|
Na.164 Jamada Awal 1419, Agosti 28 - Septemba 3, 1998 |
|
Na Muhibu Said Utume Bw. Augustine anasema, Qur’an inasema Isa alipewa Injili ili kuja kuhakikisha yale yaliyokuwa kabla yake na kuisaidikisha Torati (Almaida 46). Biblia inasema Yesu alikuja hapa duniani kutafuta na kuokoa kilichopotea (Luka 19:10). Ndani ya Qur’an hakuna aya yoyote inayozungumzia kuwa Isa alikuja kuleta wokovu, je, hii si tofauti nayo? Mwisho wa kunukuu. Wakristo waelewe kwamba siyo lazima Qur’an Tukufu itaje wazi kwamba Nabii Isa alikuja kuleta wokovu kama Bw. Augustine anavyodai hapo juu. Kwa hali hiyo, hatuwezi kusema kwamba Bwana Yesu alikuja kuruhusu watu wamle nguruwe eti kwa vile hakusema wazi "msile nyama ya nguruwe", kama ilivyokatazwa na Mwenyezi Mungu (s.w.t.) katika Torati ya Musa. Lakini ni dhahiri kuwa kule kusema kwake tu kwamba "msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua Torati wala Manabii, ila sikuja kutangua, bali kutimiliza" (Mathayo 5:17) kulitosha kuonyesha msisitizo na mkazo wa uharamu na unajisi wa kula nyama ya nguruwe kama ulivyotajwa wazi katika Torati (Kumbukumbu la Torati 14:8). Kwa mantiki hiyo, kule kuja kwake (Yesu au Isa (a.s.) kuhakikisha yale yaliyokuwa kabla yake na kuisadikisha Torati kama Qur’an Tukufu inavyoeleza inatosha kukubali kwamba alikuja kuwaokoa waliopotea zama zake, ambao waliiweka kando miongozo sahihi ya Manabii wa kabla yake (Yesu au Isa) na Torati. Kwani inajulikana wazi kwamba Manabii na Torati waliokuwepo kabla ya Yesu au Nabii Isa hawakutumwa na Mwenyezi Mungu kuwatakia binadamu shari. Ila kuwatakia nusura (wokovu) mbele ya Mwenyezi Mungu siku ya mwisho (kiama) (Qur’an 2:213). Na ndio maana Yesu akakana kuwatengua, yaani kuwapinga Manabii na Torati (Mathayo 5:17). Ni dhihiri alijua kazi na lengo la Mwenyezi Mungu kuwaleta (Luka 16:16-17). Pamoja na ukweli huo, lakini wokovu mkubwa alioleta Nabii Isa au Yesu (a.s.) ni ule wa kuonyesha matokeo ya ushirikina, kama ule wa kumfanya na yeye kuwa ni Mungu pamoja na Mwenyezi Mungu (s.w.t.) aliyemtuma. Ambapo ni kinyume kabisa na mwenyewe alivyofundisha (tazama Marko 12:29). Alisema mtu huyo (anayemshirikisha Mwenyezi Mungu) Mwenyezi Mungu ameharamishia pepo na makazi yake ni motoni (5:72). Kwa kweli huu hakika ndio wokovu mkubwa na wa kwanza aliouleta Nabii Isa. Kwani ni wazi kuwa maovu mengine yote chanzo chake kikuu ni shirki (kutomjua Mwenyezi Mungu vilivyo) (Ayubu 22:21). Kwa mantiki hiyo, ni dhihiri kuwa Yesu na Isa ni yule
yule mmoja aliyeleta wokovu kwa wana wa Israeli kama Qur’an na Biblia vinavyofundisha
(Qur’an 3:49 na Mathayo 15:24).
Matendo yake Katika kipengele hiki, Bw. Augustine anasema "Isa alipozaliwa tu alianza kuongea na kusema kuwa yeye ni mja wa Mwenyezi Mungu na amepewa kitabu na kufanywa Nabii (19:30-33). Biblia haielezi juu ya Yesu kutamka neno lolote siku ya kuzaliwa kwake." Mwisho wa kunukuu. Ni kweli Biblia haikueleza lolote juu ya Yesu kuongea siku aliyozaliwa. Na haijulikani ni kwanini tukio zito na muhimu kama hilo lisigusiwe na Biblia! Hata hivyo, napenda kumfahamisha Bw. Augustine kwamba si hilo tu liliachwa kuandikwa ndnai ya Biblia lakini Bwana Yohana anatumbia kuwa: "Kuna na mambo mengine mengi aliyoyafanya Yesu; ambayo yakiandikwa kwa moja kwa moja nadhani hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa" (Yohana 21:25). Kwa kauli hiyo ya Mwinjilisti Yohana inatosha kumwondoa wasiwasi Bw. Augustine iwapo atapata alililofanya Yesu au Isa (a.s) ndani ya Qur’an Tukufu ambalo halimo ndani ya Biblia Takatifu. Kwa kuwa litakuwa katika orodha ya mambo ambayo yalihofiwa kuandikwa moja kwa moja kama anavyotueleza Yohana ndani ya Biblia hapo juu. Kwa hali hiyo, hoja hiyo haiwezi kutofautisha Yesu na Isa. Bw. Augustine anaendelea kusema "Qur’an inasema Isa alitabiri habari za kuja Ahmad (Muhammad (61:6). Biblia inasema yeye ndiye "mwanzo na mwisho" hakuna mwingine tena (Ufunuo 21:6). Vile vile Yesu aliahidi kutuletea Roho Mtakatifu atakayedumu nasi milele (Yohana 14:14). Wala siyo Muhammad ambaye hakudumu milele. Mwisho wa kunukuu. Kwa bahati mbaya Bw. Augustine katika kudai kwamba Bwana Yesu ndiye "Mwanzo na mwisho" amenukuu kitabu cha ufunuo wa Yohana. Hakujua kwamba mafundisho na miongozo ya kitabu hicho inawahusu Wayahudi peke yao. Na yeyote aliyejifanya kuwa ni Myahudi wakati siye, kitabu hicho kilimshutumu kwamba anatokana na kundi (sinagogi) la shetani. (Tazama Ufunuo 2:9). Kwa hiyo, kitabu hicho kuwatoa wasiokuwa Wayahudi kunadhihirisha kuwa Bwana Yesu au Nabii Isa (a.s) ni "Mwanzo na mwisho" kwa Wayahudi. Ni wa "mwanzo" kwa Wayahudi kwa kuzaliwa bila ya baba (Luka 1:34-35) na ni wa "mwisho" kwa Wayahudi kwa kuwa baada ya yake haji tena Mtume mwingine kwa ajili ya nyumba ya Israeli (Mathayo 21:33-34). Kuhusu huyo Roho Mtakatifu aliyetabiriwa na Yesu bado
ni Nabii Muhammad (s.a.w) kwa kuwa lipo sharti moja muhimu alilolitaja
Bwana Yesu la kuondoka kwanza yeye (Yesu) ndipo huyo msaidizi mwingine
aje. Na Mtume Muhammad (s.a.w) alitumwa na Mwenyezi
Itaendelea toleo lijalo
|
TAHARIRI: Dawa ya ugaidi si kufanya ugaidi ndani ya ugaidi Bakwata yalaani ubabe wa Marekani
Wanakijiji wawapiga Polisi
Olesiva
Waislamu washinda kesi Same
Wasafiri ATC wadai ndege ya Jeddah
inahujumiwa
Mahojiano kati ya CNN na Bwana Usama bin Ladin Historia ya damu za mashujaa Afghanistan Msikiti wa Wagoma Kigoma wapata
viongozi wapya
Muhadhara wanguruma Masjid
Hijaz
Waislamu waitumie Misikiti
ipasavyo
Mpango wa kudhibiti uzazi utawaangamiza
wengi
Hoja za kutofautisha Yesu na Issa
ni udhaifu, ni uzushi mtupu! - 3
Wanawake wa Kiislamu washiriki
maonyesho ya kilimo
Wanawake wa Kiislamu washauriwa
kupigania haki zao
Africa Muslims Agency: Inavyohudumia
jamii
Kitengo cha Zakkah chasafirisha wanafunzi
Kupinga kifo cha Yesu ni kumpinga
Mungu?
Zanzibar na biashara ya utumwa
Marekani ishitakiwe
MAPENDEKEZO YA KATIBA YA SHIRIKISHO LA TANZANIA - 3
|
Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua kwa: webmaster@islamtanzania.org