AN-NUUR
Na.164 Jamada Awal 1419, Agosti 28 - Septemba 3, 1998
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
Kitengo cha Zakkah chasafirisha wanafunzi

Na Mwandishi Wetu

TAASISI ya Kiislamu; Tanzania Islamic Centre (T.I.C) yenye makao makuu Magomeni Mapipa Jijini imewasaidia kwa kuwasafirisha vijana saba waliobahatika kupata nafasi za masomo nchini China.

Akiongea kwenye tafrija fupi ya kuwaaga vijana hao iliyofanyika katika ofisi za Tanzania Muslim Hajj Trust mtaa wa Kipata, Katibu Mkuu wa kitengo cha Zakkah Sheikh Jabri alisema kwamba TIC kupitia kitengo chake cha Zakkah kimeamua kuchukua jukumu la kuwapitia Waislamu mbalimbali baada ya serikali kushindwa kuwasafirisha vijana hao.

Alisema gharama ya kuwasafirisha vijana hao kwenda masomoni nchini China ni takriban dola za Kimarekani mia nane na sitini na tano (865) kwa kila mmoja.

Akitoa shukrani zake kwa niaba ya wazazi wa vijana hao, Mzee Ally Omar Ally alisema ni mara nyingi nafasi kama hizi pengine hutokea lakini kutokana na hali ngumu ya kimaisha nafasi hizo huishia kwa watu ambao sio waliokusudiwa kwa hiyo amewataka Waislamu kuunga mkono kitengo hicho cha Zakkah ili vijana wao wakwamuke na udhalili.

Naye Mwenyekiti wa kitengo cha Zakkah, Sheikh Nurudin Hussein akitoa nasaha zake kwa vijana hao aliwaasa wasije wakafanya mambo yaliyo kinyume na maadili ya dini yao wawapo huko ugenini, kwani kufanya hivyo ni sawa na kuudhalilisha Uislamu.

Alisema Uislamu ni dini ya heshima na nidhamu na kwamba Waislamu ndio wanaowatuma kwenda huko na matarajio yao kwamba watavuna mavuno mazui kama walivyotarajia.

Akipokea nasaha hizo, mmoja wa vijana hao kwa niaba ya wenzake, aliahidi kulinda heshima na maadili ya Uislamu na kwamba wanajua kwamba wao ni tegemeo kubwa kwa Waislamu kutokana na ujuzi watakaoupata huko.

Vijana hao ambao wanakwenda kuchukua kozi tatu tofauti katika kiwango cha juu cha Chuo Kikuu ni Mohamed Mwinyimvua, Ligile Mahamoud Vumilia na Shaabani Ally Likonda wanakwenda kuchukua mafunzo ya udaktari kwa kipindi cha miaka sita. 

Wengine ni Haruna Said Luguluke, Kenguka Mohamed Kenguka pamoja na Omari Ally ambao watachukua sayansi ya kompyuta (computer) kwa kipindi cha miaka mitano.

Mwingine ni Mbaraka Mohamed anayekwenda kuchukua sayansi ya mazingira naye pia kwa muda wa miaka mitano.

Vijana hao wameondoka kwa ndege ya Gulf Air Agosti 25, 1998 kupitia Muscut hatimaye Shaghai nchini China.

Wakati huo huo Mkurugenzi wa Mult Travel Agency, Bw. Rajan ametoa punguzo maalum kwa wasafiri wa kwenda Umra. 

Akiongea katika hafla hiyo amesema gharama za kwenda na kurudi zitakuwa dola za Kimarekani 450 pia amesema gharama hizo ni nje ya gharama nyingine za kawaida.
 

Juu

YALIYOMO

TAHARIRI: Dawa ya ugaidi si kufanya ugaidi ndani ya ugaidi

Bakwata yalaani ubabe wa Marekani
Na Mwandishi Wetu

Wanakijiji wawapiga Polisi Olesiva
Na Mwandishi wetu, Arusha

Waislamu washinda kesi Same
Na Mwandishi Wetu, Same

Wasafiri ATC wadai ndege ya Jeddah inahujumiwa 
Na Mwandishi Wetu

KOSOVA: Bosnia nyingine

Mahojiano kati ya CNN na Bwana Usama bin Ladin

Historia ya damu za mashujaa Afghanistan

Msikiti wa Wagoma Kigoma wapata viongozi wapya
Na Suleiman Simba, Kigoma

Muhadhara wanguruma Masjid Hijaz
Na Said Shariff

Waislamu waitumie Misikiti ipasavyo
Na Ashraf Yusuph, Moshi

Mpango wa kudhibiti uzazi utawaangamiza wengi
Na Mwandishi Wetu

Hoja za kutofautisha Yesu na Issa ni udhaifu,  ni uzushi mtupu! - 3
Na Muhibu Said

Wanawake wa Kiislamu washiriki maonyesho ya kilimo
Na Habiba Swedi

Wanawake wa Kiislamu washauriwa kupigania haki zao
Na Habiba Swedi, Arusha

Africa Muslims Agency: Inavyohudumia jamii
Na Mwandishi Wetu

Kitengo cha Zakkah chasafirisha wanafunzi
Na Mwandishi Wetu

Kupinga kifo cha Yesu ni kumpinga Mungu?
Mahfudhi M. Mahfudhi

MAONI: Porojo za Ngatara -2

Zanzibar na  biashara ya utumwa
Na J. Hussein

Marekani ishitakiwe
Na Abubakar Msham

MAPENDEKEZO YA KATIBA YA SHIRIKISHO LA TANZANIA - 3

Mafundisho ya Quran

Barua za wasomaji

Mashairi

Masomo ya dini ya Kiislam

Chakula na Lishe
 
 
 
 
 
 
 
 

 

 Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org

Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita