|
|
Aidha, sababu nyingine ya kuahirishwa kwa kesi hiyo hadi Desemba 14, mwaka huu, imedaiwa kuwa Mwendesha Mashitaka anayeendesha kesi hiyo, Bi. Maria Nzuki yuko likizo. Kesi hiyo ilitarajiwa tena kuanza kusikilizwa mahakama ya Kisutu, jijini Jumanne ya wiki hii (Novemba 24, 1998) ambapo mashahidi wa upande wa serikali walitarajiwa kutoa ushahidi wao. Hata hivyo, Mwendesha Mashitaka wa polisi aliyekuwepo siku hiyo badala ya Bi. Maria Nzuki, Bw. Kihenya wa Kihenya, aliiomba mahakama hiyo ipange tarehe nyingine ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo kwa madai ya kutokuwepo mashahidi wa serikali mahakamani hapo. Aidha, Bw. Kihenya alidai mahakamani hapo kuwa sababu nyingine ya kuomba kuahirishwa kwa kesi hiyo ni kuwa Mwendesha Mashitaka wa serikali anayeendesha kesi hiyo, Bi. Maria Nzuki amekwenda likizo na kwamba anatarajiwa kumaliza likizo yake hapo Desemba Mosi, mwaka huu. Watuhumiwa katika kesi hiyo ni pamoja na Uliza Rashid (37), Ally Majapa (42), Ally Athumani (40), Hamisi Swalehe (50), Ramadhani Hamisi (30) na Magezi Shaabani. Aidha, tofauti na hati ya awali ya shitaka lao (charge sheet), sasa inadaiwa katika hati nyingine mpya kuwa watuhumiwa watano ukimtoa Magezi Shaaban kuwa katika muhadhara wao huko Mwananyamala "A" Jijini Dar es Salaam, waliwafanyia fujo waumini wa dini nyingine na kuwazuia polisi kazi yao. Pia katika hati hiyo mpya inadaiwa kuwa baada ya watuhumiwa hao watano
kukamatwa na kuwekwa ndani katika kituo hicho cha polisi cha Msisiri, Magezi
aliwachochea wafuasi wake kukishambulia kwa mawe kituo hicho, kuharibu
mali za kituo hicho ambazo ni milango miwili, meza, mlingoti wa bendera,
nyaraka mbalimbali za kituo hicho, madirisha ya kituo na baiskeli, vyote
vikiwa na thamani ya shilingi milioni 5.
ASKARI polisi waliokuwa wakilinda doria katika maeneo ya Msikiti wa Mwembechai wa Jijini, uliokumbwa na vurugu mapema mwaka huu, hatimaye wameondolewa katika maeneo hayo baada ya wakazi na waumini wa Mwembechai kupigia kelele kuwepo kwao. Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi kwa muda wa wiki mbili umeweza kugundua kuwa askari hao, waliokuwa wakifikia hata kumi, wavaao sare kwa sasa hawapo maeneo hayo, ingawa kuna nyakati askari kanzu wenye radio za mawasiliano huwa wakipiga doria sehemu hizo kwa muda lakini hutoweka. Polisi hao waliokuwa doria tangu msikiti huo ulipokabidhiwa wadhamini wa Msikiti huo mapema mwezi wa Nne, walikuwa kero kwa waumini wa Kiislamu ambao kwa hofu ya kutiwa nguvuni hawakuwa wakiswali ndani ya Msikiti huo. Pia askari hao walikuwa wakichafua mazingira ya Msikiti huo na maeneo ya karibu kwa kujisaidia katika majengo mabovu na yasiyomalizika kujengwa, hali ambao ilikuwa ikitoa picha mbaya kwa jeshi hilo na serikali kwa ujumla. Kwa hivi sasa askari wenye nguo za kiraia wafikiao wawili au watatu, huonekana katika maeneo ya msikiti huo kati ya majira ya mchana hadi jioni na hatimaye hupotea kwa kile kinachoelezwa kuwa hali sasa ni shwari. Wakazi wa maeneo hayo ya Msikiti wameonyesha kufurahishwa na hatua ya askari hao kuondoka maeneo hayo, kutokana na madai ya kuondolewa bughudha iliyokuwa ikiletwa na askari hao, ambao saa nyingine walikuwa wakirundikana msikitini hapo wakiwa na silaha wakicheza karata au kupiga soga na wanawake wenye kufahamiana nao. Waumini wa msikiti huo, walishawahi kuiomba serikali iwaondoe askari hao msikitini hapo, haijulikani kama utekelezaji huu unatokana na maombi hayo au serikali imewatoa kutokana na kutokuwa uvunjwaji wa amani msikitini hapo kama ilivyokuwa ikihofiwa mwanzoni. Hivi sasa msikiti huo licha ya kukarabatiwa baada ya kuharibiwa na askari
wa FFU, bado waumini wamekuwa wakihudhuria kwa kiwango kidogo kiasi cha
swala kuwa na safu moja au mbili, kutokana na hofu ya kukamatwa.
WAUMINI wa Msikiti wa Kiwanja Ndege mjini hapa wameanza kujenga shule ya watoto wadogo, msingi na sekondari itakayogharimu jumla ya shilingi milioni 13,931,625 hadi kumalizika kwake. Ukiongea na AN-NUUR Msikitini hapo hivi karibuni, uongozi wa msikiti huo ulisema kuwa, awamu ya kwanza ya ujenzi huo imekwishaanza na kugharimu jumla ya shilingi milioni 4 hadi hivi sasa. Mwenyekiti wa Msikiti huo Bw. Shomari Mtogo ambaye ni Mhandisi kitaaluma alisema kwamba, hatua ya ujenzi iliyobaki itagharimu jumla ya shilingi milioni 9,659,125. Akigusia sababu ya Msikiti huo kuelekeza nguvu zake zote katika elimu, mjumbe wa Kamati ya Msikiti Sheikh Ramadhan Abdallah alisema kuwa huduma za jamii na hali ya kitaaluma na kiuchumi kwa Waislamu wa Kiwanja Ndege ni duni ukilinganisha na umri wake, hivyo kuzorotesha maendelo ya jumla ya waumini wa eneo hilo. Ili kuboresha maendeleo ya Waislamu wa hapa, alisema Sheikh Ramadhan, "tumeona ni bora kuanzisha miradi ya maendeleo hususan mradi wa elimu ambao utasaidia sana kututoa katika hali duni kiutendaji, na kutuweka katika hali bora zaidi." Naye Mweka hazina msaidizi wa Msikiti huo Maarufu "Msikiti wa Mungu Mmoja dini moja" Sheikh Rajab Mwinyimvua aliliambia gazeti hili kwamba, msikiti wa Kiwanja cha Ndege unasumbuliwa na ukata jambo ambalo linapelekea ujenzi wa shule kwenda pole pole mno. "Tunaomba Waislamu kote nchini kutusaidia pesa taslimu au vifaa vya ujenzi kama mabati, mbao, nondo na saruji ili vijana wetu waanze masomo mapema mwakani, kumecheleweshwa mno na kesi zaidi ya tano zilizotukalia kooni kwa zaidi ya miaka minne mfululizo, kufuatia kushambuliwa kwa mabomu na serikali ya CCM na wenzetu wawili kuwa mashahidi", anasema Sheikh Rajab ambaye ni mmoja wa viongozi wapya wa msikiti huo kufuatia uongozi wa uliokuwepo kung’olewa madarakani na kesi zote kumalizika kwa ushindi. Uongozi wa msikiti huo aidha una mpango wa kuendesha sensa katika eneo lake, itakayowasaidia kuweza kuinua hali za maisha za waumini wake katika nyanja zote za maisha yao ya kila siku. Msikiti wa Kiwanja cha Ndege ni moja ya misikiti kadhaa ya mjini hapa inayomilikiwa na kuongozwa na waumini wenyewe bila ya ushawishi wa aina yoyote kutoka taasisi yoyote ya kidini nchini. Bw. mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Wibonella alisema kwamba tarajio lao kubwa lilikuwa tumbaku, lakini kwa mwelekeo huu mpya watakuwa ni wenye kudhulumika. Amesema kwamba hakuna dalili zozote kwamba CCM na serikali yake zinachukua mwelekeo wa kuwatetea. Habari kutoka Urambo zimeeleza kwamba wananchi mbalimbali wamekuwa wakikutana na kutafakari ni vipi watapata ukombozi. Wengine wamekuwa wakijaribu kuwasiliana na uongozi wa CUF ili kumpata aliyekuwa mgombea Urais 1995 kupitia chama hicho Profesa Lipumba ili washauriane lipi la kufanya kwa siku za usoni. Juhudi za gazeti hili kuwasiliana na makampuni ya ununuzi wa tumbaku pamoja na serikali ya mkoa juu ya madai ya wananchi wa Urambo hazikuweza kufanikiwa. Wakati huo huo, Waislamu mjini Tabora wazee kwa vijana pamoja na Masheikh wao wamekutana ili kujadili mwelekeo wa umoja wao. Mkutano huo uliofanyika Jumanne Novemba 24, mwaka huu ukiwajumuisha watu maarufu kama Sheikh Hussein Ikunji, Sheikh Salala, Sheikh Issa Mzee na wengineo ulilenga kuondoa tofauti miongoni mwa Waislamu na kujenga umoja na mshikamano madhubuti kwa maslahi ya dini na dunia yao.
|
YALIYOMO
Tahariri
Urambo wamlilia Profesa Lipumba
Sheikh aridhia Waislamu
kubatizwa
Uongozi Masjid Qadiria waitwa Polisi kuhojiwa Wakazi wa Mbagala Msalabani kuishitaki Tume ya Jiji Akhera ipo, makafiri ni wakadhibishaji
Mdahalo kati ya Waislamu na
Wakristo ni mgumu
Aina ya maudhi yaliyoharamishwa juu ya Muislamu PAROLE: Rais kasusa
au hana ubavu?
Serikali ikithamini kilimo
Umuhimu wa Elimu ya Awali kwa watoto
wadogo - 3
Madrasa Arrijalu Muswallin Damba Ijue Madrasat Fauzia - Kibondo Waislamu Kondoa waanza
kupokea misaada ya ujenzi wa Msikiti, Madrasa
Waislamu Dodoma wasali sala ya Ghaib kwa marehemu Kilima na mkewe Songea kujenga shule ya sekondari Wanafunzi wa Bihawana Dodoma wamshukuru Alhaj Ismail Dawood Mashindano ya kusoma Qur’an yafanyika Kondoa Waislamu wautazame upya mfumo wao wa elimu Ujenzi wa Chuo cha Kiislamu Shamsiya Bereko wakwama Kesi ya kushambulia kituo yaahirishwa tena Polisi waondolewa kimya kimya Mwembechai Msikiti wa Kiwanja cha Ndege wapania kujenga shule Sayansi na Teknolojia
Chakula na lishe
|