|
Na.164 Jamada Awal 1419, Agosti 28 - Septemba 3, 1998 |
|
Na Mwandishi Wetu AFRICA Muslims Agency (AMA) ni shirika la kutoa huduma kwa jamii lisilo la Kiserikali (NGO) ambalo limesajiliwa nchini toka mwaka 1987. Shirika hili ni mwanachama hai wa Baraza la Maendeleo ya Jamii Tanzania (TACOSODE) na kamati ya kitaifa inayotoa misaada wakati wa maafa (TANDRED). Shughuli za AMA zina lenga kuboresha huduma za jamii na maendeleo kupitia miradi yake ya elimu, afya na misaada ya kibinadamu. Awali, shirika hili lilianzishwa kama taasisi ya kuwasaidia Waislamu wa Malawi mwaka 1982, baada ya madaktari fulani kutoka Kuwait kuitembelea nchi hiyo na kushuhudia hali mbaya iliyokuwa ikiwakabili Waislamu. Baada ya kufanya kazi kwa miaka miwili kwa jina la Malawi Muslim Agency, shirika hilo lilipanua malengo yake na kuitazama Afrika kwa ujumla. Jina lilibadilika na kuwa Africa Muslims Agency ambapo hivi sasa lina ofisi na matawi 40 katika nchi mbalimbali za Afrika. Kwa Tanzania, ofisi kuu ipo Jijini Dar es Salaam eneo la Tabata wakati matawi ya ofisi hiyo yapo Moshi, Tanga, Zanzibar, Morogoro, Mwanza na Mtwara. AMA ina idara nne ambazo ni elimu, afya, huduma za jamii na programu za dharura. Chini ya idara ya elimu kuna shule za sekondari za Alfarooq (Dar es Salaam), Kaloleni (Moshi) na Kitaya (Mtwara). Aidha, kwa mwaka 1999 zinatarajiwa kufunguliwa sekondari nyingine kadhaa ambazo ni Alkheir Centre (Mkwakwani Tanga) na An-nuur Centre (Pongwe, Tanga). Alkheir itakuwa kwa ajili ya wasichana na wanawake watu wazima (mafunzo ya ufundi) wakati ile ya Pongwe itakuwa kwa wavulana. Shule nyingine itafunguliwa Mji Mpya Morogoro. Pamoja na shule hizo, vipo vituo 5 vya kutoa mafunzo ya ufundi kwa akina mama. Aidha, imefunguliwa "College" ijulikanayo kama Al-Shariah College huko Zanzibar ambayo imefungamanishwa na Chuo Kikuuu cha Madina. Lengo ni kuifanya Al-Shariah kuwa Chuo Kikuu kamili katika miaka michache ijayo. Chini ya idara ya afya kuna zahanati kadhaa zinazofanya kazi wakati nyingine zipo mbioni kufunguliwa. Zanahati zinazofanya kazi ni pamoja na Al-Molhem Medical Centre (Tanga) Kaloleni Health Centre na Prince Saud Medical Centre. Juhudi zinafanyika katika kuziendeleza zahanati na vituo hivyo vya afya kufuata maadili mema ambapo wanawake wana sehemu za kupatiwa huduma tofauti na wanaume huduma zikiwa sawa kwa wote. Kituo cha Prince Saud ambacho kipo katika eneo la shule ya Al-Farooq kitafanya kazi kwa masaa 24 kikiwa na huduma za kawaida na "Ultra Sound Clinic" na huduma za "Marternity" na MSH. Idara hii muhimu ya afya ikiongozwa na Dk Rashed E. Hamed inaendesha kambi za matibabu ya macho bure ambapo upasuaji hufanyika na miwani kutolewa bure. Kufikia mwisho wa mwaka huu 1998 AMA inatarajia kuwa na vituo 10 vya afya. Kwa upande wa huduma za jamii, AMA inaendesha vituo kadhaa vya kulelea yatima vyenye watoto wapatao 250. Watoto hao hupewa chakula, malazi, mavazi,matibabu na zaidi husomeshwa hadi mwisho wa uwezo wao (sekondari au Chuo Kikuu). Pamoja na watoto wanaokaa katika nyumba rasmi za kulelea yatima wapo watoto zaidi ya 100 ambao husaidiwa chakula na mavazi wakiwa katika familia zao. Chini ya kitengo hiki hutolewa pia misaada ya chakula na nguo katika maeneo yenye shida ya njaa na wakati wa maafa. Aidha, husaidia kuchimba visima vya maji katika maeneo yenye shida ya maji na zaidi ya visima 600 vishachimbwa katika maeneo mbalimbali nchini. Pamoja na shughuli zote hizi, Africa Muslims Agency huwasadia waumini kujenga Misikiti. Misikiti ipatayo 50 nchini. Wakati wa maafa kwa kushirikiana na TANDREC, AMA hushiriki
kikamilifu kutoa misaada na huduma zinazohitajika kuokoa maisha ya watu.
|
TAHARIRI: Dawa ya ugaidi si kufanya ugaidi ndani ya ugaidi Bakwata yalaani ubabe wa Marekani
Wanakijiji wawapiga Polisi
Olesiva
Waislamu washinda kesi Same
Wasafiri ATC wadai ndege ya Jeddah
inahujumiwa
Mahojiano kati ya CNN na Bwana Usama bin Ladin Historia ya damu za mashujaa Afghanistan Msikiti wa Wagoma Kigoma wapata
viongozi wapya
Muhadhara wanguruma Masjid
Hijaz
Waislamu waitumie Misikiti
ipasavyo
Mpango wa kudhibiti uzazi utawaangamiza
wengi
Hoja za kutofautisha Yesu na Issa
ni udhaifu, ni uzushi mtupu! - 3
Wanawake wa Kiislamu washiriki
maonyesho ya kilimo
Wanawake wa Kiislamu washauriwa
kupigania haki zao
Africa Muslims Agency: Inavyohudumia
jamii
Kitengo cha Zakkah chasafirisha wanafunzi
Kupinga kifo cha Yesu ni kumpinga
Mungu?
Zanzibar na biashara ya utumwa
Marekani ishitakiwe
MAPENDEKEZO YA KATIBA YA SHIRIKISHO LA TANZANIA - 3
|
Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua kwa: webmaster@islamtanzania.org