|
|
|
Madrasatul Arrijalu Muswallin Damba ipo nyumbani kwa mlezi wa madrasa hiyo Mzee Hashim Khamisi nyumba nambari 29 mtaa wa Chem Chem Magomeni Mapipa wilaya ya Kinondoni mkoa wa Dar es Salaam. Madrasa hii ilianzishwa na Maustadhi watatu nao ni Ust. Ali Musa, Ust. Seif Mubaraka na Ust. Hashim Khamisi. Madrasa ilianzishwa mwaka 1972 ikiwa na wanafunzi wasiozidi 27, wasichana kwa wavulana. Madrasa hii ni maarufu sana kwa wakazi wa maeneo hayo kutokana na kazi nzuri zinazofanywa na walimu ya kuwafundisha wanafunzi wa Kiislamu masomo ya dini yao. Kipindi hicho chote walikuwa bado hawana mwalimu mkuu, ilipofika mwaka 1974 wakaongezeka walimu wawili mmoja aitwaye Khamis Bakari Kazaliwa ambaye alikuwa mwalimu mkuu na Ali Abdulrahman Kaumbe ni mwalimu msaidizi. Ilipofika mwaka 1994 Sheikh Kazaliwa aliaga dunia na wakati huo huo akaongezeka mwalimu mwingine aitwaye Hakim Maalim toka Buguruni ndiye aliyeshika nafasi ya marehemu Kazaliwa. Mwaka 1996 wakaongezeka walimu watatu nao n Ust. Kaisari, Ust. Mwamba na Ust. Abbasi Khamisi, hawa hawakukaa muda mwingi ilipofikia mwaka 1997 mwishoni wakaondoka walimu wote akabakia Mzee Hashimu Khamis pekee na wanafunzi wake. Hivi sasa madrasa imekamatwa na Ust. Hassani Aboubakari Minchum ambaye ni mwalimu mkuu na Ust. Musa Ally ambaye ni mwalimu msaidizi, mpaka hivi sasa madrasa ina wanafunzi 60 wasichana kwa wavulana. Madrasa hii ina viongozi wa kuiongoza nao ni Omar (Kipipa) ambaye ni Katibu na msaidizi wake ni Zuberi Kassim na Hashim Khamis ambaye ni Mwenyekiti na msaidizi wake ni Musa Ally. Masomo yanayotolewa madrasani hapo ni Qur’an tukufu pamoja na tafsiri yake, Hadith za Mtume Muhammad (s.a.w.), Fiqh na mengi mengineyo yanayohusiana na dini yenyewe. Madrasa hii ina madrasa kongwe ambayo imetoa baadhi ya madrasa hapa Tanzania pia ina mpango wa kusajiliwa na serikali ya Kabidhi Wasii Mkuu. Upo utaratibu ambao umewekwa na walimu hao pamoja na viongozi wa madrasa kuwa kila mzazi atoe shilingi 300 kila baada ya mwezi mmoja ili kuweza kuwasaidia walimu hao pesa za matumizi yao binafsi. Hata hivyo, wazazi hao wamekuwa wanatoa sana pesa kwa matatizo yaani mpaka uwafukuze watoto wakati wa masomo wakachukue pesa ya ada, hayo yalisemwa na mwalimu mmoja wa madrasa hiyo. Pia madrasatul Arijalu Muswallin Damba ipo katika harakati za kusherehekea Maulidi ya kuzaliwa Mtume Muhammad (s.a.w.) Desemba 5, mwaka huu (sawa na mwezi 15 Shaaban mwaka 1419). Wito umetolewa na walimu wote wa madrasa kuja kusherehekea Maulidi hayo.
Muasisi wa Madarasat Fauzia ni muadhamu Mzee Zakuani Athman ambaye ni mhamia kutoka Kigoma. Amehamia Kibondo kwenye miaka ya 50. Kwenye miaka hiyo Mzee Zakuan alikuwa ni muumini tu kwani shughuli zake kubwa zilikuwa siasa na biashara ndogo ndogo. Mzee Zakuan pia ni muasisi wa chama cha TANU Wilayani Kibondo. Kati ya miaka ya 1958-1975 uendeshaji wa elimu ya dini hapo Kibondo ulikuwa wa wasiwasi mpaka kwenye miaka ya 70 ufundishaji ulilala kabisa. Waalimu waliokuwa wanakuja walikuwa hawakai kwa kipindi kirefu labda pengine kwa vile kulikuwa hakujakuwepo mwamko wa kidini. Madarasat za nyakati hizo zilikuwa hazipati wanafunzi zaidi ya 5; ambao nao mahudhurio yalikuwa si ya kuridhisha. Hali hiyo ilichangia katika kuwakatisha tamaa waalimu ambao walikuwa wanafundisha kwa kujitolea. Ilikuwa ni rahisi mwalimu kujiondokea ikiwa mahudhurio yamesimama au kama ameitwa kwingine kwenye maslahi. Maalim ambaye anakumbukwa kati ya waalimu waanzilishi ni Sheikh Nasibu ambaye kwa hivi sasa yuko Mwandiga, Kigoma Vijijini. Bado anaendeleza ujuzi wake huo. Ilipofika mwaka 1975 Mzee Zakuan ambaye alikuwa ameanza kujiengua katika medani ya siasa aliamua atumie muda wake mwingine katika kuendeleza Quran Tukufu kwa njia ya kusimamia ufufuaji wa Madarasat Fauzia. Mzee Zakuan amekuwa jirani sana na Masjid Kibondo ambamo ndimo imo Madarasat Fauzia. Amekuwa Bilal wa Msikiti huo kwa kipindi chote hicho ingawa hivi sasa utu nzima umepunguza kasi za ukakamavu wake. Katika kufufua Madarasat Fauzia mwaka 1975, mwalimu wa kwanza kupatikana alikuwa Ustadh Iliasi Said Bulyo. Ustadh Iliasi alifundisha kwa kipindi cha miaka 5 yaani hadi 1980. Chuo kilibaki hakina mwalimu kwa muda wa miaka mitatu (3).Kuanzia 1983 hadi 1991 chuo kilimpata maalim Khuraidin ambaye mara tu alipoondoka 1991 nafasi yake ilichukuliwa na Ustadh Khalfan Maulid. Naye Ustadh Khalfan aliachia ngazi miaka miwili baadaye yaani 1993. Desemba 1993 alipatikana maalim Zaidi Ahmad Khamis ambaye hadi sasa ndiye analiongoza jahazi hilo. Chuo hicho ambacho hivi sasa kina zaidi ya wanafunzi 40 ambao hufundishwa Quran Tukufu, Tafsiri, Lugha, Hadith, Fiqh na Sira kinakabiliwa na tatizo la kutokuwa na vitendea kazi; haswa vitabu. Ufundishaji ama unamtegemea mwalimU na vitabu vyake vya rejea au kuazimana vitabu kwa uchache mkubwa. Kutokana na tatizo hilo, chuo kinatoa kilio kwa wahisani/wafadhili kujitolea kutuma vitabu vya Quran Tukufu (misahafu); Majuzu, Lugha Juzu 1-14, Mabaduil Fiqh juzu 1-4, Muhtasar Swaghir, Durarul Bahiyah, Vitabu hivyo akabidhiwe Ustadh Swaleh N.A. Kassera, Katibu Mkuu, TAMPRO, S.L.P. 80, Iringa. Madarasat Fauzia iko mbioni kutafuta nafasi za masomo ya juu kwa vijana wenye bidii na uwezo. Nia na madhumuni ni kuandaa kikosi cha wanataaluma wazawa ambao watatarajiwa kurudi nyumbani ili kushiriki katika harakati za upanuzi wa dini ya Kiislamu. Sadaqa kwa Masjid Kibondo, Kigoma. Msikiti huo ni wa kwanza kujengwa Wilayani Kibondo mjini lakini hadi sasa haujakamilika. Ombi linatolewa kwa waumini, wahisani na wafadhili watoe sadaqa ili kukamilisha yafuatayo:- (1) Kujenga darasa kwa ajili ya Madarasat Fauzia.
Mpokeaji: Ustadh Swaleh N.A. Kassera,
Na Abu Zubeir, Dodoma WAISLAMU wa kijiji cha Dalai wilayani Kondoa wameanza kupokea misaada ya fedha na vifaa vya ujenzi wa Msikiti na Madrasat toka kwa wafadhili mbalimbali mjini Dodoma. Akithibitisha kupatikana kwa misaada hiyo, Katibu wa Kamati ya Ujenzi wa Msikiti na Madrasat Dalai, Ustadh Rashid Ramadhani aliwataja miongoni mwa wafadhili waliotoa vifaa na fedha taslimu kuwa ni Bw. Khalifa Abdallah (Hongera) ambaye alitoa mifuko 10 ya saruji, Sheikh Abdallah Ally bin Ahmed wa Masjid Qubaa bati 20, Bw. Athmani Twaja (Yarabi Salama) mifuko 10 ya saruji. Wengine ni Dk. Majala 10,000/-, Mustafa Tundu 5,000/-, Hamza Issa 5,000/-, Alhaj Hamisi Lubuva 10,000/-, Bw. Kimaro Juzuu 10 na Hamisi Nkunya boksi 5 za chaki, penseli 40 na madaftari 100. Masjid Dalai pamoja na Madrasa yake yamekadiriwa kugharimu shilingi milioni 11 pale ujenzi huo utakapokamilika. Ustadh Rashid alisema mbali na vifaa hivyo, hatua nyingine iliyofikia ni pale mafundi wawili ambao wamejitolea kujenga majengo hayo mawili bila malipo. Msikiti wa awali uliopo kijijini hapo ni wa matofali yasiyo chomwa na umeezekwa kwa nyasi na unaweza kuswaliwa na watu 25. Ni azimio la Waislamu wa Dalai kumalizia ujenzi wa Msikiti na kuswaliwa
mapema iwezekanavyo kabla ya mwezi wa Ramadhani kuandama.
|
YALIYOMO
Tahariri
Urambo wamlilia Profesa Lipumba
Sheikh aridhia Waislamu
kubatizwa
Uongozi Masjid Qadiria waitwa Polisi kuhojiwa Wakazi wa Mbagala Msalabani kuishitaki Tume ya Jiji Akhera ipo, makafiri ni wakadhibishaji
Mdahalo kati ya Waislamu na
Wakristo ni mgumu
Aina ya maudhi yaliyoharamishwa juu ya Muislamu PAROLE: Rais kasusa
au hana ubavu?
Serikali ikithamini kilimo
Umuhimu wa Elimu ya Awali kwa watoto
wadogo - 3
Madrasa Arrijalu Muswallin Damba Ijue Madrasat Fauzia - Kibondo Waislamu Kondoa waanza
kupokea misaada ya ujenzi wa Msikiti, Madrasa
Waislamu Dodoma wasali sala ya Ghaib kwa marehemu Kilima na mkewe Songea kujenga shule ya sekondari Wanafunzi wa Bihawana Dodoma wamshukuru Alhaj Ismail Dawood Mashindano ya kusoma Qur’an yafanyika Kondoa Waislamu wautazame upya mfumo wao wa elimu Ujenzi wa Chuo cha Kiislamu Shamsiya Bereko wakwama Kesi ya kushambulia kituo yaahirishwa tena Polisi waondolewa kimya kimya Mwembechai Msikiti wa Kiwanja cha Ndege wapania kujenga shule Sayansi na Teknolojia
Chakula na lishe
|