|
Na.164 Jamada Awal 1419, Agosti 28 - Septemba 3, 1998 |
|
Porojo za Ngatara -2
Hivi karibuni vyombo vya habari vimepasha kwamba kijana mmoja wa Kiislamu alikamatwa na polisi huko mjini Korogwe na kufunguliwa mashtaka kwa kuandika katika baiskeli yake kuwa Yesu si Mungu. Ni nini tafsiri ya kitendo hiki? Tafsiri yake ni kuwa kwa mujibu wa serikali (jeshi la polisi ni idara nyeti na muhimu katika serikali) Yesu ni Mungu! Bila shaka msimamo huu ni wa kutia mashaka makubwa kwa serikali inayojitangaza kuwa haiongozwi na dini yoyote. Msimamo huu wa serikali umetiliwa nguvu na yaliyojiri katika mhadhara mkubwa ulioendeshwa hivi karibuni Jijini na Mwinjilisti wa Kijerumani Rainhard Bonke ambao pia ulihudhuriwa na baadhi ya watu mashuhuri wakiwamo Makamu wa Rais Dk. Omari Ali Juma, mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Lt. Yusuph Makamba na mke wa Waziri Mkuu Bibi Esther Sumaye. Katika mhadhara huo tulibwagizwa kwa mapana na marefu kuwa Yesu ni Mungu wa Tanzania Sio tu kwamba tangazo hili lilionekana kutokuwa na walakini wowote, bali lilipata baraka zote za serikali pale serikali ilipousifia mhadhara huo na kuutaja kama unaofaa kuigwa. Sasa ni nini tunachokisoma kutoka kwenye mifano kama hii? Ni dhahiri kuwa kwa mtu yeyote ambaye atajishughulisha kutafakari na atokee kuwa na bahati ya kutoathiriwa na mafumbo ya imani, atafikia hitimisho kuwa kinachotokea ni kujaribu kulazimisha hatua kwa hatua - kwa kutumia dola, izoeleke na kukubalika hadharani kuwa Yesu ni Mungu na kwa wale ambao hawakubaliani na swala hilo walazimike kuwaonyesha msimamo huo sirini na mafichoni tu. Tujaalie, kama Bwana Ngatara anavyoamini kuwa Tanzania ni kisiwa cha amani na kuwa serikali ya Tanzania haijifungamanishi na dini yoyote - iwe wazi wazi au kwa siri. Aidha tujaalie kuwa kila Mtanzania ana uhuru kamili wa kuamini na kuabudu kupitia dini anayotaka. Pamoja na kujaalia hayo yote bado Bwana Ngatara anatokea kuwa na ufinyu mkubwa wa utambuzi kwa kule kudai kwake kuwa ni mambo haya yanayoiwezesha Tanzania kubakia ni ‘kisiwa cha amani ndani ya bara linalokabiliwa na misuguano na migongano ya hatari ya kila aina?! Kwanza ni muhimu Bwana Ngatara akatambua kuwa msisitizo kwenye kauli yake unatoa picha potofu kuwa ni bara hili pekee ambalo kwa kiasi kikubwa linakabiliwa na migogoro na migongano. Ukweli wenyewe ni kwamba migogoro na migongano iko katika mabara takriban yote. Kwa mfano tu, Ulaya inakabiliwa na migogoro hivi sasa huko Ireland ya Kaskazini, Serbia-Kosovo, Belaruss,Ukraine, Hispania, na Cyprus. Huko Amerika ya Kusini wapiganaji wa Shinning Path wanaleta dhahama katika nchi za Peru, Colombia na Bolivia wakati kule Amerika ya Kaskazini wapiganaji wa Zapatista wanacharushana na serikali ya Mexico. Huko Asia nako ukiondoa mashariki ya kati bado kuna Syrilanka, Afghanistan, Jammu - Kashmir, Burma, Cambodia, Indonesia - Timor Mashariki, na bila ya kusahau hali ya kivita isiyokwisha kati ya Korea Kusini na Korea Kaskazini. Pili, tukirejea barani Afrika ni mgogoro au mgongano hivi sasa upi ambao asili yake ni sera inayotoa kipaumble katika dini? Bila shaka Bwana Ngatara na wenzake kwa kuwa wamekaririshwa hivyo na kwa kuwa hawana uwezo wa kujua mchele ni upi na pumba ni zipi katika yale wanayoyasikia watakimbilia kuitaja migogoro inayoendelea hivi sasa kule Algeria na Sudan. Chanzo cha mgogoro wa Algeria
kinajulikana vema. Chama cha Kiislamu cha FIS kilipata ushindi kwenye uchaguzi
na ushindi huo ukaporwa na Madhalimu. Kwa kuwa ni haramu kwa Muislamu Muumini
kudhulumu au kukubali kudhulumiwa, basi FIS ikawapasa kufanya kile walichopaswa
kufanya. Walichokifanya FIS na wanachoendelea hakitofautiani na kinachotokea
hivi sasa nchini Togo. Hivi majuzi muungano wa vyama vya upinzani nchini
humo umeanzisha mapambano ya silaha dhidi ya serikali ya Rais Gyadema ambaye
na chama chake walidhulumu ushindi katika uchaguzi mkuu uliopita. Suala
la Sudan naloliko wazi. Mgogoro kati ya waasi wa kusini mwa nchi hiyo na
serikali umeanza mara tu baada ya uhuru katika miaka ya hamsini. Mgogoro
huo katika sura yake ya kileo umeanzishwa na John Garang na waasi wenzake
mnamo mwaka 1983 kabla kabisa ya kuingia madarakani kwa serikali ya Kiislamu
inayoingoza nchi hiyo hivi sasa chini ya Generali Hassan El Bashr. Sasa
katika mnyumbulisho huu suala la dini linaanzia wapi?
Insha Allah tutaendelea katika toleo lijalo.
|
TAHARIRI: Dawa ya ugaidi si kufanya ugaidi ndani ya ugaidi Bakwata yalaani ubabe wa Marekani
Wanakijiji wawapiga Polisi
Olesiva
Waislamu washinda kesi Same
Wasafiri ATC wadai ndege ya Jeddah
inahujumiwa
Mahojiano kati ya CNN na Bwana Usama bin Ladin Historia ya damu za mashujaa Afghanistan Msikiti wa Wagoma Kigoma wapata
viongozi wapya
Muhadhara wanguruma Masjid
Hijaz
Waislamu waitumie Misikiti
ipasavyo
Mpango wa kudhibiti uzazi utawaangamiza
wengi
Hoja za kutofautisha Yesu na Issa
ni udhaifu, ni uzushi mtupu! - 3
Wanawake wa Kiislamu washiriki
maonyesho ya kilimo
Wanawake wa Kiislamu washauriwa
kupigania haki zao
Africa Muslims Agency: Inavyohudumia
jamii
Kitengo cha Zakkah chasafirisha wanafunzi
Kupinga kifo cha Yesu ni kumpinga
Mungu?
Zanzibar na biashara ya utumwa
Marekani ishitakiwe
MAPENDEKEZO YA KATIBA YA SHIRIKISHO LA TANZANIA - 3
|
Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua kwa: webmaster@islamtanzania.org