|
|
| Historia:
Form IV
Uendeshaji wa Serikali ya Kiislamu wakati wa Makhalifa Ngome na kambi za jeshi zilijengwa katika sehemu mbali mbali, majengo ya ofisi na ya kukaa wafanyakazi mikoani na wilayani zilijengwa, Baitul mal yalijengwa majengo madhubuti, majela pia yalijengwa. Pamoja na majengo haya mabarabara na madaraja nayo yalijengwa. Visima na vituo kadhaa baina ya Makka na Madina vilijengwa. miji nayo ilianzishwa. Maarufu ni Basra, Kufa, Fustat na Mosal.40 14. Ulinzi na usalama Katika Dola ya Kiislamu wakati wa ukhalifa wa Makhalifa wanne ulinzi uliimarishwa kwa kiwango kikubwa. Wakati wa Mtume (s.a.w.) hakukua na kambi za kwa ajili ya Jeshi. Kila mtu alikuwa askari na vita ilipofika Waislamu walijitokeza wakapewa mafunzo na kwenda vitani. Ni kweli pia kuwa katika dola ya Kiislamu kila muumin ni askari wa Allah na wakati wowote anapotakiwa ni lazima ajitoe kupigania Dini ya Mwenyezi Mungu: "Enyi mlioamini Je! Nikujulisheni Biashara itakayokuokoeni na adhabu iumizayo? Muaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake na piganieni dini ya Mwenyezi Mungu kwa mali zenu na nafsi zenu... (61:10 - 11). Mwenyezi Mungu amenunua kwa Waislamu nafsi zao na mali zao ili nae awape pepo. Wanapigana katika njia ya Mwenyezi Mungu wanauwa na wanauwawa... (9:111). Ni dhahiri Muislamu ni askari wa Mwenyezi Mungu. Pamoja na hivi tangu wakati wa Khalifa wa pili Umar liliundwa jeshi kama yalivyo majeshi ya kileo. Khalifa ndie aliyekuwa mkuu wa majeshi aliteua kamanda wa jeshi na makamanda wa mikoa na wilaya. Ndani ya jeshi kulikuwa na vyeo mbali mbali. Kama vile "Arief" aliyekuwa mkuu wa askari kumi. Qaid au Lieutenent alikuwa mkuu wa askari mia moja. Wanawake walishiriki kwenye vita kazi zao zilikuwa kutoa huduma kuwahudumia majeruhi kwa kufunga vidonda, n.k. na mara chache walishiriki katika mapigano. Askari walikuwa wa farasi na wa miguu. Askari wa farasi walitumia silaha za mikuki, majambia. Walivaa kofia za chuma na vazi la chuma. Askari wa miguu walivaa joho linalovuka magoti kwenda chini, suruali na viatu. 41 Silaha zao zilikuwa mikuki, midogo midogo, majambia, pinde, mshale na ngao. Kila askari alikuwa akinunua vifaa vyake na wale wasioweza walinunuliwa na serikali. Vifaa vingine vilivyotumika wakati huo ni Manjaniq, 42 Dababa 43 na Zaboor.44 Idara ya ulinzi ilipoanzishwa askari wote waliorodheshwa na utaratibu wa mshahara na posho ulianza kutumika kwa askari wa kudumu, wakujitolea na wale waliopigana vita vya awali kama Badr, Uhud, n.k., walipewa posho. Kiulinzi nchi iligawiwa kwenye maeneo ya kiulinzi, makao makuu ya maeneo hayo yakawa Madina, Kufa, Basra, Mosul, Fustat, Damaskas, Hems. Jordan na palistine.45 Katika sehemu zote hizi kambi zilijengwa kwa ajili ya askari. Mashamba ya mifugo yalipanuliwa kwa matumizi ya farasi na ngamia wa vita. Pamoja na askari wa farasi na wa miguu jeshi la maji lilianza wakati wa ukhalifa wa uthman. Vita vya kwanza vya majini vilipiganwa na Muawiya alipoivamia Cyprus mnamo mwaka wa 28 A.H. Makao makuu ya jeshi la maji yalikuwa Alexandria Misri. Wanamaji wa Kiislamu walisaidia kuimarisha ulinzi wa dola ya Kiislamu. Usalama wa Taifa na ujasusi Idara hii nayo ilikuzwa. Ilianza tangu wakati wa Mtume (s.a.w.) na kuendelezwa wakati wa makhalifa wanne. Walitumika wanajeshi na wasio wanajeshi katika kazi ya kupata habari ndani na nje ya Dola na hasa kujua mwenendo wa adui. Wapo Machief kwa mfano Syria waliochagua wana usalama wao kuchunguza mwenendo wa Warumi. Wapalestine lilikuwepo kundi la Wayahudi lililojulikana kwa jina la Samara, lililojizatiti katika upelelezi. Khalifa Umar aliweka wapelelezi ndani ya jeshi ili apate habari zote. Hivyo idara hii nayo ilisaidia sana katika ulinzi na usalama wa Dola wa kiislamu. Hivi ndivyo serikali ya Kiislamu ilivyoendeshwa - kwa ufupi Serikali
ya Kiislamu iliyoendeshwa kwa muda wa miaka 40 kuanzia kwa Mtume (s.a.w.)
hadi makhalifa wake wanne iliweka misingi ya uendeshaji wa serikali zote
za leo Duniani. Pamoja na kubadili misingi lakini mambo mengi yameazimwa
kutoka katika misingi ya Serikali ya Kiislamu
|
YALIYOMO
Tahariri
Urambo wamlilia Profesa Lipumba
Sheikh aridhia Waislamu
kubatizwa
Uongozi Masjid Qadiria waitwa Polisi kuhojiwa Wakazi wa Mbagala Msalabani kuishitaki Tume ya Jiji Akhera ipo, makafiri ni wakadhibishaji
Mdahalo kati ya Waislamu na
Wakristo ni mgumu
Aina ya maudhi yaliyoharamishwa juu ya Muislamu PAROLE: Rais kasusa
au hana ubavu?
Serikali ikithamini kilimo
Umuhimu wa Elimu ya Awali kwa watoto
wadogo - 3
Madrasa Arrijalu Muswallin Damba Ijue Madrasat Fauzia - Kibondo Waislamu Kondoa waanza
kupokea misaada ya ujenzi wa Msikiti, Madrasa
Waislamu Dodoma wasali sala ya Ghaib kwa marehemu Kilima na mkewe Songea kujenga shule ya sekondari Wanafunzi wa Bihawana Dodoma wamshukuru Alhaj Ismail Dawood Mashindano ya kusoma Qur’an yafanyika Kondoa Waislamu wautazame upya mfumo wao wa elimu Ujenzi wa Chuo cha Kiislamu Shamsiya Bereko wakwama Kesi ya kushambulia kituo yaahirishwa tena Polisi waondolewa kimya kimya Mwembechai Msikiti wa Kiwanja cha Ndege wapania kujenga shule Sayansi na Teknolojia
Chakula na lishe
|