|
|
Katika mahojiano yaliyofanyika kituoni hapo ilidaiwa kwamba kuna muhadhara wa kashfa unaokashifu dini nyingine katika msikiti huo na pia muhadhara huo unachanganya dini na siasa. Waumini walikanusha madai hayo na kusema kwamba muhadhara huo unatangaza dini ya Kiislamu kwa kusoma vitabu vinne vya Allah (s.w.). Kuhusu kuchanganya dini na siasa waumini hao waliiomba Polisi kabla ya yote iwathibitishie kama nchi hii ni ya Kikristo au la kwa sababu wimbo wa Taifa ni wimbo wa Kikristo uliomo katika kitabu cha Kikristo kiitwacho "Chuo kidogo cha sala na nyimbo, wimbo huo umo katika ukurasa wa 86 katika kitabu hicho", walidai huku wakionyesha hicho kitabu, na kuongeza kwamba, pia dua ya kuliombea Bungeni dua ya Kikristo ambayo imo katika ukurasa wa 12 wa kitabu hicho hicho. Kutokana na hali hiyo mashtaka yalibadilishwa
likaja shtaka la kufanya muhadhara bila kibali. Waumini hao waliachiwa
huru kwa sharti kwamba wakitoka kuendelea na muhadhara watafute kibali
hata kama ni msikitini kutokana na sababu za kiusalama.
Wakazi wa Mbagala Msalabani kuishitaki Tume ya Jiji BAADHI ya wakazi wa eneo la Mbagala Msalabani huenda wakaishitaki Tume ya Jiji kwa madai ya kuwaingilia katika makazi yao na kuweka alama za kubomolewa nyumba bila ridhaa zao; na makubaliano. Kutokana na maelezo kamili ya baadhi ya wahusika wa maeneo hayo wakazi hao wanatakiwa kuhama makazi hayo kwa sababu imedaiwa ni mali ya Kanisa Katoliki (Catholic Secretariat) jambo ambalo wakazi hao wanalipinga. Wamesema kuwa, kuwepo kwa Msalaba katika eneo lao sio sababu ya kuwa si eneo lao, na kuwa ni mali ya "Catholic Secretariat", kwani Msalaba huo umekuwepo tangu mwaka 1932, zama za Wajerumani. Baadae eneo lilirudishwa kwa serikali katika miaka ya 1960. Baada ya Uhuru Serikali ililirudisha eneo hilo na kwamba wakazi hao walikuwa wanapatumia kama bustani. Wakazi hao wa sasa wanasema kuwa wao wapo hapo kwa muda mrefu . Wamesema kwamba Kanisa limeanza kufuatilia eneo hilo tangu mwaka 1994 na kuanza kazi ya upimaji wa viwanja hivyo. walipohojiwa ni kwa nini wanachukua hatua ya kuishtaki Tume ya Jiji muda huu na si tokea mwanzo wa mgogoro huo walisema kuwa mwanzo walikutana na uongozi na kuahidiwa kupatiwa fidia, lakini cha ajabu ni kwamba mpaka hii leo hawajapewa chochote wala viwanja. "Tumeandikiwa barua ya kutuamuru kuondoka, katika eneo hili bila ya kuonyeshwa wapi pa kwenda", walisema. Aidha, walidai kwamba waliambiwa wafuatilie malipo pamoja na viwanja kwa Mkurugenzi wa Jiji wa Kanda ya Temeke lakini kila wakifuatilia anasema ana kazi nyingi. Pia wakazi hao wamedai kwamba walifika kwa Afisa Ardhi Wilaya Temeke ambaye aliwajibu kuwa yeye hana nakala ya kuwaamuru waondoke na kuwaambia waende Makao Makuu ya Jiji wamuone alie waandikia barua hiyo. Eneo hilo lenye mgogoro linakaliwa na Waislamu watupu na kuna madrasa
na miti ya Matunda (miembe, midizi n.k.).
|
YALIYOMO
Tahariri
Urambo wamlilia Profesa Lipumba
Sheikh aridhia Waislamu
kubatizwa
Uongozi Masjid Qadiria waitwa Polisi kuhojiwa Wakazi wa Mbagala Msalabani kuishitaki Tume ya Jiji Akhera ipo, makafiri ni wakadhibishaji
Mdahalo kati ya Waislamu na
Wakristo ni mgumu
Aina ya maudhi yaliyoharamishwa juu ya Muislamu PAROLE: Rais kasusa
au hana ubavu?
Serikali ikithamini kilimo
Umuhimu wa Elimu ya Awali kwa watoto
wadogo - 3
Madrasa Arrijalu Muswallin Damba Ijue Madrasat Fauzia - Kibondo Waislamu Kondoa waanza
kupokea misaada ya ujenzi wa Msikiti, Madrasa
Waislamu Dodoma wasali sala ya Ghaib kwa marehemu Kilima na mkewe Songea kujenga shule ya sekondari Wanafunzi wa Bihawana Dodoma wamshukuru Alhaj Ismail Dawood Mashindano ya kusoma Qur’an yafanyika Kondoa Waislamu wautazame upya mfumo wao wa elimu Ujenzi wa Chuo cha Kiislamu Shamsiya Bereko wakwama Kesi ya kushambulia kituo yaahirishwa tena Polisi waondolewa kimya kimya Mwembechai Msikiti wa Kiwanja cha Ndege wapania kujenga shule Sayansi na Teknolojia
Chakula na lishe
|