|
Na.164 Jamada Awal 1419, Agosti 28 - Septemba 3, 1998 |
|
Wakati iliyokuwa Jamhuri ya Muungano wa kisovieti (USSR), ikivamia Afghanistan, Akhtar Khan, aliyekuwa mkuu wa idara ya usalama ya Pakistan (ISI), alitoa ushauri kwa Rais Zia Ul Haq ulioitaka Pakistan kusaidia vita vya msituni, vilivyokuwa vikiendeshwa na makundi ya Mujahidiin dhidi ya majeshi hayo ya uvamizi na vibaraka wake nchini Afghanistan. Kufuatia ushauri huo makachero wa Serikali ya Pakistan walianza kupenyezwa ndani ya urusi ambao kwa kusaidiana na vikosi vya mujahidiin, walifanya hujuma kadhaa dhidi ya vituo vya kijeshi sambamba na kushambulia miji ya Urusi iliyopo mpakani na Afghanistan. Aidha Pakistan chini ya Generali Zia iliendesha mafunzo ya kijeshi kwa wapiganaji wa kiislamu waliojitolea kuingia msituni kupambana na madhalimu hao wa kirusi wakisaidiana na vibaraka wao. Hata hivyo wakati Mashambulizi dhidi ya adui yakiendelea kushika kasi, Nchini Pakistan msiba mkubwa ulitokea. Ilikuwa yule yule mfadhili wa Wapiganaji hao, Rais Zia Ul Haq na mshauri wake wa mambo ya usalama bwana Akhtar Khan, walioripotiwa kufariki dunia katika ajali ya ndege iliyotokea wakati kiongozi huyo akiwa katika ziara ya kikazi ndani ya Pakistan. " Ndege ya Jeshi la Anga la Pakistan C-130 ikiwa imemchukua Rais Generali Zia na baadhi ya maafisa wa ngazi za juu wa jeshi ililipuka angani na kuua wote waliokuwemo", amendika Brigedia Muhammad Yousaf mmoja wa washiriki wa vita vya Afghanistan katika kitabu chake Afghanistan’s untold story. Ulikuwa msiba mkubwa kwa makundi ya Mujahiidin hawa wachanga, wasio na uzoefu wowote wa vita, kulinganisha na nguvu ya kutisha iliyokuwa mkabala nao. Mauaji ya Generali Zia yalipangwa na majasusi wa CIA na KGB kwa kumtumia bwana Aslam Beg, mtu aliyekuja kushika uongozi mara tu baada ya kifo cha Rais Zia Ul Haq. Ili kuukanganya Ulimwengu, mauaji hayo yaliwajumuisha waambata wawili wa kijeshi wa Marekani ambao walikufa sambamba na Generali Zia katika mlipuko huo. Kutoka Marekani Maafisa wa FBI walitumwa "kuchunguza" sababu na chanzo cha mlipuko huo wa ndege uliosababisha pamoja na watu wengine, waambata wake wa kijeshi kupoteza maisha! Hata hivyo, pengine kwa kuwa na taarifa rasmi ya kadhia hiyo FBI haikujishughulisha kabisa na kuwahoji walioshuhudia tukio hilo. " Wingu lililozingira mauaji hayo lilitokana na ukweli kwamba Marekani ilikuwa na mkakati tangu awali wa kudhibiti Mujahidiin wasiweze kusimamisha serikali ya kiislamu nchini Afghanistan ingawa ilijitia kuwa nao bega kwa bega kuwafurusha warusi", anafafanua Brigedia Yousaf katika moja ya kurasa za kitabu chake. Kuuawa kwa Generali Zia kulikuwa ni hitimisho la njama kadhaa zilizofanywa dhidi ya kiongozi huyo. Njama ya mwanzo ilipangwa na Mkuu wa majeshi wa Urusi wakati huo, ambaye aliona kuwa kazi ya kudhibiti Mujahidiin ingechukuwa muda mrefu iwapo ngome yao kuu( Pakistan) haitasambaratishwa. Mkuu huyo alisuka njama kuipindua serikali ya Rais Zia Ul Haq kutokea Urusi. Alituma makachero nchini Pakistan kutega mabomu katika maduka, ndege za abiria, kuyauzia silaha ki magendo makabila yaliyokuwa yakiishi mpakani mwa nchi hizo mbili na kuchochea migawanyiko, kero zote hizo zililenga kuwaghadhibisha Wananchi wa Pakistan dhidi ya serikali ya Generali Zia hatimaye ipinduliwe. Harakati hizi hazikufanikiwa. Kifo cha Rais Zia Ul Haq kilitoa ishara ya mapambano magumu na ya muda mrefu mbeleni yaliyokuwa yakiwakabili Mujahidiin, kwani kuchanganyikiwa kwao kulikotokana na kifo hicho kulitoa mwanya kwa Majeshi ya adui yakiwa na zana nzito nzito huku yakipata msaada wa Najibullah na vibaraka wenzake waliokuwa wakiiongoza nchi hiyo, kujichimbia barabara ndani ya Afghanistan. Wataalamu wa masuala ya kijeshi walilielezea jaribio la Mujahidiin kutaka kupambana na Taifa hilo kubwa likiwa limejikita sawa sawa ndani ya Afghanistan, kwamba ni kichekesho cha karne hii, na isingechukuwa hata miezi mitatu kabla hawajasagiliwa mbali. Katika hali hiyo ya ukiwa Idara ya usalama ya ISI ikipigana nyuma ya Mujahidina, ilibeba jukumu la usafirishaji na usambazaji wa silaha na misaada mingine ya fedha na chakula kwa wapiganaji (logistics). Misaada hiyo ilitoka kwa Wahisani mbali mbali ikiwemo serikali ya Saudi Arabia. Pasipo uratibu wa upiganaji, mipango wala mbinu madhubuti, Mujahidiin hawa wachanga walitumia silaha kufanya mashambulizi ya kushtukiza katika ngome za majeshi ya adui. Hata hivyo mashambulizi yao yalijibiwa vikali na adui kiasi cha kusababisha hasara kubwa ya mali na maisha ya watu. Mtihani mwingine uliojitokeza katika kipindi hiki kigumu, ni ule wa migogoro ya viongozi wa makundi ya wapiganaji. badala ya kusonga mbele kumkabili adui, viongozi wa makundi walianza kunyoosheana vidole hadi kufikia kuyapambanisha makundi yao katika vita ya wenyewe kwa wenyewe. Nusra ilijitokeza pale makundi hayo yalipoketi na kurejea Qur’an, hatua
iliyopelekea kuundwa shuura iliyounganisha makundi saba ya Mujahidiin yaliyokuwa
msituni wakati huo.
Itaendelea toleo lijalo
|
TAHARIRI: Dawa ya ugaidi si kufanya ugaidi ndani ya ugaidi Bakwata yalaani ubabe wa Marekani
Wanakijiji wawapiga Polisi
Olesiva
Waislamu washinda kesi Same
Wasafiri ATC wadai ndege ya Jeddah
inahujumiwa
Mahojiano kati ya CNN na Bwana Usama bin Ladin Historia ya damu za mashujaa Afghanistan Msikiti wa Wagoma Kigoma wapata
viongozi wapya
Muhadhara wanguruma Masjid
Hijaz
Waislamu waitumie Misikiti
ipasavyo
Mpango wa kudhibiti uzazi utawaangamiza
wengi
Hoja za kutofautisha Yesu na Issa
ni udhaifu, ni uzushi mtupu! - 3
Wanawake wa Kiislamu washiriki
maonyesho ya kilimo
Wanawake wa Kiislamu washauriwa
kupigania haki zao
Africa Muslims Agency: Inavyohudumia
jamii
Kitengo cha Zakkah chasafirisha wanafunzi
Kupinga kifo cha Yesu ni kumpinga
Mungu?
Zanzibar na biashara ya utumwa
Marekani ishitakiwe
MAPENDEKEZO YA KATIBA YA SHIRIKISHO LA TANZANIA - 3
|
Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua kwa: webmaster@islamtanzania.org