|
Na.164 Jamada Awal 1419, Agosti 28 - Septemba 3, 1998 |
|
MIAKA michache iliyopita vyombo vya habari vilitanda habari za kuuliwa, kuteswa na kuvunjwa kwa haki za binadamu, kunyanyaswa Waislamu huko Bosnia ndani ya Ulaya iliyostaarabika. Wakati machungu, majeraha na makovu ya Waislamu bado hayajakauka; Kosova imegeuzwa kuwa Bosnia nyingine; Waislamu wanachinjwa na makazi yao kuangamizwa kwa kutamka kwao Shahada. Warsebia wanaopiga miji na vijiji vya Waislamu huko Kosova kwa mabomu wakiua Waislamu wasio na hatia kwa maelfu hawana haki yoyote juu ya eneo hilo kama ambavyo Wacroats na Waserbia kwa pamoja hawakuwa na haki juu ya Waislamu wa Bosnia. Halikadhalika, kama ambavyo Wayahudi wasivyo na haki juu ya Wapalestina na Wahindu juu ya wananchi wa Kashmir. Kosova ina watu wapatao milioni 2.2 ambapo asilimia 90 ni wa asili ya Albania Wakatoliki wakiwa asilimia 5 na waliosalia wakiwa Waislamu. Waserbia wapatao asimilia 10 ya wananchi wa Kosovo wakisaidiwa na Waserbia wa Serbia (Yugoslavia) wanataka kuwadhibiti Waislamu na ikiwezekana kuwasafisha wote. Mbinu zinazotumika ni kupiga mabomu miji na vijiji ili watu wakimbie. Kuchoma moto nyumba ili waliokimbia baada ya mabomu wasirejee, kuwaua wanaume mbele ya macho ya wanawake na watoto ili watakaposilimua unyama huo, asitamani yeyote kurejea Kosova. Kuwanajisi wanawake mbele ya wanaume na watoto. Ili yote hayo yasijulikane hivyo kutolaaniwa vyombo vya habari na wanadiplomasia wamekuwa kana kwamba wanazuiwa katika kusema ukweli juu ya mauaji hayo ya kuangamiza. Historia fupi ya Kosova: 1300 BC: Wahenga wa Waalbania wajulikanao kama Illyraina walihamia Balkans. Karne ya sita AD: Makundi mbalimbali ya Waslav na Wahenga wa Waserbia walihamia Balkans. 1180 AD: Stefan Nemanj aliunda taifa la awali la Muugano la Waserbia. 1389: Waserbia walishindwa na jeshi la Waislamu wa Uturuki (Ottoman). Kuanzia hapo Waseribia wakajenga chuki kali dhidi ya Waturuki na Waislamu. 1459: Kosova ikawa jimbo katika ‘Ottoman Empire’ 1912-13: Vita vya Balkan. Waserbia wakashinda katika maeneo mengi ya Serbia. 1939: Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Waalbania wa Kosovo wakaasi dhidi ya utawala wa Serbia. 1946: Muungano wa nguvu za Urusi, Ufaransa na Uingereza iliunganisha kwa nguvu Kosovo na Serbia. Kosovo ikabaki chini ya utawala wa Kikomunisti wa Serbia. 1974: Mamlaka haba yalitolewa kwa Kosovo. Milosevic akiwa kiongozi wa chama cha Kikomunisti cha Serbia aliingia madarakani kwa kutumia kampeni za chuki dhidi ya Waalbania. 1990: Milosevic alifuta mamlaka ya watu wa Kosovo, na kuwatenza nguvu chini ya utawala wa kijeshi na kuvunja haki zao zote za kiraia. Juni 25, 1991: Slovenia na Croatia yalikuwa majimbo ya awali kujitangazia uhuru toka Yugoslavia. Oktoba, 1991: Kosova ilijitangazia uhuru. 1992: Macedonai na Bosnia nazo zikajitangazia uhuru toka Yugoslavia. 1992: Waserbia wakaanza mauaji ya maangamizi dhidi ya Waislamu wa Bosnia. Agosti, 1992: Yakagunduliwa makambi ya kuwatesea na kuwabaka Waislamu. Julai, 1995: Majeshi ya Serbia yakakamata mji wa Srebrenica maelfu ya Waislamu wanaume na vijana wakauliwa. Umoja wa Mataifa haukuingilia. Novemba, 1995: Baada ya Waislamu kuelekea kushinda NATO ikaingilia kati na kulazimisha mkataba wa Dayton (The Dayton Accords). 1995: Dk. Ibrahimu Rugova kwa kutumia demokrasia ya kura alichaguliwa kuwa Rais wa Kosovo. Marekani ikapinga na kutaka asitambuliwe. 1997: Jeshi la ukombozi wa Kosova (Kosova Liberation Army - KLA ) likaanzishwa. 1998: Waserbia wakaanza kuwachinja watoto na wanawake katika kijiji
cha Dremica ikifuatiwa na mauaji ya kuangamiza sawa na yale ya Bosnia.
|
TAHARIRI: Dawa ya ugaidi si kufanya ugaidi ndani ya ugaidi Bakwata yalaani ubabe wa Marekani
Wanakijiji wawapiga Polisi
Olesiva
Waislamu washinda kesi Same
Wasafiri ATC wadai ndege ya Jeddah
inahujumiwa
Mahojiano kati ya CNN na Bwana Usama bin Ladin Historia ya damu za mashujaa Afghanistan Msikiti wa Wagoma Kigoma wapata
viongozi wapya
Muhadhara wanguruma Masjid
Hijaz
Waislamu waitumie Misikiti
ipasavyo
Mpango wa kudhibiti uzazi utawaangamiza
wengi
Hoja za kutofautisha Yesu na Issa
ni udhaifu, ni uzushi mtupu! - 3
Wanawake wa Kiislamu washiriki
maonyesho ya kilimo
Wanawake wa Kiislamu washauriwa
kupigania haki zao
Africa Muslims Agency: Inavyohudumia
jamii
Kitengo cha Zakkah chasafirisha wanafunzi
Kupinga kifo cha Yesu ni kumpinga
Mungu?
Zanzibar na biashara ya utumwa
Marekani ishitakiwe
MAPENDEKEZO YA KATIBA YA SHIRIKISHO LA TANZANIA - 3
|
Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua kwa: webmaster@islamtanzania.org