AN-NUUR
Na.164 Jamada Awal 1419, Agosti 28 - Septemba 3, 1998
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
Chakula na lishe

Hatari ya kumnyonyesha mtoto maziwa ya kopo


 


Na Mujahiid Mwinyimvua

KATIKA makala yetu ya chakula na lishe ya wiki iliyopita tulijifunza faida zinazopatikana endapo mtoto atanyonyeshwa maziwa ya mama (breast-feeding). Makala hiyo ilikusudiwa kuongeza nguvu ya uhamasishaji kwa kina mama na jamii kwa ujumla ili wawanyonyeshe watoto wao maziwa ya mama.

Vilevile makala hiyo ililenga kuwabadili mawazo mabaya waliyopandikiziwa kina mama ya kupenda kuwanyonyesha watoto wao maziwa ya kopo (bottle – feeding).

Kwa vile teknolojia ya maziwa ya kopo (bottle-feeding) imeleta maafa makubwa kwa watoto wadogo hasa katika nchi za Magharibi (walioanza kuitumia teknolojia hiyo), na kwa vile kuna baadhi ya kina mama bado wanaendelea kuwanyonyesha watoto wao maziwa ya kopo, nimeonelea katika makala hii kuendeleza juhudi za kuwahimiza kina mama kuwanyonyesha watoto wao maziwa ya mama. 

Nitafanya kazi hiyo katika makala yetu ya wiki hii kwa kutazama hatari ya kuwanyonyesha watoto maziwa ya kopo.

Awali ya yote, watu wakumbuke kuwa maziwa ni chakula kizuri kwa afya na binadamu. Lakini jambo hilo lisichukuliwe juu juu hasa tunapomtazama mtoto mdogo, mwenye umri chini ya miaka miwili. Kwa maneno mepesi ninaweza kusema kwamba, kunyonyesha mtoto mwenye umri chini ya miaka miwili maziwa ya kopo ni jambo la hatari kama ninavyoligusia kidogo hapa chini.

Mara nyingi watoto wanaonyonyeshwa maziwa ya kopo (bottle-feeding) hupata maambukizo (infections). Jambo hili liantokana na ukweli kwamba maziwa ya kopo hayana kinga kama yalivyo maziwa ya mama.

Pia uandaaji wa maziwa ya kopo (mfano maji yanayotumika) na chupa ya kunyonyeshea mtoto huwa ni sababu nyingine inayochangia watoto wanaonyonyeshwa maziwa ya kopo kupata maambukizi (mwili kuingiliwa na vijidudu vya maradhi).

Sababu nyingine inayochangia maambukizi ni kuwa, maziwa ya kopo baada ya kuandaliwa huweza kuingiwa na vijidudu vya maradhi wakati yamehifadhiwa katika joto la kawaida, kama hili la Dar es Salaam.

Hatari nyingine inayoweza kupatikana kwa kuwanyonyesha watoto maziwa ya kopo ni kuwa watoto wanaweza kuwa na lishe duni, jambo hili linasababishwa na mambo kadhaa, baadhi yake ni haya yafuatayo:

Kwanza, maziwa ya kopo hayana virutubisho vyote vinavyotakiwa kwa ukuaji na maendeleo ya mtoto. Pili, maziwa ya kopo ni aghali. Hivyo watu wengi hushindwa kumpatia mtoto kiasi cha maziwa kinachohitajika na mwili wake. 

Matokeo ya hayo yote ni kuwa mtoto ana kuwa na lishe duni (yaani mwili haupati virutubisho vyote na kwa kiasi kinachotakiwa).

Zaidi ya hayo, maziwa ya kopo yanaweza kuleta hatari inayojulikana kwa kimombo kama "Allergies". Haya ni matatizo ya kiafya ambayo yana dalili nyingi kama vile kuumwa kichwa, tumbo, kupata mafua na kikohozi cha muda mrefu.

Tukizingatia yote tuliyoyaona katika makala hii na yale ambayo hayakuandikwa, ninaimalizia makala yetu kwa kuwahimiza kina mama na jamii kwa ujumla kwamba, tujitahidi kadiri tunavyoweza kuwanyonyesha watoto wetu maziwa ya mama.

Kwa maneno mengine tujitahidi kadiri tunavyoweza kuwa mbali na utamaduni angamizi wa kuwanyonyesha watoto wetu Lactogen na mengineyo ya kopo.
 

Juu

YALIYOMO

TAHARIRI: Dawa ya ugaidi si kufanya ugaidi ndani ya ugaidi

Bakwata yalaani ubabe wa Marekani
Na Mwandishi Wetu

Wanakijiji wawapiga Polisi Olesiva
Na Mwandishi wetu, Arusha

Waislamu washinda kesi Same
Na Mwandishi Wetu, Same

Wasafiri ATC wadai ndege ya Jeddah inahujumiwa 
Na Mwandishi Wetu

KOSOVA: Bosnia nyingine

Mahojiano kati ya CNN na Bwana Usama bin Ladin

Historia ya damu za mashujaa Afghanistan

Msikiti wa Wagoma Kigoma wapata viongozi wapya
Na Suleiman Simba, Kigoma

Muhadhara wanguruma Masjid Hijaz
Na Said Shariff

Waislamu waitumie Misikiti ipasavyo
Na Ashraf Yusuph, Moshi

Mpango wa kudhibiti uzazi utawaangamiza wengi
Na Mwandishi Wetu

Hoja za kutofautisha Yesu na Issa ni udhaifu,  ni uzushi mtupu! - 3
Na Muhibu Said

Wanawake wa Kiislamu washiriki maonyesho ya kilimo
Na Habiba Swedi

Wanawake wa Kiislamu washauriwa kupigania haki zao
Na Habiba Swedi, Arusha

Africa Muslims Agency: Inavyohudumia jamii
Na Mwandishi Wetu

Kitengo cha Zakkah chasafirisha wanafunzi
Na Mwandishi Wetu

Kupinga kifo cha Yesu ni kumpinga Mungu?
Mahfudhi M. Mahfudhi

MAONI: Porojo za Ngatara -2

Zanzibar na  biashara ya utumwa
Na J. Hussein

Marekani ishitakiwe
Na Abubakar Msham

MAPENDEKEZO YA KATIBA YA SHIRIKISHO LA TANZANIA - 3

Mafundisho ya Quran

Barua za wasomaji

Mashairi

Masomo ya dini ya Kiislam

Chakula na Lishe
 
 
 
 
 
 

 

 Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org

Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita