshafahamishwa wema na uovu na akaletewa Mtume akiwa na kitabu kumkumbusha hivyo huyu anaweza kusema kuwa amepotoshwa na Allah? au mtu huyu ana haki ya kusema kuwa Allah hakutaka kumuongoza? Aya ya pili inaelezea uongofu wa Allah na hamna anavyoongoka mtu. Kama ilivyo kwa aya iliyotangulia, Allah anamuwafikisha kuongoka yule ambaye ameletewa uongofu na akaupokea na kisha akaufuata. Na hii ndiyo maana ya kumuongoza yule "aliyeelekea kwake." Ama kwa upande wa nani awe Mtume na nani asiwe hilo Allah hulifanya mwenyewe hata kabla ya mtu anayehusika kuzaliwa. Mitume wote huzaliwa Mitume ingawaje wenyewe hawajifahamu hadi wanapodhihirishiwa na Allah wakati unapofika. Mitume wengi pamoja na kuwa na sifa tofauti na watu wa jamii zao walijifahamu kuwa wao ni Mitume walipotimia miaka 40 na kutangaziwa hivyo na Allah Mwenyewe au Malaika Jabril (a.s.) Kwa kuwa aya tunayoendelea nayo (272) imo katika mtiririko wa kutoa inakamilika kwa kuelezea mambo mawili ya msingi: -mtu anapotoa mali yake huwa ni kwa manufaa yake binafsi na siyo anapoteza bali atarudishiwa kwa malipo yaliyo bora zaidi kuliko hicho kidogo alichokitoa. - Mtu anapotoa anatakiwa afanye hivyo kwa lengo moja tu ambalo ni kumridhisha
Allah Ambaye ndiye aliyetoa agizo hilo. Kutoa kwa matarajio mengine yasiyo
ya kupata radhi za Allah kutampelekea mtoaji kuwemo hasarani.
|
YALIYOMO
Tahariri
Urambo wamlilia Profesa Lipumba
Sheikh aridhia Waislamu
kubatizwa
Uongozi Masjid Qadiria waitwa Polisi kuhojiwa Wakazi wa Mbagala Msalabani kuishitaki Tume ya Jiji Akhera ipo, makafiri ni wakadhibishaji
Mdahalo kati ya Waislamu na
Wakristo ni mgumu
Aina ya maudhi yaliyoharamishwa juu ya Muislamu PAROLE: Rais kasusa
au hana ubavu?
Serikali ikithamini kilimo
Umuhimu wa Elimu ya Awali kwa watoto
wadogo - 3
Madrasa Arrijalu Muswallin Damba Ijue Madrasat Fauzia - Kibondo Waislamu Kondoa waanza
kupokea misaada ya ujenzi wa Msikiti, Madrasa
Waislamu Dodoma wasali sala ya Ghaib kwa marehemu Kilima na mkewe Songea kujenga shule ya sekondari Wanafunzi wa Bihawana Dodoma wamshukuru Alhaj Ismail Dawood Mashindano ya kusoma Qur’an yafanyika Kondoa Waislamu wautazame upya mfumo wao wa elimu Ujenzi wa Chuo cha Kiislamu Shamsiya Bereko wakwama Kesi ya kushambulia kituo yaahirishwa tena Polisi waondolewa kimya kimya Mwembechai Msikiti wa Kiwanja cha Ndege wapania kujenga shule Sayansi na Teknolojia
Chakula na lishe
|