AN-NUUR 
Na.177 Shaaban  1419, Novemba 27 - Desemba 3, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Waislamu Dodoma wasali sala ya Ghaib kwa marehemu Kilima na mkewe
 

MAMIA ya Waislamu walikusanyika Masjid Qubaa kusali sala ya ghaib kwa marehemu Sheikh Abbas S. Kilima na mkewe Bi. Rukia Fundi waliopatwa na ajali ya gari Chalinze mkoani Pwani mwanzoni mwa Novemba mwaka huu. 

Akitoa taarifa fupi, baada ya sala hiyo iliyosaliwa baada ya sala ya Ijumaa, Imam wa Masjid Quba, Sheikh Abdallah Ally bin Ahmed alimueleza marehemu alikuwa mtu shupavu, shujaa na mtetezi wa haki za Waislamu na mwenye kujituma kwa ajili ya Allah (s.w.). 

Sheikh Abdallah aliwaeleza waumini kuwa marehemu alipita mjini Dodoma akitokea Kondoa ambako alihudhuria mazishi ya binti yao Bi. Mwilwa ambaye pia alisaliwa sala ya ghaib ya marehemu huyo Novemba 6, mwaka huu. 

Sheikh Abdallah alimalizia kwa kuwaeleza waumini kuwa hili tukio ni zingatio kubwa kwa wale wamuogopao Allah (s.w.). 

Wakati huo huo, kikundi cha akina mama wa Kiislamu cha Bi. Khadija cha mjini hapa walipatwa na mshtuko mkubwa kufuatia kifo cha Sheikh Abbas na mkewe. 

Mwenyekiti wa kikundi hicho Bi. Mwanahamisi Abdallah alisema wanamfahamu marehemu pamoja na familia yake jinsi walivyokuwa mstari wa mbele katika kuusimamisha Uislamu. 

Bi. Mwanahamisi alisema Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu limeondokewa na kiongozi hodari, mvumilivu, jasiri na mwenye ghera katika kuuendeleza Uislamu na Waislamu. 

Aidha, Mwenyekiti huyo Bi. Mwanahamisi ameuomba uongozi wa Baraza Kuu katika kipindi hiki cha majonzi wakae waombe msaada kwa Allah (s.w.) wapate kiongozi atakayeweza kufuata nyao za marehemu, na kuyafanyia kazi yote aliyoyaacha. 


Songea kujenga shule ya sekondari

Waislamu wa mkoa wa Ruvuma wameamua kufyatua matofali kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari ya Kiislamu inayotarajiwa kujengwa katika eneo la Msamala nje kidogo ya mji wa Songea. 

Uamuzi huo umefikiwa katika mkutano mkuu wa mwaka wa Taasisi ya Ruvuma Muslim Education Development Trust Fund (RUMEDETF) uliofanyika katika majengo ya muda ya sekondari ya Kiislamu ya Msamala. 

Wajumbe kwa kauli moja waliamua ufyatuzi wa matofali hayo uanze mara moja na kwa kuanzia imeamliwa zifyatuliwe tofali laki moja na zichomwe kabla ya mvua hazijaanza. 

Taasisi ya RUMEDETF ndiyo inayomiliki sekondari ya Msamala Muslim, ambayo kwa sasa ina madarasa mawili yaani kidato cha kwanza na cha pili na hapo mwakani itakuwa na darasa la kidato cha tatu, shule itakapokamilika itakuwa na wanafunzi wa kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita. 

Akitoa taarifa ya mwaka ya Taasisi hiyo kwa wajumbe wa mkutano huo, Mwenyekiti wa RUMEDETF, Bw. Ismail Gawaza aliwaambia wajumbe kuwa Kamati Kuu ya taasisi hiyo inafikiria kubadilisha shule hiyo na kuwa Seminari ya Kiislamu badala ya sasa ambapo ni sekondari ya kawaida tu. 

Aliendelea kuwaeleza wajumbe kuwa shule ina upungufu mkubwa wa wanafunzi na wamewahimiza Waislamu wote kuwapeleka watoto wao katika shule hiyo ambayo kwa sasa inajitosheleza kwa walimu ambao ni wa taaluma kwa masomo yote. 

Katika kuhakikisha ujenzi wa shule hiyo unakwenda kama ulivyokusudiwa, wajumbe waliunda kamati ya watu watano ambao kazi yao itakuwa kukusanya fedha za ujenzi kwa Waislamu mbalimbali wa mkoa wa Ruvuma na nje ya mkoa. 

Kamati hiyo itakuwa chini ya Mwenyekiti Bw. Ismail Gawaza, Bw. Hassan Msham Katubu, Bw. Idrisa Mbunda, Bw. Aman Chimgege na Sheikh Nahodha Mpaka watakuwa wajumbe wa kamati hiyo. 

Kamati hiyo imepewa jukumu la kuwaelimisha Waislamu umuhimu wa mkoa kuwa na shule ya sekondari ya Kiislamu kwani shule hiyo ya Msamala itakuwa ya kwanza kuanzishwa, hivyo ni vizuri kila Muislamu kuchangia ujenzi wa shule hiyo. 

Wakati huo huo, Katibu aliyevuliwa madaraka akifuatana na walimu Nchimbi na Haule waliamua kuvamia shule hiyo na kutaka kufanya fujo shuleni hapo. 

Katibu huyo Bw. Faraji Hasara na wenzake walikwenda shuleni hapo na kudai kuwa wamekuja na mambo matatu, la kwanza kugawa barua kwa wanafunzi ili kuzipeleka kwa wazazi wao kuwa shule inahamishwa na kupelekwa katika maeneo yake na kung’oa vibao kupeleka huko na kuwahamisha wanafunzi. 


Wanafunzi wa Bihawana Dodoma wamshukuru Alhaj Ismail Dawood
 

UMOJA wa vijana wa Kiislamu tawi la shule ya sekondari ya Bihawana umetoa shukrani kwa Alhaj Ismail Dawood na familia yake kwa kujengewa kibla cha Msikiti wao. 

Ustaadh Issa Athman ambaye ni mwanafunzi wa shule hiyo, pia ni Mwenyekiti wa Vijana wa Kiislamu, alitoa shukrani hizo alipotembelewa na mwandishi wa gazeti hili hivi karibuni ambaye alifika shuleni kutaka kujua hali ya maendeleo ya Msikiti huo ambao una ukosefu wa misala na chumba cha kusalia kwa wanafunzi wa kike. 

Ustadh Issa Athmani alisema Msikiti wa wanafunzi wa Bihawana bado una ukosefu wa misala, majamvi na chumba cha kusalia kwa wanafunzi wa kike. 
 
 

Juu 
 

YALIYOMO 
 

Tahariri
Hii siyo Demokrasia ni fedheha

Urambo wamlilia Profesa Lipumba
Na Mwandishi Wetu

Sheikh aridhia Waislamu kubatizwa
Na Rajab Rajab, Morogoro

Zanaki kupiga marufuku Hijab?

Uongozi Masjid Qadiria waitwa Polisi kuhojiwa

Wakazi wa Mbagala Msalabani kuishitaki Tume ya Jiji

Wasemavyo wanaharakati

Akhera ipo, makafiri ni wakadhibishaji
Na Abubakar Marwilo

Mdahalo kati ya Waislamu na Wakristo ni mgumu
Na Elia Batendi

Aina ya maudhi yaliyoharamishwa juu ya Muislamu

PAROLE:   Rais kasusa au hana ubavu?
Na Bisura Waziri Nyello

Serikali ikithamini kilimo
Na Abdallah Ahmad Seif

Umuhimu wa Elimu ya Awali kwa watoto wadogo - 3
Na Ustaadh Kupa Pazi Said

Madrasa Arrijalu Muswallin Damba

Ijue Madrasat Fauzia - Kibondo

Waislamu  Kondoa waanza kupokea misaada ya ujenzi wa Msikiti, Madrasa
Na Abu Zubeir, Dodoma

Waislamu Dodoma wasali sala ya Ghaib kwa marehemu Kilima na mkewe

Songea kujenga shule ya sekondari

Wanafunzi wa Bihawana Dodoma wamshukuru Alhaj Ismail Dawood

Mashindano ya kusoma Qur’an yafanyika Kondoa

Waislamu wautazame upya mfumo wao wa elimu

Ujenzi wa Chuo cha Kiislamu Shamsiya Bereko wakwama

Kesi ya kushambulia kituo yaahirishwa tena

Polisi waondolewa kimya kimya Mwembechai

Msikiti wa Kiwanja cha Ndege wapania kujenga shule

Sayansi na Teknolojia
[Kwenye Kompyuta RAM ni kitu gani?]

Mafundisho ya Quran

Masomo ya Dini ya Kiislamu 

Barua za Wasomaji 

Mashairi 

Chakula na lishe 
[Madini ya chuma]

 

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita